BoyOfGod
JF-Expert Member
- Jan 3, 2019
- 483
- 641
Habari wakuu!
Mimi ni kijana ambaye ni mzalendo na Mpenda kusimamia ukweli
Kiufupi sina chama chochote cha siasa ila nimekuwa anti-CCM kwa Muda mrefu isipokuwa kipindi cha magufuli(mambo mengi nilimwelewa)
Kiukweli maandamano ya chadema ni maandamano ya ambayo sijayaelewa maana hayana kichwa wala miguu.
Na moja kati ya hoja za hovyo zinazonifanya nisikitishwe na Chadema ni Hoja ya kuwa na Wabunge 740 badala ya Wabunge 360.
Mh. Mbowe ameonyesha dhahiri ulafi wa madaraka na kutanguliza maslai ya chama kuliko taifa
Nimefuatilia hotuba ya mbowe, Nimegundua unafki aliounyesha dhahiri alipodai Serikali ya CCM ni Serikali ya anasa, kwani hutumia Pesa hovyo hovyo kwenye mambo yasiyo ya msingi, anasema hayo huku wakiwa wametoa hoja ya kuongezwa kwa Wabunge (shame)
Kama haitoshi anakuja kusema Serikali ipunguze kodi(tozo) (shame again)
Chadema wameonyesha dhahiri kuwa sio watu wa Shukran , kwa hoja yao nyingine ya kutaka makonda afungwe Kwani ni mhalifu
Wanasahau huruma za Rais samia zilifanya mbowe afutiwe kesi
Wamekosa hata ubinadamu na fadhila huku wakijinasibu na msemo wa uongo "NO HATE NO FEAR"
Kwani Rais Samia angeamua kumuacha mbowe ndani aseme Mimi sihusiki kwenye kesi ya kipindi cha Mwendazake angekuwa wapi.
Kitu nilichokiona ni kwamba, Chadema hawajali maslai ya taifa hili hata kidogo isipokuwa matumbo yao
Wanajua kuwa wakiendelea kukaa kwenye maridhiano watakosa nguvu ya kuipinga CCM hata kama kinachofanywa na CCM ni chema
Wameona nguvu yao ipo kwenye chuki na ugomvi
Inshort hawaeleweki wanataka nini
Ingekuwa heri kama wameunga mkono 100% maandamano ya akina Mwabukusi
Ila wao kwa jeuri yao na kupenda kunyenyekewa hawakusupport 100%
Nawaomba Sana chadema wafute hoja hii vinginevyo watapoteza kila kitu na
watapoteza Imani kwa watanzania
Kama mtu unajiamini una hoja za msingi za kupinga Kwanini ukatae mdahalo
Unaambiwa mdahalo unajibu huyo ni mhalifu Makonda kaeleza kuwa kati ya hoja 84 hoja 63 tayari zimefanyiwa kazi
Tuseme hizo zilizobaki ikiwepo na hiyo ya Wabunge ndio zinafanya waandamane??
Nimesikitika sana