Nawaomba radhi wana CHADEMA, nilimwelewa vibaya Mhe. Mbowe - Pasco

Kwa kawaida kwa mtu makini unapoomba radhi lazima uweze grounds za hoja zako haitoshi tu kusema naomba radhi. Lazima Pasco ni mtu makini sana na mstaarabu!
 
Pasco huna maana kabisa unaomba samahani kweli wewe zuzu

Lini JF imekuwa kituo cha reconciliation...

Simama kwenye kitu unachoamini ...hata kama wote hawataki huo ndio uongozi wa maana.
 
Pasco huna maana kabisa unaomba samahani kweli wewe zuzu

Lini JF imekuwa kituo cha reconciliation...

Simama kwenye kitu unachoamini ...hata kama wote hawataki huo ndio uongozi wa maana.


Rudia kusoma tena na tena, kuanzia heading mpaka mwisho, tuone kama unachosema ni sahihi. Something is wrong in your thinking, au utakuwa umevamia tu na kutoa statement bila kusoma, which is not the quality of Great Thinker.
 
Rudia kusoma tena na tena, kuanzia heading mpaka mwisho, tuone kama unachosema ni sahihi. Something is wrong in your thinking, au utakuwa umevamia tu na kutoa statement bila kusoma, which is not the quality of Great Thinker.

Na wewe umekuwa mwalimu wa nidhamu JF..

Kuomba msamaha kwa jambo unaloamini ni uzuzu period
 
Na wewe umekuwa mwalimu wa nidhamu JF..

Kuomba msamaha kwa jambo unaloamini ni uzuzu period


Wewe ndio zuzu, sababu Pasco hajaomba msamaha sehemu yoyote. Tatizo ni uwezo wako mdogo wa kuanalyze alichoandika Pasco, from the heading to the text itself. Tatizo ni uelewa wako sio mwandishi.
 
Pasco;

Sikuwahi kusoma post yako ya kwanza kuhusu aliyosema Mbowe na wala sijawahi kupata muda wa kusoma ile ya Regia na majibu yake; vile vile sikusoma post yako yote hapo juu. Hata hivyo abstract na conclusion za post yako hiyo zimenifurahisha sana. Kukubali makosa na kuyarekebesha ni uungwana ambao wanasiasa wetu hawana. Wangalikuwa na uungwana huo angalau tungekuwa tumesogea mbele kidogo kwani serikali ingelikuwa hairudii rudii makosa.
 
Big up Pasco, pride has to be swallowed sometimes. You are showing the way.

Haya mambo ya expressly or impliedly... sijui ni kimombo ndo kinanipita? Mfano, hivi Obama alitoa Tamko, au Alimpongeza Mheshimiwa baada ya kuchaguliwa, au hakumpongeza? Najaribu kulinganisha mazingira na/au matumizi ya maneno, huku ukiwa umebeba/umeficha maana nzito nyuma yake...

Jikumbushe: Tamko la Rais Obama Kuhusu Uchaguzi wa Tanzania (Novemba 13, 2010)
 
Pasco kukubali kukosolewa na kuomba samahani ndio ustaarabu wenyewe. Ni tofauti na pale rais wetu alipoomba radhi mbele ya mabalozi kuhusu mauaji ya Arusha then anawapiga vijembe watanzania afterwards! Huu si ustaarabu!
Nimekuweka kati ya watu muhimu sana hapa JF
 
MSAMAHA SIO SABABU YA KUFANYA KOSA,
WATANZANIA WENGI WANA FANYA MAKOSA MAKUSUDI KWA SABABU WANATEGEMEA KUOMBA MSAMAHA SAAS HILI NI TATIZO NA MIMI SIKUBALIANI NALO

JITAHIDI ,KUWA MAKINI,FANYA UCHUNGUZI WA KINA KABLA YA KUSEMA AU KUANDIKA CHOCHOTE,KWANGU MSAMAHA SIO TIBA KWANI HATA POLISI WETU WANAUA HALAFU WANAOMBA MSAMAHA SASA HII INA FAIDA GANI KWA MAREHEMU

badilika msamaha sio TIJA
Sahihi, kuwepo kwa nafasi ya kuomba msamaha sio sababu ya kufanya kosa na anayeomba msamaha hana adabu kwa sababu alifanya kosa mwenye adabu anajitahidi kuzuia kufanya kosa.
Kuwa makini
 
Ninacho kielewa mimi CDM wanamtambua rais ila hawazitambui kura zilizo mfanya kuwa rais.
Kwa sababu katiba inasema tume ya uchaguzi ikisha mtangaza rais hakuna anayeweza kupinga kwa njia yeyote kutokana na kipengele hicho CDM wanalazimika kumtambua rais ila hatutambui kura zilizomfanya kuwa rais.
I stand to be corrected
 
Waandikie pia barua ya kuomba msamaha. Kuna post moja ulipost huko nyuma nafikiri mwaka jana kuhusiana na mgawanyiko wa vyama vya upinzani, watu walicriticise sana ukaomba msamaha. Leo tena unaomba msamaha kwa issue nyingine. Mkuu inabidi uwe makini or stick with what you say. Wahenga wetu walisema kufanya kosa si kosa bali kurudia kosa ndio kosa. You need to learn from this then. A great thinker needs to be very careful with what they say to avoid saying sorry latter.

Hakuna makosa kuomba msamaha, but doesn't look good when you say sorry most of the time. And this especially when your signature say that "Principle ya uchangiaji wangu ni kuongea nothing but the truth kwa kuzingatia truthfulness, accuracy, objectivity, impartiality, fairness, na balance nikiweka mbele maslahi ya taifa.". Anayesema ukweli hawezi kuomba misamaha mara kwa mara.
 
Inatakiwa kuwa waangalifu zaidi kujadili hoja hii maana ni rahisi kuteleza na kulowana tope ambalo mwenzako ameamua kunawa ili awe safi. Muda haudanganyi, kaomba msamaha na kaeleza alichojifunza, sasa kama hukubaliani na jinsi alivyo "present" ombi lake la msamaha hilo ni jambo tofauti lakini usikatae kuwa hajaomba masamaha. Ukivumilia utafahamu kama kaomba radhi kweli au la. Naamini hawezi rudi hapa akakana kuwa hakuomba msamaha. Ila muhimu ni kuelewa na kukiri tu kuwa ni wengi sana hawakuelewa vizuri cdm walimaanisha nini. Tena Pasco nampongeza sana maana alipogundua hilo alihisi kuwa wapo wengi waliotetereka kama yeye akajaribu kuliweka wazi ili aone kama ataweza pia kusaidia wengine. Which is good! I do believe that baadhi ya wabunge wa CCM waliozomea ile siku wabunge wa CDm wanatoka nje ya ukumbi leo hii wameelewa umuhimu wa tendo lile kwa maendeleo ya baadaye ya siasa za nchi yetu. Ninahakika Kiwete pia alielewa baadaye ndiyo maana hawakukurupuka kuleta zile hoja walizoahidi kuleta bungeni. Watanzania tuwe makini kutafakari mambo yanayolihusu Taifa zima siyo yanayoridhisha kundi la watu au yanayotutoa kwenye tatizo la siku moja.
 
- Mkuu saafi sana mkuu nothing but uungwana, na viongozi wetu wangejifunza kutuomba radhi wananchi wanapokosea, ingesaidia sana kupunguza tension zisizo na faida kwa taifa, kwa mfano kiongozi wa taifa kunukuu Biblia kuhitimisha matendo ya serikali badala ya kutumia katiba ya Jamhuri!

- Ubarikiwe sana mkuu!, SALUTE!


William, @ NYC, USA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom