Sifa zooooteee hizo je ana pesa? maana ndiyo sifa kuu yao.Kama ni Kapt. Jaka Mwambi basi CCM itabadilika na labda kuinusuru na kufika sehemu.
Balozi nchini Urusi. Mwanachama mzuri wa CCM. CCM ipo kwenye damu kabisa, huyu ni kweli ukimkata anatoka damu ya kijani na njano na bado anadumisha fikra za baba wa Taifa. Nikiwa na maana ya kuwa ni muadilifu, muogopa Mungu na Mzalendo wa kweli wa nchi yake. Wenye kumjua hamna atakayepinga haya.
Digrii yake ya kwanza amesomea Chuo Kikuu Dar es Salaam mlimani, Digrii yake ya pili yaani ya Masters ameipatia Chuo kikuu cha Kiev (Ukraine sasa) wakati ikiwa chini ya Urusi na naamini kabla ya mwisho wa mwaka atakuwa na stashahada yake ya udaktari.
Amekuzwa na chama, baada ya kumaliza shule alishika nafasi tofauti mkuu wa wilaya wa kinondoni, pwani (bagamoyo), masasi. Katika viongozi wa Kitanzania ambao wanaweza kujivunia rekodi yao basi Kapt. Mwambi ni mmoja ya hao wachache. Kwani yeye ndiye aliyeweza kuanzisha na kuleta mafanikio makubwa ya program ya Ondoa Njaa Masasi (ONJAMA) katika miaka ya themanini (tafadhali google uone mafanikio ya ONJAMA). ONJAMA imekuwa ni mfano wa kuigwa hapa nchini na duniani kote (UNESCO waliifagilia sana).
Amekuwa mkuu wa Mkoa wa Tanga na Rukwa. Sasa ni balozi nchini Urusi na ni balozi mwenye kusifiwa sana na Rais na Waziri wake kwani yeye ndiye mwenye kuongoza kwa mfano kitu alichotumwa na Rais wake, Diplomasia ya Uchumi.
Anaongea kirusi bila matatizo. Ni mtu wa Morogoro na mcha Mungu mzuri sana.
Kwa kweli huyu anatakiwa kuwa kwenye serikali kuu na sio kwenye chama wala ubalozini. Basi kama CCM watamfanya kuwa Katibu Mkuu na kumuachia afanye kazi yake basi naamini ataweza kuwasogezasogeza kwani ni mtu mwenye kupenda kuona matokeo.
La kuvunda halina ubani bana!
Hakuvunja secretariat kwa sababu imeshindwa kazi bali kwa sababu kumetokea hoja ya kutenganisha mkti na rais, fungukeni macho!
Basi abaki Makamba maana nikifikiria waropokaji ni yeye au Anna Kilango. Mamaaaa nilimsahau sofia simba. Llabda safari hii wafanye na gender balance
hadija Kopa!Nani anafaa? Anna Chilango?