Nape Nnauye: Tumehujumiwa..

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Katibu Mwenezi wa CCM,Nape Nnauye amekaririwa akidai kuwa kushindwa kwa CCM katika uchaguzi wa Ubunge wa Arumeru Mashariki kumetokana na hujuma.

Nape alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa na Kagenzi na kuonyesha kuwa Joshua Nassari wa CHADEMA ameibuka mshindi.

Nape amedai kuwa kulikuwa na watu wasiokubalika kwenye jamii katika uchaguzi huo ambao ndio waliosababisha kushindwa kwa CCM.

Hata hivyo, Nape hakuwataja watu walioihujumu CCM uchaguzini.

Alisema kwa kuuliza: "Mbona Igunga hatukushindwa?'.

Alionekana amepagawa...
 
Ni kweli kauli ya SENDEKA ya kuendekeza ukabila na ile ya LUSINDE kumwaga matusi zaidi ya mlevi wa gongo hata kama mimi ningekuwa mpiga kura wa Arumeru nisengekipigia kura chama cha namna hiyo.

Wawatumie watu wenye staha na lugha njema kwenye kampeni zao
 
Mdwanzi, hakuliona hilo wakati wanatukana majukwaani!! Na huu ni mwanzo tu, wandhani watanzania ni wajinga na wanarubuniwa kwa vijihela, kanga na kofia zao.
Ole wao, siku inakuja na watalipia kwa maovu yote waliyo na wanayowanfanyia Watanzania, come 2015!
 
..yote 9..kumi ni ccm chaliii..dadeek,hakuna cha hujuma wala nin,na uo ni mwanzo tu!wawadanganye uko uko vijijin ambao hawajafunguka macho..ila wajue wakija mjini imekula kwaoo..im so happy 4CDM..So so happy! Mwendo spidi240,ileile ad 2015 ..na igunga c arumeru vijana arusha wana ulinzi zaid yaulinzi..kabwa ad penat,no uchakachuz.com..********!
 
Nape ajue kuwa Igunga walishinda kwasababu Chadema hawakutumia chpper kuthibiti wizi!! Sasa Nape ameshindwa kuiba vizuri Arumeru aende akawaibie magamba wenzie kwenye uchaguzi wa magamba wa kuteua wagombea wa ubungee wa E.A ambao yeye na fisadi Kinana wanasimamia!! Hawa jama wanaibiana hata wao kwa wao. Chadema next stop Segerea kwenda kumvua fisadi Mahanga , kijakazi mwingine wa EL!!
 
huo ni upumba.vu tu. sasa kama watu hao hawakubaliki katika jamii kwanini ccm inaendelea kuwa nao? nape anadai lowassa na rostam wanapaswa kufukuzwa uanachama, halafu baadaye anaonekana nao majukwaani wakipiga kampeni. subirini chaguzi za kanda ya ziwa nawahakikishia nape atapanda jukwaani na andrew chenge kuombea kura wagombea wa ccm.
 
Ni kweli yale yaliyosemwa na Lwaitama kuwa ushindi au kushindwa kwa CCM huko Arumeru kutazua mengi zaidi ndani ya CCM, yaani yote yalikua ni hatari, akasema kama CCM wangeshinda basi wale wa kundi la akina fuklani wangesema ...mmeona mtu wetu huyu anakubalika na kwamba kampeni za kumvua gamba zilikua ni visa na kushindwa kwa CCM ni mzozo mwingine kuwa mmepeleka mtu asiekubalika kwa jamii ndio maana tumeshindwa na hivyo kampeni ya kuvuana gamba itapata nguvu tena huku kundi fulani likfaidika dhidi ya maumivu ya kundi jingine, kimsingi makundi ndio kifo cha CCM na kwa ushindi huu wa CDM basi ni wazi hata Mhe Mwenyekiti ana wakati mgumu
 
Ni kweli yale yaliyosemwa na Lwaitama kuwa ushindi au kushindwa kwa CCM huko Arumeru kutazua mengi zaidi ndani ya CCM, yaani yote yalikua ni hatari, akasema kama CCM wangeshinda basi wale wa kundi la akina fuklani wangesema ...mmeona mtu wetu huyu anakubalika na kwamba kampeni za kumvua gamba zilikua ni visa na kushindwa kwa CCM ni mzozo mwingine kuwa mmepeleka mtu asiekubalika kwa jamii ndio maana tumeshindwa na hivyo kampeni ya kuvuana gamba itapata nguvu tena huku kundi fulani likfaidika dhidi ya maumivu ya kundi jingine, kimsingi makundi ndio kifo cha CCM na kwa ushindi huu wa CDM basi ni wazi hata Mhe Mwenyekiti ana wakati mgumu. Mwacheni MUNGU aitwe MUNGU
 
NAPE TOFAUTISHA USHINDI WA KUPIGIWA KURA NA USHINDI WA KUIBA KURA!! IGUNGA MLISHINDA KWA KUIBA KURA JAMBO AMBALO LINAWAFANYA MSITAMBUE HALI HALISI YA CHAMA CHENU!! MNGEACHA KUIBA KURA PAMOJA NA KUTUMIA VYOMBO VYA DOLA then MNGEWEZA KUTAMBUA HALI HALISI YA CHAMA CHENU!! KWA SASA KATI YENU NYOTE MLIOKO JUU HAKUNA HATA MMOJA ANAYETAMBUA HALI HALISI YA CCM KWA SABABU KUU MATATU:-
1. MMEPEANA MADARAKA KI-NDUGU HIVYO KUPUNGUZA WIGO WA UTAMBUZI WA MAMBO
2. MNAPOOMBA USHAURI WA VYOMBO VYA DOLA MNATUMIA VITISHO HIVYO KUWAFANYA WAWASHAURI MAMBO AMBAYO MNGEPENDA KUYASIKIA.
3. kILA MNAPOIBA KURA MNAOGOPA KULICHADILI KWA PAMOJA MKIOGOPA KUPOTEZA UMAARUFU WA MTU MMOJA MMOJA!


Katibu Mwenezi wa CCM,Nape Nnauye amekaririwa akidai kuwa kushindwa kwa CCM katika uchaguzi wa Ubunge wa Arumeru Mashariki kumetokana na hujuma.Nape alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa na Kagenzi na kuonyesha kuwa Joshua Nassari wa CHADEMA ameibuka mshindi.

Nape amedai kuwa kulikuwa na watu wasiokubalika kwenye jamii katika uchaguzi huo ambao ndio waliosababisha kushindwa kwa CCM.Hatahivyo,Nape hakuwataja watu walioihujumu CCM uchaguzini.Alisema kwa kuuliza:'mbona Igunga hatukushindwa?'.Alionekana amepagawa...
 
Wako wapi wale wana-CCM waliotukana na wale waliotumiwa hapa jukwaani kutukana? sijaona hata mmoja, ziko wapi mimba za Chadema alizzisema Lusinde? Wako wapi Mashoga aliowasema Lusinde? Uko wapi uchungu aliousema Lusinde dhidi ya Mbowe? Uko wapi Ubabe wa Lusinde kwa Mzee Slaa kuwa anaweza kumpiga ngumi moja tu? Uko wapi ule ukosefu wa akili ulionyeshwa na viongozi hawa wa CCM??????? Hakika malipo mengine hulipwa hapa hapa
 
Nape !!!!!!!!!!!! Nape!!!! Hayo magamba yatawamaliza kudadeki !! Nyie mnadhani watu wamelala siku hizi , hizi enzi sio za mwaka 47 Hayo magamba yatawaondoa hizo ni rasha rasha , 15 mnasepa tu
 
Katibu Mwenezi wa CCM,Nape Nnauye amekaririwa akidai kuwa kushindwa kwa CCM katika uchaguzi wa Ubunge wa Arumeru Mashariki kumetokana na hujuma.Nape alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa na Kagenzi na kuonyesha kuwa Joshua Nassari wa CHADEMA ameibuka mshindi.

Nape amedai kuwa kulikuwa na watu wasiokubalika kwenye jamii katika uchaguzi huo ambao ndio waliosababisha kushindwa kwa CCM.Hatahivyo,Nape hakuwataja watu walioihujumu CCM uchaguzini.Alisema kwa kuuliza:'mbona Igunga hatukushindwa?'.Alionekana amepagawa...

Nape anagundua leo kuwa kuna watu hawakubaliki kwenye jamii? Inapasa akubali kuwa chama chake hakikubaliki kwenye jamii kwa sababu kimefika mahali kimewasahau watu waliyokiweka madarakani. Walala hoi waliyo zoea kuwa nunua kwa kanga, kofia na fedha kila baada ya miaka mitano na wanawasahau kwa muda wa miaka minne au yote mitano isipokuwa kipindi cha uchaguzi.
Si amini kama Nape hajui kuwa wao ni watu wa maneno mengi bila vitendo na hapaswi kulalamika.
Hii ni Dalili na njema kwa CDM.
Hongereni sana wananchi wa Arumeru kwa kufanya maamuzi ya maana na kuonyesha kuwa kila jambo linawezekana kwa kila mtu kutimiza wajibu wake.
 
Na bado kama kuhujumiwa mtaenderea kuhujumiwa kumbe mkuki kwa guluwe kwa binanadamu mchungu
 
Hawawezi kukosa kisingizio. Najuwa hawatasingizia kuibiwa kwa kura zao, manake mwizi ni vigumu kuibiwa. Watasingiziana wao kwa wao, kulaumiana wenewe napengine lazima kuna magamba flani yatalazimika kujivua. Aibu tupu. Huenda wakamtupia lawama Lowasa.
 
Back
Top Bottom