Nape Nnauye: Tumehujumiwa..

There are worse things that can happen in life than losing in election, but we all know the pain we can feel after a difficult loss, or even the joy we feel after a great win. This game (uchaguzi) is one of joy and pain. If you want to feel the joy, you must be willing to suffer. Sasa kama hamkuwa kushindwa na kuugulia machungu yake hii basi msingeshiriki kabisa

This game is not a matter of life and death - it only feels that way sometimes! Sasa ni wakati wenu ( CCM) kuikubali hali hii na mjisikie wenzenu wanavyojisikia wanaposhindwa, tena mbaya zaidi wanaposhindwa kwa uhuni wenu wa kupika matokeo.

Hongera CHADEMA kwa ushindi
Moto uwe huo huo hadi 2015
 
Ni raha ilioje kwa wananchi kushinda katika uchaguzi.. Juu ya mazingira ya haki kutokuwapo bado wananchi wamechagua kile wanachoamini.. Wako radhi kucheleweshewa maendeleo yao lakini CCM waondoke madarakani.. Nape kudai kuna hujuma ni kujaribu ku-justify kwamba wameshindwa kwa matatizo yao ya ndani.. wakati ukweli ni kwamba wameshindwa kwa kuwa wameshindwa kuwaletea maendeleo wananchi kwa miaka 50 waliokuwa madarakani.. Wananchi wamewachoka..
 
Haya MANENO NI YAKO NA WALIOKUTUMA KUSEMA HAYA SIJAWAHI KUTAMKA MANENO HAYA, UWE NA AIBU WALAU KIDOGO KUZUSHA UONGO......



Katibu Mwenezi wa CCM,Nape Nnauye amekaririwa akidai kuwa kushindwa kwa CCM kxatika uchaguzi wa Ubunge wa Arumeru Mashariki kumetokana na hujuma.

Nape alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa na Kagenzi na kuonyesha kuwa Joshua Nassari wa CHADEMA ameibuka mshindi.

Nape amedai kuwa kulikuwa na watu wasiokubalika kwenye jamii katika uchaguzi huo ambao ndio waliosababisha kushindwa kwa CCM.

Hata hivyo, Nape hakuwataja watu walioihujumu CCM uchaguzini.

Alisema kwa kuuliza: "Mbona Igunga hatukushindwa?'.

Alionekana amepagawa...
 
Ndugu Nape,watanzania wa leo wanahitaji maendeleo ya kweli,watu wamechoshwa na siasa uchwara za kuchafuana,kijana Nassari amechaguliwa kwa kuuza sera za CDM vizuri,bado wa-TZ wanahitaji mabadiko zaidi ya hayo,
kila la kheri Nassari
 
Haya MANENO NI YAKO NA WALIOKUTUMA KUSEMA HAYA SIJAWAHI KUTAMKA MANENO HAYA, UWE NA AIBU WALAU KIDOGO KUZUSHA UONGO......

Okey afathali umekuja, hebu sema maneno yako hapa ili usizushiwe tena.
Unauzungumziaje matokeo ya chaguzi zote za jana???
 
Kaka daudi mchambuzi vp ume amini ile dhana kua ccm inapata ushindi katika maeneo wanayo ishi watu wajinga na masikini

mkuu, werevu hawawezi kuichagua CCM kamwe.
Tulianza na mungu tunamaliza na mungu.
CCM walianza kwa matusi na sasa wanamaliza kwa matusi.
 
Nape umehujumiwa na nani, Labda gamba halijatoka, na usipoangalia na wewe utavaa gamba muda si mrefu.

Kuruhusu Lowasa kupanda jukwaani arumeru ni sawa na CCM nzima kuvaa gamba.
Ukiona kijana anashabikia CCM ujue kuna walakini katika malezi yake hasa ya utotoni.
 
Nakubaliana na Nape kwa aslimia 100++ kwamba kuna hujuma, cdm au chama chochote pinzani hakiwezi kushinda mbele ya serikali yote, tume ya uchaguzi, wana usalama na zaidi ya yote jeuri ya pesa..

Hakika Mungu amewahujumu na hawana budi kulalamika ila tatizo lao hawajui aliyewahujumu, wanaweza kuanza na mkurugenzi kwa kumhamisha kituo cha kazi wakati kuihalisia huyo sie..
 
NAPE TOFAUTISHA USHINDI WA KUPIGIWA KURA NA USHINDI WA KUIBA KURA!! IGUNGA MLISHINDA KWA KUIBA KURA JAMBO AMBALO LINAWAFANYA MSITAMBUE HALI HALISI YA CHAMA CHENU!! MNGEACHA KUIBA KURA PAMOJA NA KUTUMIA VYOMBO VYA DOLA then MNGEWEZA KUTAMBUA HALI HALISI YA CHAMA CHENU!! KWA SASA KATI YENU NYOTE MLIOKO JUU HAKUNA HATA MMOJA ANAYETAMBUA HALI HALISI YA CCM KWA SABABU KUU MATATU:-
1. MMEPEANA MADARAKA KI-NDUGU HIVYO KUPUNGUZA WIGO WA UTAMBUZI WA MAMBO
2. MNAPOOMBA USHAURI WA VYOMBO VYA DOLA MNATUMIA VITISHO HIVYO KUWAFANYA WAWASHAURI MAMBO AMBAYO MNGEPENDA KUYASIKIA.
3. kILA MNAPOIBA KURA MNAOGOPA KULICHADILI KWA PAMOJA MKIOGOPA KUPOTEZA UMAARUFU WA MTU MMOJA MMOJA!

Unafikiri kunamtu atakuelewa pale.
 
Hayo ya kuhujumiwa au la tuwaachie wana ccm kwa sasa! nafikiri CDM ni muda muafaka kuanzia sasa hivi kuanza 2015 wining campaign. katika vijana 12 ambao ni marafiki zangu na wapenzi wa CDM,ni vijana 3 tu wenye vitambulisho vya kupigia kura na ni 2 tu wenye kadi za uanachama. nafikiri kampeni unit ya CDM ianze kucheki hili sasa kuhakikisha siyo watu wanakipenda kwa mdomo tu ila wanavitambulisho vya kupigia kura na kadi za uanachama. Tukianza sasa hivi tutakuwa na pressure ndogo sana wakati wa 2015 campaign. Let start at very low screening wanachama kwa wetu walio active with vitambulisho na kadi. ni maoni tu!
 
Katibu Mwenezi wa CCM,Nape Nnauye amekaririwa akidai kuwa kushindwa kwa CCM katika uchaguzi wa Ubunge wa Arumeru Mashariki kumetokana na hujuma.

Nape alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa na Kagenzi na kuonyesha kuwa Joshua Nassari wa CHADEMA ameibuka mshindi.







Nape amedai kuwa kulikuwa na watu wasiokubalika kwenye jamii katika uchaguzi huo ambao ndio waliosababisha kushindwa kwa CCM.

Hata hivyo, Nape hakuwataja watu walioihujumu CCM uchaguzini.

Alisema kwa kuuliza: "Mbona Igunga hatukushindwa?'.

Alionekana amepagawa...

Kula CCM, kura CDM - Yametimia.
 
Back
Top Bottom