Nape Nnauye: Tumehujumiwa..

hadi sasa hatuamini kama Igunga CDM ilishindwa ndiyo maana kesi ipo mahakamani si vizuri Kuingilia kesi zilizoko mahamani yasije yakamkuta ya Arusha tena au kwa sababu alisingizia kuumwa
 
Naamini huu ni mwanzo tu,mageuzi makubwa yanakuja mbele yetu na Ccm iwapo haitorekebisha mapungufu yake kuingia ikulu 2015 ni ndoto.
Karata ya kujivua gamba ilikuwa ilikuwa sahihi kuitekeleza kwa vitendo ili kurudisha imani ya wananchi lakini walishindwa kuitumia na wanazidi kulindana. Na bado,mpaka kieleweke 2015.
 
Kauli ya nape ni kauli ya ulofa. Mbona yeye alishindwa kura za maoni Ubungo na hakudai kuwa alihujumiwa? Kila mtu atakuja na kauli yake. CCM mufilisi kabisa.
 
Katibu Mwenezi wa CCM,Nape Nnauye amekaririwa akidai kuwa kushindwa kwa CCM katika uchaguzi wa Ubunge wa Arumeru Mashariki kumetokana na hujuma.

Nape alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa na Kagenzi na kuonyesha kuwa Joshua Nassari wa CHADEMA ameibuka mshindi.

Nape amedai kuwa kulikuwa na watu wasiokubalika kwenye jamii katika uchaguzi huo ambao ndio waliosababisha kushindwa kwa CCM.

Hata hivyo, Nape hakuwataja watu walioihujumu CCM uchaguzini.

Alisema kwa kuuliza: "Mbona Igunga hatukushindwa?'.

Alionekana amepagawa...

Huwa sijui kwanini Nape alipewa nafasi nyeti ndani ya chama kama hii wakati akiwa na uwezo mdogo wa kujenga hoja na kufikir! Anajifanya hajui kuwa Igunga walichakachua!

Hawa ndo walevi wa madaraka ndani ya CCM. Watakuwa wanashangaa nchi inachukuliwa na kukombolewa bila wao kujua watajikuta kizuizini.
 
Kwanza nataka kutofautiana na Nape kwamba Igunga walishinda, ukweli ni kwamba Chadema ndio ilioshinda Igunga walichofanya ni wizi mtupu sasa mbinu zote zimejulikana na zimewekwa wazi na kuanzia sasa watalala doro kila uchaguzi watu wamechoka
 
Hivi huyu bwana cheo chake si ni itikadi na UENEZI?? Sioni ajabu anavyoeneza...anafanya kazi yake.
Anasema mbona Igunga walishinda.....akumbushwe kuwa hii haikuwa Igunga ni Arumeru!! Watu tofauti kabisaaa.

Halafu, kama wazee wa khanga, kofia na "wallet" wametumia nguvu kubwa vile kule Arumeru kumnadi bwa mdogo, wakati wa kumpigia kampeni mgombea wao wa urais 2015 si watamwomba OBAMA aje na viongozi wote wa G7???

Ingikuwa nipo kwenye safu ya wanaojulikana kama vigogo wa chama twawala.....ikifika Desemba 2014 NASTAAFU MAMBO YA SIASA.

Namalizia hivi....People's power, God with us!
 
pipooooooooooooooooooos Nape karibu CDM ila ukija hatukupi cheo chochote kwa sababu mnafiki ulisema EL gamba bado ukampeleka kumnadi SIWOWI MSUMARI kweli??????????????????????????? Haya mbaya zaidi Nape mnataka nchi hii ya kurithishana wewe baba yako alikuwa kiongozi, SIWOSI baba yake alikuwa kiongozi, nanihiii nae hivi hivi wakati tupo na tuliomaliza ma phd tumetulia na ajira issue kweli halafu mnataka kupenndeleana tu hakuna ishieni huko ubunge wa AFRIKA MASHARIKI WATOTO WA VIGOGO WAPENI ILA SIYO KWENYE KURA ZA WANANCHI. MWANZO WA ANGUKO LA CCM
 
Igunga uelewa wao bado haujafikia kiwango ndiyo maana kampeni za stail ya Lusinde zinaweza kufanikiwa huko. Ila kule Arumeru walimuona ni chizi na alipaswa awe Mirembe ndiyo maana wakaamua kuwaadhibu ccm na kikundi chao cha akina prof maji marefu! Watanzania wa ARumeru nao wameamka sasa hawataki tena kuendelewa kudharauliwa kwa stail ya kampeni za Huyo bwana Lusinde na akina BM na Steven Wassira (Tyson)!
 
Nape ameamua kusema chama kimehujumiwa, baada ya kukosa maneno ya kusema. Hivi awali alipotamba kuwa chama chake tayari kimeshashinda katika uchaguzi huo hata kabla ya siku ya uchaguzi hakujua kama wananchi ndio wanaoamua nani awe mbunge wao?. Au alifikiri yeye ndo kila kitu.
 
Ulinzi wa chopper si mchezooo!maana matokeo ya awali yalipokuwa yanatangazwa mi akili yangu yooote ili kuwa inashughulika na ulinzi tu najiuliza makamanda watazuia hujuma? nafikiri tuitumie arumeru kama blue print ya 2015.
 

Anamaanisha Lusinde hakubaliki katika jamii?

Sidhani; kwani Lusinde pia si ali-kampeni Igunga? Pia ningependa kufahamu kwani Rostam anakubalika kwenye jamii? Mbona alikampeni Igunga? By the way Rostam na Lowassa nani anakubalika zaidi? Ningeelewa kidogo kama mtu angezungumzia tofauti za uelewa kati ya watu wa Igunga na Arumeru.
 
Naomba vikao vinavyohusika cdm vikae mara moja kupitisha hili. Ukishapiga kura kaa mita 103 kulinda kura yakoo.......... Sehemu zote ambazo hatukulinda walichakachua. .. Tulizolinda kama arumeru, arusha mjini, ubungo mwanza etc walitupiga mabomu, risasi na nk lakini at last walishindwa kuchakachua
 
Tumemsikia Nape Ch. 10 amekuwa mkweli. Tena mkweli kupita kiasi. Kwa hili asibebeshwe mzigo wa mtu kumtetea mkwewe, wa watu tulio waamini kuhubiri ukabila na matusi, kututönesha kidonda kilichoanza kupoa cha kifo cha mwalimu, kutoa laana kwa mwana mwenye wazazi, timu ya watu waliopotea. Waliokosa katibu mkuu makini ambaye hajui awe wapi. Tulimsema mzee Yusufu haya hao wasomi wako wapi? Nape tumia nafasi hii kubadili mwelekeo wa chama kwa kusema makosa bila woga labda wana ccm wakweli watakuelewa.
 
Back
Top Bottom