Mar 15, 2019
39
111
Habari za mchana wakuu, natumai hamjambo kabisa na mnaendelea katika harakati za kusaka mkate na kwa wale wanaugua Mungu awaponye kwa uwezo wake tuseme Amin !!

Kwanza kabisa mimi ni mtu ambaye karibia kila baada ya dakika 5 lazima nizame kwenye deep thinking kuhusu kitu chochote ( positive lakini :D :D ) kwahiyo katika hali hiyo najikuta kwa siku nakuwa nachanganua mambo mengi sana hasahasa ya kibiashara na ujasiriamali. Kichwani mwangu nina ideas kibao za kibiashara na ujasiriamali ambazo zipo nilizoziandika na zipo ambazo zipo tu kichwani na siwezi kuzitekeleza zote.

Leo nimeona nilete huu mchongo wa kuuza simu used ( refurbrished smartphones ) kutoka Dubai, UK, USA na Japan. Kama tunavyojua mahitaji ya kuendana na kasi ya globalizationa ni makubwa sana kwa sasa na kila mmoja anataka apate internet akiwa kiganjani kwake, sasa kupata internet kiganjani lazima uwe na simu yenye uwezo na simu nyingi zenye uwezo na imara zina gharama kubwa kwa sisi watu wa kawaida.

Njia pekee ni kutumia zile simu ambazo watu walioendelea wamezitumia na kuziacha kwa kuamua kubadili brand au zilikuwa na tatizo dogo then wataalam wanazitengeneza na kutuletea huku Afrika na sisi tufaidi.

KWA MILIONI 8 YAKO

Hapa naona nilete biashara inayohitaji mtaji wa kueleweka ili uweze kupata faida ya kueleweka pia, kwa mtaji wa milioni nane unaweza kuzungusha kwa mwaka mmoja ukajikuta na faida ya milioni 20 huku mtaji wako ukiwa bado uko vile vile. Ngoja nitoe mchanganuo wa haraka haraka.

KODI
Frame kwa miezi 6 = Tsh 600,000
- Marekebisho ya frame na vifaa vyake = Tsh 400,000
JUMLA = TSH 1,000,000

USAJILI
Usajili wa biashara = 500,000

PESA YA MZIGO WA KWANZA
  • Kiasi cha Tsh milioni 6 kitatumika kuagiza mzigo.
  • Wastani wa bei ya kuagizia piece moja ni Tsh 100,000 ambapo zitapatikana simu 60 na jumla yake ni Tsh 6,000,000.
  • Makadirio ya Gharama za usafirishaji hadi kupokea mzigo = Tsh 500,000
JUMLA = TSH 6,500,000

MALIPO YA MUUZAJI KWA MWEZI
- Muuzaji = Tsh 300,000

MAKADIRIO YA MAUZO KWA MWEZI
  • Simu zitakazouzwa = 60 ambapo piece moja itauzwa kwa Tsh 150,000
  • Jumla yake kwa simu 60 itapatikana Tsh 9,000,000

HELA YA MAUZO KWA MWEZI - HELA YA MZIGO KWA MWEZI
9,000,000 - 6,500,000 = 2,000,000
INAYOBAKIA = TSH 2,500,000

FAIDA YA MAUZO KWA MWEZI - MSHAHARA KWA MFANYAKAZI
2,500,000 - 300,000 = 2,200,000
INAYOBAKIA = TSH 2,200,000

FAIDA YA BIASHARA KWA MWEZI = 2,200,000

Kwenye faida hapo toa TSH 500,000 kwa ajili ya kulipia matangazo ya social media ambayo ni kama $200 ili uendelee kuuza zaidi mwezi unaofuata.

Utabaki na faida ya TSH 1,700,000 KWA MWEZI

Ukiwa na consistency ya namna hiyo kwa mwaka mzima lazima upate faida ya milioni 20 wakati huo mtaji wako uko palepale. Lakini inahitaji nidhamu, kujituma na maombi kwa Mungu.

Kama una hiyo pesa jitose hapo upambane nayo, kama utahitaji ideas zingine za kufanya basi nicheki.
WHATSAPP: 0683535699
 
Doesn't work, biashara za nadharia, Biashara ni Kama Imani ya dini, unajitoa haswa, sio kupige hesabu tu.
 
Back
Top Bottom