Naweza kujenga nyumba kwa TZS Milioni 20?

tumia toali za kuchoma tofali 8000 ni tzs 800,000
mafundi tzs 2000,000
mbao tzs 2000,000
cement mifuko 100 tzs 1,500,000
umeme 3,000,000
finishing +rangi 7,000,000
milango na madirisha 4,000,000
chenji inabaki

finishingi ya 7m ni ya kitu gani au anasiliba mavi ya ngombe ukutani ndo iwe plaster!!!!!
 
Ngoja tuone! Kwa 'nyumba ya kawaida' na kwa 'ujenzi wa kawaida' rate per sq m sio chini ya tzs 500,000. Kwa nyumba ya vyumba 4 (vya say 4mx3m) inaweza kuwa na square metre 57.6 (i.e. 4mx3mx4rooms+20% circulation). So gharama inaweza kuwa kama 57.6x500,000=28,000,000. Labda kama vyumba hiyo unavijenga kama 'fremu' za maduka (fremu nne), lakini kama unakusudia nyumba hiyo 20m haitoshi!
 
kwenye red ume inflat sana. mil 20 unaweza kujenga bwana wasikudanganye watu uka[poteza pesa zako ila sasa inabidi use,me nyuma isiyo na decorations maana ukizungumzia decorations inaweza fika mil 100.

Kwa kuwa kiwanja unacho millioni 20 mbona unahamia kwenye nyumba lakini finishing hutamaliza. Angalia mgawanyo wa gharama ( I assume uko Dar es Salaam na nyumba unayojenga ni ya mtu anayejenga nyumba yake ya kwanza):
  1. Matofali 5,000 @700=TZS3,500,000
  2. Mafundi (kujenga toka msingi mpaka kuezeka)=4,000,000/=
  3. Cement mifuko 150 @15,000=2,250,000/=
  4. Mbao zote TZS4,000,000/=
  5. Bati 60 @ 15,000=900,000/=
  6. Fundi umeme na vifaa vyake=5,000,000/=
  7. Finishing (madirisha na milango)=5,000,000/=
  8. Finishing (plastering + ceiling works)=5,000,000/=
 
Ngoja tuone! Kwa 'nyumba ya kawaida' na kwa 'ujenzi wa kawaida' rate per sq m sio chini ya tzs 500,000. Kwa nyumba ya vyumba 4 (vya say 4mx3m) inaweza kuwa na square metre 57.6 (i.e. 4mx3mx4rooms+20% circulation). So gharama inaweza kuwa kama 57.6x500,000=28,000,000. Labda kama vyumba hiyo unavijenga kama 'fremu' za maduka (fremu nne), lakini kama unakusudia nyumba hiyo 20m haitoshi!

Tatizo wengine hapa wanatumia ya kitabuni ukifanya utendaji mwenyewe tofauti. Niliyokuambia si ya kufikirika na ndicho kilichofanyika. Jamaa ananunua matofali karibu na anapojenga na kuyachukua kwa tolori yeye mwenyewe. Maji madumu na anasukuma mwenyewe kumsaidia mjenzi wa kawaida. We unafikiria mahesabu ya kukodi kampuni ya kukujengea hicho si kiwango tunachotaka yakhe.

Mimi mwenyewe niliamua kujenga nyumba kwa mtindo huo niliisimamisha na kukamilika within 4 month pamja na kudril kisima cha maji kwa kuwatumia local people wanatumia mbavu kwa kucharge nguvu kwa kula ugali mwingi. Wanaondoka na milioni yao ya kidril ksima cha maji wakati ukialika kampuni leo hata milioni tatu kudril kisima watakutolea nje.

Tusikatishane tamaa bali tupeane njia za kuokoa gharama za ujenzi zisizo za lazima kwa kuwaajiri local people kuwapa ajira.

Hizo ulizoandika 28,000,000/= nitakujengea nyumba nzuri ya kawaida yenye 3 bedroom, dining na kitchen hadi inakamilika finishing, tunajua mbinu za kujenga kuokoa gharama na hiyo ufanyayo wewe unajitahidi kutafuta ulaji.
 
kwenye red ume inflat sana. mil 20 unaweza kujenga bwana wasikudanganye watu uka[poteza pesa zako ila sasa inabidi use,me nyuma isiyo na decorations maana ukizungumzia decorations inaweza fika mil 100.

Umesema kweli kabisa bora umetoa mwanga zaidi kuwasaidia wenzetu wanaostruggle kuwa na vibanda vyao, tusiwatenze nguvu ila tuwape ukweli na kuwatia moyo wajikwamue .

Watu wanajenga nyumba ya mapaa mawili tu lakini umaliziaji unawavunja shingo wapita njia, ni kwa sababu ya simple but good kuliko complications zinazoweza kukugharimu pesa nyingi ambazo zitakupa presha kila kukicha na nyumba haiishi.
 
Mgawanyo Wa Vitu Na gharama zilizotajwa hapo chini zipo sahihi kabisa isipokua amesahau mchanga, kokoto na maji. Kama Kweli Unayo M20 Kwa Mara Moja Utaweza kujenga kwa urahisi kuliko gharama za kudunduliza fedha.
Hata mimi niliona hivyo!!!
 
Umesema kweli tatizo watanzania TUNAJIFANYA matajiri Kumbe wapi! Wengi wetu tuliwakuta wazazi wetu wapo kwenye Nyumba ambazo si kama mnazozipigia Mahesabu sa hvi.Nyingi tulikuta hakuna UMEME lakini baadae ukawekwa.. Mtu anapiga Mahesabu utadhani anataka Nyumba ionekane ya kifahar sana.

Anza Kawaida Utaendelea kidogo kidogo si lazima kila kitu kwa wakati Mmoja. Hiyo Pesa Inatosha asikudanganye Mtu. Kama utakuwa unajishughulisha na we katika kazi., na kuwa makini sana na Mafundi wizi ni Mkubwa

Tatizo wengine hapa wanatumia ya kitabuni ukifanya utendaji mwenyewe tofauti. Niliyokuambia si ya kufikirika na ndicho kilichofanyika. Jamaa ananunua matofali karibu na anapojenga na kuyachukua kwa tolori yeye mwenyewe. Maji madumu na anasukuma mwenyewe kumsaidia mjenzi wa kawaida. We unafikiria mahesabu ya kukodi kampuni ya kukujengea hicho si kiwango tunachotaka yakhe.

Mimi mwenyewe niliamua kujenga nyumba kwa mtindo huo niliisimamisha na kukamilika within 4 month pamja na kudril kisima cha maji kwa kuwatumia local people wanatumia mbavu kwa kucharge nguvu kwa kula ugali mwingi. Wanaondoka na milioni yao ya kidril ksima cha maji wakati ukialika kampuni leo hata milioni tatu kudril kisima watakutolea nje.

Tusikatishane tamaa bali tupeane njia za kuokoa gharama za ujenzi zisizo za lazima kwa kuwaajiri local people kuwapa ajira.

Hizo ulizoandika 28,000,000/= nitakujengea nyumba nzuri ya kawaida yenye 3 bedroom, dining na kitchen hadi inakamilika finishing, tunajua mbinu za kujenga kuokoa gharama na hiyo ufanyayo wewe unajitahidi kutafuta ulaji.
 
Unaweza kabisa; usiogope kujenga kwanza chumba self contained, sehemu ya kupikia, na sebule ndogo - kitu kama a studio flat, huku ukiwa na ramani nzima ambayo utaimalizia taratibu hata ukishahamia humo. lakini siri kubwa ya mafanikio pia ni procurement - simamia kila kitu, kuanzia kufuata kokoto, mpaka kusimamia every step ya ujenzi unaondelea pale;that way uta save cost by half. Kama utasimamia kwa mtindo huu, with 20 million today in Dar, u can build a very nice house with two bedrooms, a bathroom, kitchen and living room.
 
Tatizo wengine hapa wanatumia ya kitabuni ukifanya utendaji mwenyewe tofauti. Niliyokuambia si ya kufikirika na ndicho kilichofanyika. Jamaa ananunua matofali karibu na anapojenga na kuyachukua kwa tolori yeye mwenyewe. Maji madumu na anasukuma mwenyewe kumsaidia mjenzi wa kawaida. We unafikiria mahesabu ya kukodi kampuni ya kukujengea hicho si kiwango tunachotaka yakhe.

Mimi mwenyewe niliamua kujenga nyumba kwa mtindo huo niliisimamisha na kukamilika within 4 month pamja na kudril kisima cha maji kwa kuwatumia local people wanatumia mbavu kwa kucharge nguvu kwa kula ugali mwingi. Wanaondoka na milioni yao ya kidril ksima cha maji wakati ukialika kampuni leo hata milioni tatu kudril kisima watakutolea nje.

Tusikatishane tamaa bali tupeane njia za kuokoa gharama za ujenzi zisizo za lazima kwa kuwaajiri local people kuwapa ajira.

Hizo ulizoandika 28,000,000/= nitakujengea nyumba nzuri ya kawaida yenye 3 bedroom, dining na kitchen hadi inakamilika finishing, tunajua mbinu za kujenga kuokoa gharama na hiyo ufanyayo wewe unajitahidi kutafuta ulaji.

Upo sahihi.
 
Kwa kuanzia unaweza kujenga mabanda ya uweani ya uhakika na ni modern 3 room kitchen one living room
na ukipata pesa zaidi utaanza nyumba kubwa kwani bora uwe na kitu kidogo cha uhakika kuliko kuwa na kitu kikubwa ambacho hakijakamilika , wakati huohuo ukatumia kiwanja chako cha mbele kwa bishara ya kufuga kuku
 
Kama una kiwanja unajenga nyumba nzuri tu, ila kama huna kiwanja inkubidi ununue kiwanja cha bei rahisi nje kidogo ya mji kisizidi m2.5 na hela iliyobakia unajenga nyumba na inaisha. Unatakiwa usimamizi wa hali ya juu sana na mafundi waaminifu. Ukitaka msaada nitakupa mafundi wazuri na waaminifu na wa bei nzuri.
 
we huna hela hapo..nunua kivitz cha milioni 5 cha kuuzia nyago mjini..halafu nunua bb torch ya kuchat mambo ya facebook ,then nedna pale azam kwa akina madenge chukua samsung galaxy 2 ya deal anza kuchat jf...zinazobaki piga koka ama kesto laiti..achana na mambo ya kujenga ni mawazo ya kizee hayo...

akili za tope zimechanganywa na haja kubwa.
 
jamani siwezi kujenga nyumba ya vyumba vinne hapo dar kwa milioni 20????niambieni kama siwezi kabla sijaipoteza hii pesa...

thanks,
Kama ni selfcointaned huwezi hata kwa bakora, lkn kama ni nyumba zetu za kawaida choo nje na chenji itabaki ya kufungulia ka genge ka kuanzia maisha.
 
Hongera da Neema me najitolea kusimamia ujenzi wa nyumba yako bila malipo ila nyumba ikiisha uni- accomodate japo kwa miezi sita wakati unaangalia kama ninaweza kuwa mpangaji wa kudumu aka mume, au kuwa mpangaji wa muda aka boi friend au mwangalizi aka joka la kibisa
 
mimi nazungumza through experience,kwa hiyo hela inadepend unataka kujenga nyumba ya aina gani, ukubwa
,Hadhi gani na wapi.

Kwa nyumba ya kuishi kama utajenga ya kiswahili angalao unaweza ukamaliza na kuhamia,nafikiri nikikuambia ya kiswahili unanielewa kama huelewi vizuri nenda tandale au m/nyamala utaona mfano wake,kwa ya kiswahili unamaliza hata room 5.

Sasa basi kama unataka kujenga nyumba kama nyumba angalao mtu akasema una nyumba na sio banda ya room 3 na sitting room,msingi gharama zake zitadepend na eneo kama tambarare au mwinuko na udongo pia hapo approximate milion 8 na kuendelea na umesimamia mwenyewe msingi umeisha umebakia na milion 12 anza pandisha tofali utaenda mpaka juu kwenye lenta biashara imeisha,uanze msako wa kutafuta 20 nyingine za kumalizia kwa hiyo hujaanzia pabaya.

So kwa kweli mie maono yangu kwa hiyo milion ishirini kusema unajenga nyumba kama nyumba eti room 3 from msingi mpaka kupaua madirisha,milango finishing vyooo uchimbe tiles hiyo million ishirini inakuangalia tu huo ni uwongo hata nyumba ya room 2 na sebule kwa hiyo hela bado ni uongo,munielewe mie nazungumzia nyumba na sio banda.
 
OB-RS502_0210Ga_D_20120208161702.jpg

Hizo 20,000,000 ningekuwa nazo ningeamua kujenga nyumba ndogo ya kawaida yenye 3 bedroom including muster, living room ya kawaida na kitchen. Ninachoweza kukwepa ni ramani ambayo upauaji wake hugharimu kidogo. Mapaa kama haya pichani ambayo hayaingiliani hupunguza sana gharama za roofing.

Kuna mtu amefanikiwa kupandisha kuta tayari kwa 5 milion, alikosea mahesamu ya ramani inayoweza kumpunguzia gharama, eti wanasema mjengo wa kisasa, mapaa yanaingiliana, na nyumba hiyo ni just three bedroom, anahitaji mabati karibu 80, mbao nyingi tu, tatizo ni nini ubunifu wa ramani ambayo hakuangalia na sasa unamgharimu sana roofing. Ukubwa wa nyumba kama hiyo mimi ya kwangu nilitumia bandle moja na nusu tu kwa vile niliplan ukubwa wa nyumba mapema na kuhakikisha uezekaji unatumia bati moja refu toka juu hadi chini badala ya kuunganisha mabati mawili, yeye anahitaji zaidi ya 3 1/2 bandle kuelezeka bati na bado mbao, misumari nk. Mabati mengi yanakatwa na kutupwa kutokana na mapaa ya mwingiliano, hapo vipande vya mabati yanayotupwa ni pesa zinatupwa, lakini kama angeplan mabati yatumike yote asingeingia hasara ya kukata vipande vya bati na kuvitupa.

Mchambuzi amechambua vizuri sana, tuachane na kujenga nyumba za kushindana wakati nafasi na uwezo tunatofautiana. Unaweza kukuta mtu umeanza vizuri na kisha unaishia kupata stress ya kumalizia na nyumba hizo za kisasa umaliziaji wa paa ni lazima ufanyike kwa pamoja, vigumu kusema uezeke kwanza sehemu ya nyumba ili upate pa kujihifadhi.

Ushauri huu tunautoa kwe wenzetu wanaohangaika kama mie kutumia kidogo walicho nacho kupata mahali salama pa kulaza ubavu kuondokana na dhana ya kuwa tenant katika nchi yako mwenyewe. Ukishamaliza kibanda chako cha awali na unaishi kwa utulivu, kisha nafasi ikikuruhusu baada ya kutulia ndani ya kibanda chako, unaweza kubuni nyumba yako ya kiwango unachotaka ambayo ni dream ya retirement yako, ambayo utaijenga kwa utaratibu na kwa ufanisi mkubwa. Ukifanikiwa hiyo plan ya retirement nyumba yako ya awali unaweza ukaifanya kitega uchumi kwa kupangisha baadaye ikupe chai kidogo.
 
Bora Candid Scope umewaambia watu naona wanapenda kukatisha tamaa wenzao. Nyumba yangu ya kwanza kujenga ilikuwa ndogo na ya kawaida. Hii imeniwezesha kumiliki nyumba mapema kabla ya watoto kuanza shule. Sasa hivi ninaanza nyingine na hii ndio ninafikiria itakuwa ya kuishi tukistaafu. Bado sipendelei nyumba kuubwa sana kwani uzeeni pia ni mzigo kufanya usafi na refurbish kwenye vyumba ambavyo haishi mtu!
kama ni watoto na wageni ni bora nijenge nyumba ndogo pembeni inayojitegemea, ambayo waweza hata kuifanya kitega uchumi kwa kupangisha au investment nyingine
Ukitaka viwango vya gharama za nyumba pia check hapa nyumba poa ingawa nao wameongeza kidogo sio sawa na mtu unayejenga ukisimamia mwenyewe na kujitahidi to minimize costs as much as possible

::NyumbaPoa - Design & Price Range
 
hivi nyie jamaa mumeshajenga ama? maana inakuaje mtu anakushauri kitu ambacho hajawahi fanya?
 
Back
Top Bottom