Naweza kujenga nyumba kwa TZS Milioni 20?

Hivi kwanini wabongo hatujengi jiko na dining pamoja? naona hii inapunguza nafasi kubwa sana kwenye nyumba.
small-house-plans-kitchenfinished.jpg

Mkuu hii wanaweza wazungu sana kufanya hivyo vyakula vyao vingi havi involbe mapishi ya uchafu...ukiwe dining na jiko dada wa kazi akisahau kutupa taka nje Dinning yote halufu mpaka sebuleni...ila ni nzuri sana...kama mnao ishi wa wachache na wasafi.
 
Hapo mi siwezi hata kuachangia kitu chochote labda
niwasubiri mafundi maana naona bila bila tu daaa

kwa hiyo sisi hatutajenga kabisa nyumba M 170 .
 
wakuu mi structure yangu ni 11 kwa 9 mita je makadirio inaweza kutumia bati ngapi
note. sijapandisha gebo msaada tafadhali
 
Ujenzi bongo ni ghali lakini mafundi nao niwezi. Hivyo haya mawili yanashaabiana kabisa moja kwa moja.

Kingine mafundi wapya kutoka vyuo vikuu ndio msiba kabisa, sababu wao wanachojali ni ratio zao walizoma kwenye building structure class 101. Ukweli ni kwamba vitu vingi wanavyovitaja ni unnecessary kwenye ujenzi.

Tukija kwenye swali lako, kusema kweli M20 kwa kujenga ni chini sana, sababu bei za vifaa ziko juu. Ila unaweza kuanza kisha ukamalizia pole pole hakuna haraka kaka.
 
Hivi kwanini wabongo hatujengi jiko na dining pamoja? naona hii inapunguza nafasi kubwa sana kwenye nyumba.
small-house-plans-kitchenfinished.jpg

Mara nyingi hiyo unayoiona huwa ni zaidi kwa ajili ya breakfast au mlo mwengine wa harakaharaka lakini kikawaidia huwa kunakuwa na dining space proper (ingawa yes, nakubali inaweza kuwa jikoni).

Halafu kuna tatizo pia la hali ya hewa....scheme ya kuwa na dining jikoni inafaa zaidi kwa sehemu za baridi lakini sio kwenye maeneo ya joto. Hata ukiangalia nyumba za zamani za kiafrika/kienyeji (african architecture) utaona kuwa kwa maeneo ya baridi sehemu ya jiko na kulia mara nyingi vilikuwa sehemu moja na mara nyinge hata sehemu ya kualala ilikuwa humohumo. Lakini kwa sehemu za joto mara nyingi sehemu ya kupia inakuwa open (with or without a roof) na inakua tofauti na ile ya kulia.

So tunapo copy ramani hizi ni vema tukazingatia hali ya hewa ya kwetu pamoja na tamaduni zetu.
 
tumia toali za kuchoma tofali 8000 ni tzs 800,000
mafundi tzs 2000,000
mbao tzs 2000,000
cement mifuko 100 tzs 1,500,000
umeme 3,000,000
finishing +rangi 7,000,000
milango na madirisha 4,000,000
chenji inabaki
 
tofali la kuchoma moja kwa bei ya tanurini ni tshs 70 kwa bei ya kawaida tshs 80 hadi kufika dar tshs 100,
matofali 8000 unajenga nyumba ya bedroom 4,sitting,stoo,toilet,kitchen.
milioni 18 unajenga kila kitu hadi tiles.wasiliana nami nikuelekeze kama upo serious
 
Wachangiaji wengi hapa wanaonyesha figure za kumkatisha tamaa mtoa mada wakati ukweli ni kwamba 20,000,000 kama ameamua kuchukua njia ya mkato nyumba inakamilika kabisa kwa nyumba za kawaida kwa mazingira ya kiafrika ambayo haina mambo ya kifahari bali ya kawaida na itakuwa na mvuto.

Juzi tu mmoja hapa Dar alifanikiwa kupata Tsh 4,000,000 akaamua ajenge kibanda nje ya mji ili nyumba yake iliyopo mjini aitumie kama kitega uchumi ili kukabiliana na chamgamoto za hali ya maisha.. Nyumba ndogo ya vyumba vinne ameweza kufikisha renta kwa usimamizi wake. We kwa hiyo 20,000,000 mbona nyumba itaamilika katika mambo mengi mradi jitahidi kutumia ramani ambayo mjengo wake hautahitaji gharama kubwa.

Ukiamua kujenga aanza na ukiwa na nia utamaliza nyumba yako.
 
ujenzi wa 20m unawezekana lakin usikimbilie kwenye finishing za gharama, fanya iwe rahisi kwa kurahisisha mipangilio (plan) yako... ila pia unaweza kununua vifaa kwa wakati mmoja inasaidia kupunguza mkimbizano kwa kila kifaa unapokihitaji,
 
small-house-plans-construction-foyerframed.jpg


Tusipotoshe watu, nyumba za aina hiyo ni za huko ukanda wa baridi amako hakunaga misukosuko ya hali ya hewa kama ya ukanda wa tropical. Umeshuhudia nchini USA maafa wanayopata nyumba kubomoka kutokana na mvua za upepo wa kisulisulili. Inapotokea ni balaa unabaki kukusanya tu mbao hizo. Lakini huku kwetu itokeapo hali ya namna hiyo nyumba kadhaa huezuliwa paa tu jambo ambalo halikupi hasara kubwa sana..

Hizo nyumba za wazungu moto ukitokea kitakachobaki ni majivu tofauti na kwetu matofati hayaungui.
 
jamani siwezi kujenga nyumba ya vyumba vinne hapo dar kwa milioni 20????niambieni kama siwezi kabla sijaipoteza hii pesa...


thanks,

we huna hela hapo..nunua kivitz cha milioni 5 cha kuuzia nyago mjini..halafu nunua bb torch ya kuchat mambo ya facebook ,then nedna pale azam kwa akina madenge chukua samsung galaxy 2 ya deal anza kuchat jf...zinazobaki piga koka ama kesto laiti..achana na mambo ya kujenga ni mawazo ya kizee hayo...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom