Tanzania Ruzuku ya vyama vya siasa inatolewa kwa mujibu wa sheria au kwa hisani ya Mhe. Rais?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Nimemsikia Kinana kila jambo hata lililowekwa kisheria anasema Mhe. Rais kafanya.....naomba wataalam wa sheria watusaidie; Ruzuku ya vyama vya siasa utolewa na Rais? Kwa sheria gani inayompa rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha siasa kugawa Ruzuku?

Kama hakuna kifungu cha sheria kinachompa mamlaka Raisi kugawa Ruzuku, HIZI BILIONI 2.7 zilizopelekwa Chadema zilipelekwa kwa masharti gani? Je, zilitolewa kwenye akaunti ya chama cha mapinduzi au akaunti binafsi ya Mhe. Rais?

Kama Mzee kinana anaweza kuwa mwongo kiasi hiki unategemea aweze kuongoza maridhiano ya kitaifa? Kwamba yeye anaamini kuachiwa wa wanachama 400 waliofungwa kisiasa na kutoa bilioni 2.7 zinatosha kuwanyamazisha chadema?

Kama walidhani chadema itanyamaza kwa kudai na kupewa haki yao basi bora waamue sasa kutokuendelea kuamini hivyo. Haki zao watapata na maandamano yakipinga uonevu yataendelea.......
 
Back
Top Bottom