Status
Not open for further replies.

Feld Marshal Tantawi

JF-Expert Member
Dec 24, 2014
609
1,007
Hili suala la Bandari naona baadhi yenu mmelibeba katika namna fulani ya UDINI, kila nikimuangalia kiongozi wangu wa KIISLAM akisimama mahali analizungumzia katika upande wa UDINI.

Sikilizeni, TEC imejaa watu wenye ELIMU kuanzia ya Elimu Dunia hadi elimu ya DINI (THEOLOJIA), ndo maana utasikia Askofu Dr, Eng, Prof fulani fulani wa Parokia fulani. Sisi ukishamqliza kusoma Quran umemaliza, mengineyo ni majungu. Yaani mtu kama Prof Lipumba alitakiwa awe Imamu wa Msikiti fulani mahali fulani na kiongozi fulani katika nafasi za Bakwata taifa, lakini matokeo yake kule tumewaweka wengine. Sisemi kwamba waislam hatujasoma, hapana, PhD zilizopo katika nafasi za uongozi misikitini ni chache mno kulinganisha na wenzetu.

Ndo maana linapofikia jambo la kuongea na kiongozi mkuu wa nchi, hawa TEC, KKKT na mengineyo utaona utofauti, sisi runaomba kupunguziwa ama kuondolewa kodi za TENDE na kuomba tupatiwe VIFAA vya kisasa vya KUUTAZAMA MWEZI mtukufu. Wenzetu wanaomba mismaha ya kodi ya makontena ya vifaa tiba, vifaa vya elimu na mengineyo. Sisi tukishakunywa juisi za tende Ikulu tunashukuru na kuondoka na kushika shikashika videvu kama SUNNAH, tunaondoka.

Leo tunawaona TEC wabaya katika msimamo, mali zetu wenyewe tunashindwa kuzisimamia wenyewe, hapa Kinondoni nadhani kidogo tupigwe na wachache kwenye eneo letu ambalo Bakwata ipo. Tumshukuru Hayati Magufuli (Mkristo) alitusaidia na kutuombea msaada wa kujengewa Msikiti.

Kuna namna nawatazama viongozi kama wanafki, na mnafki siku zote maendeleo kwake yanakawia. Najua huu ujumbe mchungu na mnaweza hata kuitisha kikao mkanisomea ALBADIRI. Ndio, TEC wametoa WARAKA wenye HOJA, mbona hamzikosoi HOJA zao mnajikita katika UDINI? Kwani huu mkataba unaopingwa nyinyi hamkwenda IKULU pamoja nao kabla ya huu waraka? Mlienda kufanya nini? Si mlipeleka mapendekezo ya marekebisho?

Mbona leo mnasita kusema kwamba mlikuwa pamoja? UNAFKI mtupu! Ndo maana katika viongozi wa kidini namkubali Sheikh Nurdin Kishki, Mziwanda, Mazinge na Dr Sulle. Hawa hawana manenomaneno, kazi yao ni kutoa DAGH'AWA tu. Huu unafki nafki umebaki kwa wasiotambua wajibu wao. Kuna shule nyingi za kiislam, matokeo yake ni mabovu. Hatuangalii kuboresha shule zetu, tumekazana kuvaa kanzu na misuli kuzodoana. Tuache Unaa. Astaghafirulah!

Mmenikwaza sana. Kuna huo Sheikh mmoja amesema yeye atasambaza waraka wa kuunga mkono nchi nzima kama tamko la msikiti, huyu hasababishi UDINI, hachochei Udini? Nani katika Uislamu amemuonya aache huo ujinga?

Mnahitaji semina! Mnahitaji kujitokeza na tamko lenye mashiko la aidha kwa nini mnaunga mkono ama mnapinga huu mkataba na muwe na sababu za kujitosheleza. Msijitokeze kwa sababu TEC wametoa WARAKA, mnatengeneza mashindano na mtachochea vurugu zisizo na msingi wowote.

Tuache UDINI, huu mkataba haupingwi kwa sababu ulisainiwa Msikitini au mbele ya imamu na wala huu mkataba hauhusiani na msikiti kwa maana DP World hawaji kujenga misikiti wala kueneza Quran. Wanakuja kuwekeza katika bandari zetu. Tukipinga tupinge kwa hoja na tukikubali tukubali kwa hoja. Tunahitaji kueleweshana, inawezekana mimi sijaelewa na pengine akijitokeza mtu akanielewesha nitamuelewa na nitaunga mkono lakini ukitumia UDINI sintokuelewa. Maana naona kila anaesimama anasema "NYUMA YA PAZIA"; hiyo nyuma ya pazia kwenye ule waraka hiyo "NYUMA YA PAZIA " iko wapi?

Asalaam alaykum!
 
Umeongea ukweli,, ukweli mtupu,, Ndugu zangu mashehe,,Toeni pointi Kwa Nini mnaupinga Au kwanini tunaukubari,, Lakini Kila anayeongea anaongea pumba tuuu.

Yule DP world ni mfanyabiashara Siyo mtangaza Dini,,Ni Mwarabu mfanya Biashara Siyo Mwarabu Dini,, Kiongozi anapokuwa kiongozi Ana Dini yake.

Pale anapokuwepo anatekereza masuala ya Watu Wote Siyo ya Dini Fulani, Tukiibiwa twaibiwa Wote,, Wote twateseka.

Please leteni pointi Watu wanatudharau Sasa.
 
Hili suala la Bandari naona baadhi yenu mmelibeba katika namna fulani ya UDINI, kila nikimuangalia kiongozi wangu wa KIISLAM akisimama mahali analizungumzia katika upande wa UDINI...

Ingekuwa bakwata ina watu wa5 kama wewe hakika makubwa mazuri yangetendeka,tatizo ni boko haramu wamejaa kuanzia ngazi ya familia hadi bakwata. Wabadilike kwa kweli.

Inshu ya bandari wajadili vipengele vya mkataba na sio mapadri na ukatoliki.
 
IMG-20230823-WA0028.jpg
 
Wewe waseme na hata uwatukane BAKWATA hakuna tatizo ...Usitaje waislamu hao BAKWATA sio nguzo za uislamu hao ni tawi la CCM na wanajiingiza kweny siasa moja kwa moja hata kuwatetea wenzao waliofungwa kimya.

Waislamu wanasoma elimu za wamesoma sana ila hawanaga mambo ya kishabiki sijui taasisi kama BAKWATA hao nI branch ya CCM.

Hakuna muislamu anaendeshwa kwa matamko ya BAKWATA ...

Hkuna muislamu asome eti aache kutumia taaluma yake akakusanye sadaka na kuwashikia akili wengine ndo lipumba huwezi kumkuta kweny taasisi za dini hata nyie ,ukiwa chini ya taasisi kuna asilimia ndogo ya kutumia akili yako zaidi itakuwa kupingana na kufuata matamko ya watu bila ya kupenda.

Hilo ni bifu lako na BAKWATA kama una hakika hawajasoma ni sawa maana mimi hata huyo kiongozi wao simjui wa BAKWATA ,kama wamepiga majungu bora useme wapi wamepiga .

Nyuma ya pazia watu wana bifu zao kama wanadamu kabisa .
 
Huku Mitaani wale wakatoliki wanaouza soksi mitaani, wanaoendesha boda boda, mama ntilie, ma house girls , ma jobless n.k wananufaika vipi na hiyo miakili na mikakati ya Viongozi wao wa kiimani?

nafananisha na Mwa CCM fukara anaemtambia Mwana Chadema fukara kwa kumtajia miradi inayomilikiwa na Chama chake wakati huo wanabishania kuchangia umeme wa elf 5 umeisha kwny kijumba wanachopanga kila mtu na chumba chake

au ndio kama zile mbwembwe za Waarabu koko wa Ilala kukutajia Anko zake walioko Oman na London wakati tukiwa kwny foleni ya kusubiria Mihogo ya kukaanga tukanywe chai na Familia zetu au kwny vijiwe vya bhangi?
 
Ndio maana huwa nawakubali sana waislamu unamkuta hata kama amesoma huwezi kumuona akijimwambafai.

Mimi binafsi nimesaidiwa sana na waislamu wengi mtaa ninaokaa wana uwezo kifedha kiukweli sijawahi kuoneshwa dharau wala haya majigambo na kujisifu.

Wenzetu wamejaliwa utulivu na hekima hata kama ana pesa. Njoo sasa kwa kina samweli mtu hela kidogo anataka apigiwe magoti mpaka na vichaa. Shenzi sana.
 
Kazi kweli kweli
 
Hapa point ya msingi ni
Kila anaunga mkono mkataba wa bandari, akubali kwa hoja zake na kuwatangazia wafuasi wa kundi lake.

Kila anaye kataa mkataba akatae kwa hoja zake na kuwatangazia wafuasi wa kundi lake.

Viongozi wa makundi mbalimbali wawe kama walivyofanya Wahashamu wetu, kama walivyofanya chadema na wengine km wale walioenda mahakamani, lakini sio kama mzee wa upako, au baadhi ya watu wanaopinga waraka wa TEC kwa hoja tofauti na mkataba wa bandari...

Mungu wabariki Watanzania
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom