Nape asema utakuwa mtu wa ajabu sana ukiamini kuwa CCM hutoa takwimu sahihi kwa umma

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameibua mjadala kwenye mtandao wa X baada ya kusema kuwa amefanya kazi makao makuu ya CCM kwa takriban miaka 20, na mtanzania atakayepata takwimu zozote zinazokihusu chama hicho na akazimini atakuwa mtu wa ajabu.

“Mpaka report ikufikie wewe ya CCM bado ukaamini iko hivyohivyo utakuwa wa ajabu sana. CCM haifanyi Kazi hivyo, nimefanya Kazi makao makuu miaka Karibu 20, CCM ni zaidi ya unavyoiona nje” amesema Nape.

Waziri huyu ametoa hoja hii wakati akijibu hoja ya mtumiaji mwingine wa mtandao huo aliyekosoa takwimu alizotoa Septemba 19, 2023 mbele ya Raid wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwanba ni 16% pekee ya Watanzania ndio hutumia mitandao, na kati yao 40% ni diaspora hivyo asiwe na wasiwasi na kelele zao, hivyo atashinda uchaguzi ifikapo mwaka 2025.

“Mheshimiwa umeridhika sana, unatema mambo ya ajabu mtandaoni, now unathibitisha kwamba CCM ni wataalamu wa kudanganya au kupika data, huoni unakipika chama chetu?? Unafeli sana, unajali maslahi yako tu, hujali maslahi mapana ya nchi, ma raia wake. Nyie ndio mnaharibu chama chetu” alisema mchangiaji mmoja akikosoa hoja hii ya Nape.

“Hatupiki lakini ikikufikia wewe document Kama hiyo lazima iwe fake” alijibu Nape.

IMG_8543.jpeg
 
Nape mwenyewe ni fake. Si mnajua babake ni nani? Kwa nini atumie jina la Nnauye badala ya Mwandosya? Kwani angepungukiwa nini?

Nape kila siku amekuwa fake kwa kila kitu, kuanzia jina mpaka matendo yake. Na anayafurahia maisha ya namna hiyo. Kwa ufahari kabisa, aliwahi kutamka kuwa CCM itashinda kwa goli la mkono.
 
Chama cha mapinduzi ndicho chama pekee kilicho na taratibu safi kwa ngazi zote, kuanzia kwa mwenyekiti mpaka ngazi ya shina na mjumbe!
-Hayo mengine ni ya vijiweni tu.
Dosari za watu wachache zisituchafulie chama chetu.
 
Nape mwenyewe ni fake. Si mnajua babake ni nani? Kwa nini atumie jina la Nnauye badala ya Mwandosya? Kwani angepungukiwa nini?

Nape kila siku amekuwa fake kwa kila kitu, kuanzia jina mpaka matendo yake. Na anayafurahia maisha ya namna hiyo. Kwa ufahari kabisa, aliwahi kutamka kuwa CCM itashinda kwa goli la mkono.
Masikini mzee Mussa aliuziwa mbuzi kwenye kiroba,yule mama wa Kinyirimba Mungu anamuona.
 
Kumbebabake ni nani? Kwa nini atumie jina la Nnauye badala ya Mwandosya? Kwani angepungukiwa nini?
Kumbe
 
Back
Top Bottom