Nawaomba radhi wana CHADEMA, nilimwelewa vibaya Mhe. Mbowe - Pasco

Mwenyekiti wa Chadema Mhe. Freeman Mbowe, aliwahasisha Chadema kususia uchaguzi wa serikali za mitaa, wakasusa, CCM wakatwaa ushindi wa mezani.

Katika bandiko hili nililaumiwa sana.

Jana pale Mwanza, Mhe. Mbowe kaomba maridhiano, swali ni jee Chadema waliposusa, walisusa ili wapate nini kama mwisho wa siku unakuja kubembeleza kuomba maridhiano?.

Siku zote haki haiombwi wala hailetwi kwenye kisahani cha chai, huwa inapiganiwa!.
P
 
wamekusamehe ila huna mkia
Mkuu sana Mhe. Regia Mtema,

Heshima mbele!.

Kwanza samahani kuchelewa kuomba radhi, nilikuwa nasubiri ile hansard uliyoahidi, ili nijiridhishe, nilimwelewa vibaya Mhe. Mbowe.
Baada ya kusoma michango mingi humu kuhusu hoja hii, nimeona sina sababu ya kuendelea kuisubiria hansard, hivyo ninatumia fursa hii kwa kusema yafuatayo,

Mimi Pasco wa JF, "Nawaomba Radhi CHADEMA, Nilimwelewa Vibaya Mhe. Mbowe".

Nawaomba radhi kwa dhati, wale wote waliofedheheshwa na uelewa wangu.

Kwa vile sisi ni binadamu na tumeumbwa tofauti, hivyo tofauti za uelewa kati ya mtu na mtu ni kawaida, hakuna binadamu mkamilifu, kufanya makosa ni jambo la kawaida na kuombana misamaha pale mnapotofautiana pia ni kawaida, hivyo sanahani sana.

Msamaha huu nimeufungulia thread inayojitegemea, ili niweke na chanzo cha uelewa wangu huo uliopelekea kumwelewa vibaya Mhe. Mbowe hivyo kutoa fursa kwa Chadema, kutuelewesha vizuri kusije jitokeza mikanganyiko kama hii kwa siku za usoni.
Utangulizi
Baada ya kumalizika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kilitangazwa kutokuridhishwa kwake na jinsi zoezi zima la uchaguzi lilivyoendeshwa, hivyo wakakataa kuyakubali matokeo ya kura za urais na kutangaza rasmi kutomtambua mshindi.

Binafsi sikukubaliana na msimamo wa Chadema na niliandika humu jamvini kwanini sikukubaliana nao. Tangu mwanzo wa mchezo, Chadema wakijua wazi, the playing ground is not level, lakini walikubali kuingia uwanjani na kupambana hivyo hivyo, huku mmoja ameshika mpini, ungetegemea nini?.

Chadema walikubali kutia saini kanuni za mchezo, hivyo sio busara kuja kukiuka kanuni hizo kwa kukataa matokeo, ndio maana kwa maoni yangu nilisema, the right forum kwa Chadema, kuyakataa matokeo, ni kufika siku yanatangazwa, kususa kusaini na kuwaeleza Watanzania sababu, ikiwemo kutomtabua rais, unamweleza pale pale in front of his face, na jamii yote ya kimataifa.

Kwa kutomtambua rais, Chadema walitoka nje siku ile rais akilihutubia Bunge.
Kilichotokea
Ulipowadia wakati wa kuchangia hotuba ya rais, waliosusa kuisikiliza, nilitegemea Chadema, wangenyamaza kimya, kuonyesha kuendelea kumsusia rais, au wangechangia bila kumtaja ili kuonye kutomtambua.

Kitendo cha Mwenyekiti wa Chadema, kusimama, akaanza kumsifu na kumshukuru na kumpongeza rais Kikwete, mimi nilichanganyikiwa na kuhamanika kwa furaha nikiamini sasa Chadema wanamtambua rais Kikwete ndipo nikapost thread hii
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...li-yaishe-yamtambua-rais-yampongeza-rais.html

Kwenye thread yangu hiyo, chini niliweka angalizo hili
Angalizo!.
Kuna kitu kinaitwa expressly na impliedly!
Expressly ni kwa Mbowe kutangaza kwamba sasa Chadema inamtambua Rais!
Impliedly ni pale Mbowe alipompongeza rais, akamsifu na kumshukuru na kuonyesha spirit ya reconciliation.

mkubali msikubali, Chadema imemtambua Rais JK impliedly na wamekubali yaishe zaidi ya hapo ni ubishi tuu, vinginevyo Mhe. Mbowe afanye Press Conference afafanue na kukazia kutomtambua JK!


Pamoja na angalizo hilo, haikusaidia watu kunielewa ni mpaka Mbunge wa Chadema, Mhe. Regia Mtema aliponitaka kuomba msamaha kupitia thread hii

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...i-chadema-umemwelewa-vibaya-hon-mbowe-14.html

Hitimisho
Mwanzo niliamini kwa vile Chadema, walitamka expressly kuwa hawamtambua JK, kubadilika na kutamkata tena expressly kuwa sasa wanamtambua itakuwa ni kugeuka nyuma na kugeuka jiwe la chumvi, hivyo niliamini wamechukua njia ya ustaarabu zaidi kwa kutosema expressly wamemtambua, bali impliedly kuonyesha kumtambua kwa kauli na matendo na hili ndilo kosa langu, nakubali kosa na naomba msamaha wa dhati.

Natumaini msamaha wangu emeeleweka japo sio lazima ukubalike, tuendelee kuchambua hoja mbalimbali humu jamvini kwa maslahi ya taifa.

Natanguliza shukrani.

Wenu

Pasco.

Angalizo: Pasco wa JF siyo mwanachama wala mshabiki wa chama chochote cha siasa, ila ni mkereketwa wa demokrasia ya kweli ndani ya Bunge. Principle ya uchangiaji wangu ni kuongea nothing but the truth kwa kuzingatia truthfulness, accuracy, objectivity, impartiality, fairness, na balance nikiweka mbele maslahi ya taifa.
 
Mwenyekiti wa Chadema Mhe. Freeman Mbowe, aliwahasisha Chadema kususia uchaguzi wa serikali za mitaa, wakasusa, CCM wakatwaa ushindi wa mezani.

Katika bandiko hili nililaumiwa sana.

Jana pale Mwanza, Mhe. Mbowe kaomba maridhiano, swali ni jee Chadema waliposusa, walisusa ili wapate nini kama mwisho wa siku unakuja kubembeleza kuomba maridhiano?.

Siku zote haki haiombwi wala hailetwi kwenye kisahani cha chai, huwa inapiganiwa!.
P

Mkuu salaam bandiko lako naona kama limekaa kipersonal attack zaidi kwa Mh. Mbowe kwanini unasema Mbowe alihamasisha CHADEMA kususia uchaguzi haya maneno si ya Busara kwa Kariba yako.

Maamuzi yote yalifanywa na Kamati kuu hiki ndicho chombo chenye mamlaka ya jambo lolote la kiaamuzi baada ya kupitia hatua kadhaa.

Binafsi naona kunaupotoshaji.
 
Mwenyekiti wa Chadema Mhe. Freeman Mbowe, aliwahasisha Chadema kususia uchaguzi wa serikali za mitaa, wakasusa, CCM wakatwaa ushindi wa mezani.

Katika bandiko hili nililaumiwa sana.

Jana pale Mwanza, Mhe. Mbowe kaomba maridhiano, swali ni jee Chadema waliposusa, walisusa ili wapate nini kama mwisho wa siku unakuja kubembeleza kuomba maridhiano?.

Siku zote haki haiombwi wala hailetwi kwenye kisahani cha chai, huwa inapiganiwa!.
P
Ni faida gani iliyopata kama nchi juu ya vyama vyengine vya siasa kukimbiwa,office kufungwa wakati wa kurejesha fomu za wagombea nchi mzima?


Hebu jiulize kama wewe wagombea asilimia karibu wote wameenguliwa ungefanyaje?

Kiufupi ni kwamba yote yanayoendelea ccm haikubali kushindwa kiuhalali na haiwezi kushindana.

Magufuli anasema maendeleo hayana vyama kwanini ni mbaguzi kwenye upelekaji maendeleo? Jibu lake baada ya kuelezwa shida ya maji ni mama mmoja huko mkoani anajibu akawaeleze aliowachagua au mume wake. Huyu ndio kiongozi wa nchi?

Kiufupi uongozi wa sasa haupo tayari kiushindani.
 
Mimi Pasco wa JF, "Nawaomba Sana Radhi Wana CHADEMA, Nilimwelewa Vibaya Mhe. Mbowe".

Nawaomba radhi kwa dhati ya moyo wangu, wale wote waliofedheheshwa na uelewa wangu.

Kwa vile sisi ni binadamu na tumeumbwa tofauti, hivyo tofauti za uelewa kati ya mtu na mtu ni kawaida, hakuna binadamu mkamilifu, kufanya makosa ni jambo la kawaida na kuombana misamaha pale mnapotofautiana pia ni kawaida, hivyo samahani sana.
Kuna tukio hili limenitokea, hivyo kuomba msamaha kupitia JF, A shock of my life, furaha yageuka shubiri. Be good to people on your way up, you might meet them on your way down, mwenzenu leo yamenikuta! basi kuna watu wakadhani leo ndio mara yangu ya kwanza kuomba msamaha kupitia jf!. Hivyo hapa nawakumbusha tuu, mimi ni mtu mstarabu sana, nikikosea, huwa naomba msamaha!.
P
 
I wish waandishi wote wangekuwa kama wewe, wasiofungamana na chama chochote cha siasa, wenye kuzingatia truthfulness, accuracy, objectivity, impartiality, fairness, na balance nikiweka mbele maslahi ya taifa, tungefaidika sana kupata habari za uhakika zisizo na upendeleo wala chumvi. I LIKE YOUR APPROACH - Big up Pasco.
Mkuu elimumali, niunge mkono kwenye jambo langu ili hili jambo tulipeleke mbali.
P
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom