Nawaomba radhi wana CHADEMA, nilimwelewa vibaya Mhe. Mbowe - Pasco

Mkuu sana Mhe. Regia Mtema,

Heshima mbele!.

Kwanza samahani kuchelewa kuomba radhi, nilikuwa nasubiri ile hansard uliyoahidi, ili nijiridhishe, nilimwelewa vibaya Mhe. Mbowe.
Baada ya kusoma michango mingi humu kuhusu hoja hii, nimeona sina sababu ya kuendelea kuisubiria hansard, hivyo ninatumia fursa hii kwa kusema yafuatayo,

Mimi Pasco wa JF, "Nawaomba Radhi CHADEMA, Nilimwelewa Vibaya Mhe. Mbowe".

Nawaomba radhi kwa dhati, wale wote waliofedheheshwa na uelewa wangu.

Kwa vile sisi ni binadamu na tumeumbwa tofauti, hivyo tofauti za uelewa kati ya mtu na mtu ni kawaida, hakuna binadamu mkamilifu, kufanya makosa ni jambo la kawaida na kuombana misamaha pale mnapotofautiana pia ni kawaida, hivyo sanahani sana.

Msamaha huu nimeufungulia thread inayojitegemea, ili niweke na chanzo cha uelewa wangu huo uliopelekea kumwelewa vibaya Mhe. Mbowe hivyo kutoa fursa kwa Chadema, kutuelewesha vizuri kusije jitokeza mikanganyiko kama hii kwa siku za usoni.
Utangulizi
Baada ya kumalizika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kilitangazwa kutokuridhishwa kwake na jinsi zoezi zima la uchaguzi lilivyoendeshwa, hivyo wakakataa kuyakubali matokeo ya kura za urais na kutangaza rasmi kutomtambua mshindi.

Binafsi sikukubaliana na msimamo wa Chadema na niliandika humu jamvini kwanini sikukubaliana nao. Tangu mwanzo wa mchezo, Chadema wakijua wazi, the playing ground is not level, lakini walikubali kuingia uwanjani na kupambana hivyo hivyo, huku mmoja ameshika mpini, ungetegemea nini?.

Chadema walikubali kutia saini kanuni za mchezo, hivyo sio busara kuja kukiuka kanuni hizo kwa kukataa matokeo, ndio maana kwa maoni yangu nilisema, the right forum kwa Chadema, kuyakataa matokeo, ni kufika siku yanatangazwa, kususa kusaini na kuwaeleza Watanzania sababu, ikiwemo kutomtabua rais, unamweleza pale pale in front of his face, na jamii yote ya kimataifa.

Kwa kutomtambua rais, Chadema walitoka nje siku ile rais akilihutubia Bunge.
Kilichotokea
Ulipowadia wakati wa kuchangia hotuba ya rais, waliosusa kuisikiliza, nilitegemea Chadema, wangenyamaza kimya, kuonyesha kuendelea kumsusia rais, au wangechangia bila kumtaja ili kuonye kutomtambua.

Kitendo cha Mwenyekiti wa Chadema, kusimama, akaanza kumsifu na kumshukuru na kumpongeza rais Kikwete, mimi nilichanganyikiwa na kuhamanika kwa furaha nikiamini sasa Chadema wanamtambua rais Kikwete ndipo nikapost thread hii
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...li-yaishe-yamtambua-rais-yampongeza-rais.html

Kwenye thread yangu hiyo, chini niliweka angalizo hili
Angalizo!.
Kuna kitu kinaitwa expressly na impliedly!

Expressly ni kwa Mbowe kutangaza kwamba sasa Chadema inamtambua Rais!
Impliedly ni pale Mbowe alipompongeza rais, akamsifu na kumshukuru na kuonyesha spirit ya reconciliation.

mkubali msikubali, Chadema imemtambua Rais JK impliedly na wamekubali yaishe zaidi ya hapo ni ubishi tuu, vinginevyo Mhe. Mbowe afanye Press Conference afafanue na kukazia kutomtambua JK!

Pamoja na angalizo hilo, haikusaidia watu kunielewa ni mpaka Mbunge wa Chadema, Mhe. Regia Mtema aliponitaka kuomba msamaha kupitia thread hii

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...i-chadema-umemwelewa-vibaya-hon-mbowe-14.html

Hitimisho
Mwanzo niliamini kwa vile Chadema, walitamka expressly kuwa hawamtambua JK, kubadilika na kutamkata tena expressly kuwa sasa wanamtambua itakuwa ni kugeuka nyuma na kugeuka jiwe la chumvi, hivyo niliamini wamechukua njia ya ustaarabu zaidi kwa kutosema expressly wamemtambua, bali impliedly kuonyesha kumtambua kwa kauli na matendo na hili ndilo kosa langu, nakubali kosa na naomba msamaha wa dhati.

Natumaini msamaha wangu emeeleweka japo sio lazima ukubalike, tuendelee kuchambua hoja mbalimbali humu jamvini kwa maslahi ya taifa.

Natanguliza shukrani.

Wenu

Pasco.

Angalizo: Pasco wa JF siyo mwanachama wala mshabiki wa chama chochote cha siasa, ila ni mkereketwa wa demokrasia ya kweli ndani ya Bunge. Principle ya uchangiaji wangu ni kuongea nothing but the truth kwa kuzingatia truthfulness, accuracy, objectivity, impartiality, fairness, na balance nikiweka mbele maslahi ya taifa.

Pasco,

Mi nakuona hapa umeomba radhi huku ukiwa unashadidia hoja yako ile ile ya mwanzo. Labda umemuomba radhi mh. Regia, manake naona hata heading yako iko ndani ya funga na fungua semi, sasa sijui umeifanya hivyo kwa bahati mbaya ama umekusudia.

Lakini mwenye macho amekusoma na kukuelewa, bora tuendelee na masuala mengine manake hii ni kama umesisitiza msimamo wako wa tangu awali.
 
mbowe anamtambua jk kama rais wa jmt, ila dr.slaa yeye hamtambui jk kama rais wa jmt. Matendo na kauli za hawa viongozi 2 wakuu wa cdm yanadhihirisha wazi kukinzana kwao, mkubali au mkatae ukweli unauma japo mambo yako wazi tena sana, peupe hadharani! Natoa changamoto kwa mbowe na dr.slaa, kama wanabisha jambo hili basi waitishe pc kwa pamoja, na watoe kauli yao kuthibitishia umma wa tz msimamo wao wa kutomtambua jk kama rais wa jmt.

Sidhani kama wewe unaelewa au umekataa kuzielewa post za wasomaji wa awali. Pengine urejee post no 21 ya Mwangaza utapata mwangaza.
 
Pasco;

Watch your tongue sometimes.

wahenga walisema fikiri kabla hujatamka.

Kama TZ ingekuwa Nchi ya vurugu inawezekana kuwa madhara yangekuwa yametokea.

Kumbuka wewe ni mwandishi wa habari, usiongozwe na hisia zako bali una wajibu wa kuleta taarifa kamili ambayo haiko biased. Nafahamu kuwa unasimamia hilo na ndiyo maana tunaokufahamu tulishangaa mihemko yako imetoka wapi.

Siasa za Tanzania sasa hivi ziko katika transition na waandishi kama nyie mnatakiwa muwe makini kuiweka sawa jamii ielewe ukweli na wala si kuleta "Taarifa za Kiitenteligensia" ulivyoelewa wewe.

otherwise big up kwa kujitambua na hiyo ni hatua makini sana ya ukomavu na uelewa.

A.
 
Tusiwalaumu walimu wakati wote kwa wanafunzi kufeli mitihani...Mbowe kajitahidi sasa kuelezea kuwa wao wanamtambua Raisi..sababu kikatiba ni halali,...hata kama kwa kura za siku ile NEC ingemtangaza Dovutwa kuwa Raisi pamoja na kura zake chahche bado angekuwa ni rais halali KIKATIBA....na wao Chadema wangemtambua, sababu kwa mujibu wa katiba Tume ikishamtangaza Rais basi hawezi kupingwa popote na yeyote. Wanachopinga ni mchakato na kanuni zinazotumika kumpata Rais. Mbowe kalisema hili mara nyingi na watu WALIO WENGI hawajaelewa bado.
 
Sijui watu tunabishana kitu gani hapa jamvini.
Maana ya alama za kufungua na kufunga usemi kwenye kichwa cha habari cha mwerevu Pasco zinaonesha kuwa Pasco ameomba radhi ila hiyo ni kama taarifa amabyo jamvi hili linafahamishwa na mtu mwingine ambaye siye Pasco kuhusu kuomba radhi huko kwa Pasco. Ili kujua kama hajaomba radhi Pasco anatakiwa akanushe taarifa hizo hapo juu, kwani kwa jinsi ilivyoandikwa hapo inamaanisha kuwa mtu mwingine ameomba msamaha kwa niaba ya Pasco. Ikibaki hivyo hivyo ni kuwa PASCO AMEOMBA RADHI kwisha.
 
Nimegundua kwamba watu wengi sana hapa JF hawasomi message vizuri, au hawajui matumizi ya alama katika maandishi. Nasema hivi kwa sababu wengi wenu (ukiondoa wachache sana, nafikiri wawili au watatu) wamevamia kusoma text bila kuangalia kwa makini kilichoandikwa kwenye heading. Pasco kwa makusudi kabisa akijua kwamba haombi msamaha ametumia alama "....." kwenye heading yake, which implies that the meaning of the heading is actually the opposite of what he wrote. Ndio maana pia baadhi yenu mmeweza kuona kwamba kwenye text hajabadili msimamo, anaendelea kuwa na maana ileile na kichwa chake habari.

Duuh! Jamaa atakuwa amekaa somewhere anawachora sana...LMAO:laugh:.
 
Kuna mkanganyiko katika thread ya Pasco; mtu anaomba msamaha baada ya kuridhika kuwa ametenda kosa, kitu ambacho hakionekani kwenye thread ya Pasco. Kwa maoni yangu Pasco bado ameshikiria huo msimamo wake wa awali kwamba, kimazingira chadema imemtambua JK kwa kukubali kushiriki katika kuijadili hotuba yake walio hisusia hapo mwanzoni. Mimi sijui hii hoja ya chadema kutomtambua JK kama rais ameipata wapi. Chadema imetamka mara nyingi ya kwamba wanamtambua JK kama rais aliyewekwa kwa mujibu wa sheria, ingawaje wanaamini hakuwekwa kiharari. Pamoja na hayo, napenda namimi niungane na Pasco, kuhoji busara iliyotumika kwa chadema kuungana na ccm kuipa umuimu mkubwa kuliko kiasi hiyo hotuba ya JK. Kwa baadhi yetu hizo siku tano zilizotumiwa na mbunge kujadili hotuba hiyo huku mkitumbua zaidi ya shs 100milioni kila siku ilikuwa ni ushahidi mwingine wa matumizi mabaya ya fedha za umma.
 
Sijui watu tunabishana kitu gani hapa jamvini.
Maana ya alama za kufungua na kufunga usemi kwenye kichwa cha habari cha mwerevu Pasco zinaonesha kuwa Pasco ameomba radhi ila hiyo ni kama taarifa amabyo jamvi hili linafahamishwa na mtu mwingine ambaye siye Pasco kuhusu kuomba radhi huko kwa Pasco. Ili kujua kama hajaomba radhi Pasco anatakiwa akanushe taarifa hizo hapo juu, kwani kwa jinsi ilivyoandikwa hapo inamaanisha kuwa mtu mwingine ameomba msamaha kwa niaba ya Pasco. Ikibaki hivyo hivyo ni kuwa PASCO AMEOMBA RADHI kwisha.


Nafikiri unajaribu kubishia the obvious. Alama za kufungua na kufunga semi (quotation mark) zinaweza kutumika kwa namna nyingi tu zaidi ya ku-quote. Mojawapo ya matumizi ni ku-indicate irony kwenye sentence au paragraph husika, yaani kutoa ujumbe kinyume cha kile mwandishi anachoamini/maanisha, kama alivyofanya hapa ndugu Pasco.

Unapojaribu kusema kwamba hii thread ni mtu ametumwa kuomba radhi kwa niaba ya Pasco si kweli maana iko wazi kwamba Pasco mwenyewe ndio kaanzisha thread, au mwenzetu unasoma kinyume?!
 
mtu anawezaje kuomba msamaha na maelezo kibao hivyo?....

kulikuwa na ugumu gani kwa pasco kuandika very short and clear kwamba

"Nawaomba Radhi Wana CHADEMA, Nilimwelewa Vibaya Mhe. Mbowe"
yani kwamba akaishia hapo hapo na ndo ikawa main content ya thread yake....

kuna ugumu gani?
 
Ndio maana huwa tunaingizwa mkenge kwenye mikataba tunasaini tu bila kujali contents zake....Halafu hapo chini ndo nazidi kujiuliza kulikoni great thinkers?
Byendagwero said:
Chadema imetamka mara nyingi ya kwamba wanamtambua JK kama rais aliyewekwa kwa mujibu wa sheria, ingawaje wanaamini hakuwekwa kiharari
Yani rais aliyewekwa kisheria lakini si halali?
 
huyu jamaa (Pasco) ina bidi aadabishwe kidogo walai ningekuwa namjua ningemchapa makofi nane iv!, au kama wewe ni muungwana kweli leo jioni tunaweza tukutane apo askari monument ili 'nikupongeze' kidogo ngudu yango Pasco?
 
content ya hii sredi haioneshi kuwa unaomba msamaha bali unazidi kung'ang'aniza lilelile. Naona umeanzisha hii sredi kujaribu kutushawishi kivingine tuamin jambo ambalo halikufanywa na mbowe. Hulazimishwi kuomba bali tulijaribu kukuelekeza umeelewa ila unagoma kuridhia.

the guy he is very clever hata mie nikiwa na msimamo wangu huwa natum,ia tricks kama za pasco.....kwa kifupi jamaa naweza kuwa mwanasiasa kwani anweza kuwahadaa watu.
 
...sad watu wanaingizwa laini kirahisi rahisi hivi, Pasco hapa kapiga usanii tu usanii sawa sawa na ule wa NEC, usanii wa kisisiemi sisiemu kubadili miongozo kwa manufaa yao.....!

Hakuna msamaha wowote ameomba Pasco hapo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom