Naamini kwa dhati kabisa nguvu ya Makonda haitokani na kuwa kwake katibu mwenezi wa CCM, lazima kuna chanzo kingine kinampa kujiamini kiasi hiki

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Niite jina lolote, lakini mimi ni mojawapo ya watu ambao huwezi hata kabisa kunishawishi kwamba hii nguvu na mbwembwe ambazo Makonda amekuwa akizionyesha zinatokana na kuwa kwake na cheo cha katibu mwenezi wa CCM. Tusidanganyane hapa.

Makonda sio katibu mwenezi wa kwanza CCM, na wamekuwapo wengine huko nyuma, lakini ni mara ya kwanza tunapata katibu mwenezi wa CCM ambae anaonyesha kujiamini kupita mamlaka yanayostahili ya katibu mwenezi wa CCM.

Leo hii katibu mwenezi awapigie simu mawaziri, amkebehi mwanasheria mkuu wa serikali, awaamrishe wakuu wa mikoa, ma-RPC, eti kwa sababu yeye ndie msemaji mkuu wa chama, hilo tu? Haiwezekani.

Leo hii katibu mwenyezi apewe bajeti, misafara ya magari, kuliko inavyokuwa kwa makamu mwenyekiti wa CCM au katibu mkuu wa CCM, kwa sababu gani? Kwamba katiba ya CCM imebadilishwa kisiri na hawa wote wameambiwa kuanzia sasa bosi wenu ni katibu mwenezi wa CCM? Pamoja na mawaziri? Wakuu wa mikoa? Mwanasheria Mkuu? Wenyeviti wa CCM wa mikoa?

Sote tunajua msemaji mkuu wa chama chochote anasema yale chama kilichoamua katika vikao vyake rasmi. Kuwa msemaji wa chama haina maana wewe ndio unakuwa unakisemea chama, hata siku moja. Kuwa katibu mwenyezi sio katika mpangilio wa vyeo vya chama, ni nafasi tu. Huwezi hata kusema katibu mwenezi wa CCM ni mkubwa kuliko mwenyekiti wa CCM wa mkoa. Lakini sio hivyo kwa Makonda. Yeye amejipa madaraka ambayo nadhani yanazidi hata ya kuwa makamu mwenyekiti wa CCM, au katibu mkuu wa CCM. Kujiamini huko kunatoka wapi? Mamlaka haya yanatoka wapi? Kwamba siku zote hatukujua kuwa katibu mwenezi wa chama ni mtu mkubwa namna hii? Ni kweli?

Nyie watu wa CCM, nyie mawaziri, nyie wakuu wa mikoa, tuambieni ukweli. Kinachowafanya muufyate Makonda akiunguruma ni nini hasa, Ukatibu mwenezi wa CCM? Na kwa nini sasa wenye akili tukiwauliza mbona mambo yako hivi, mnaishia kutabasamu tu bila kusema lolote? Kuna kitu gani msichotuambia?

Na niwaambie wazi nyie watu wa CCM. Kama nguvu ya Makonda sio ya kikatiba ndani ya CCM, kama kuna chanzo kingine kisicho rasmi kinampa nguvu na kujiamini kiasi hiki, basi anguko la CCM liko karibu sana!
 
Naona sasa mmeanza kuweweseka kama kawaida yenu. Hata kabla ya kuwa mkuu wa wilaya na baadaye mkuu wa mkoa kila mmoja hakufahamu majukumu ya nafasi hizo, pamoja na mamlaka yake katika kuchochea maendeleo.ni mpaka alipoteuliwa mwamba mwenyewe Mheshimiwa Makonda kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara.

Mheshimiwa Makonda ni kijana jasiri na anayetambua majukumu yake.afanyayo ni majukumu yake kabisa. Chama ndicho kilichounda serikali na siyo serikali iliyounda chama. Ni chama kinachokwenda kwa wananchi kuomba kura na siyo serikali inayokwenda. Ni CCM Ndio itakayoulizwa maswali majukwaani na wananchi na siyo serikali.serikali ikiharibu kinachochukiwa ni chama kilichounda serikali na ndicho kitakacho adhibiwa kwenye sanduku la kura wakati wa uchaguzi.

Sasa kwa akili yako unataka chama kikawa kimya? Unataka chama kinyamaze bila kuwasemea watanzania? Unataka chama kisiende kwa wananchi kuwasikiliza kero zao na kuwapa majibu? Unataka wananchi wasipelekee kero zao kwa chama walichokichagua wao wenyewe?

Kwa akili yako hiyo hiyo unafirikiri chama kikianguka hao wakuu wa mikoa watabaki? Hao mawaziri watakuwepo ? Hao madc na na Ded watabakia? Sasa kwanini wasikiheshimu chama kilichowapa nafasi hizo kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM? Kwanini wasikumbushwe wajibu wao na majukumu yao katika kuwatumikia wananchi?
 
Si Wapendi CCM, Simkubari Makonda kwa historia yake...!

Ila nakubaliana na anachokifanya, tena nilitamani angepata nafasi ya juu zaidi....!

Kama anaweza kuwafikia Wananchi na kuwasikiliza, hilo binafsi ni Muhimu sana, sisi hohehahe ndo tunataka, mtu atusikilize, pale tunapofukuzwa kwenye office za Umma, pale tunapoambiwa kama hujatoa kitu kidogo, kiwanja chako kinaenda kupotea, halafu anakuja mtu ananambia nieleze matatizo yako ntakusaidia, sisi tutampenda huyo....!

Kama nafasi yake haitambuliki kikatiba, hiyo sisi sio juu yetu, kama yeye sio kitu mbele ya Waziri ki cheo ama mbele ya Katibu Mkuu, hilo sisi hatujari, sisi tunajua kuna mtu ana nafasi huko CCM, anapita nchi nzima kujaribu kutatua changamoto zetu masikini...!

Hata kama kwa namna yoyote mkamwondoa, tutaendelea kuomba siku moja aje apatikane kiongozi kama yeye ambaye atatusikiliza...!

Kama anavunja Sheria hiyo sisi haituhusu, coz hata wanaofata sheria hawataki kutusikiliza...!

Makonda wewe ni Wapoti wangu, japo mimi sikukubari wewe kwa historia yako.... Ila piga kazi hivyo hivyo, mradi kuna Masikini wenzangu wanasaidika....!!!!
 
Naona sasa mmeanza kuweweseka kama kawaida yenu. Hata kabla ya kuwa mkuu wa wilaya na baadaye mkuu wa mkoa kila mmoja hakufahamu majukumu ya nafasi hizo, pamoja na mamlaka yake katika kuchochea maendeleo.ni mpaka alipoteuliwa mwamba mwenyewe Mheshimiwa Makonda kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara.

Mheshimiwa Makonda ni kijana jasiri na anayetambua majukumu yake.afanyayo ni majukumu yake kabisa. Chama ndicho kilichounda serikali na siyo serikali iliyounda chama. Ni chama kinachokwenda kwa kuomba kura na siyo serikali.

Kwa akili yako hiyo hiyo unafirikiri chama kikianguka hao wakuu wa mikoa watabaki? Hao mawaziri watakuwepo ? Hao madc na watabakia? Sasa kwanini wasikiheshimu chama kilichowapa nafasi hizo kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM?
Wewe naona uko gizani afadhali ungekaa kimya usijibu. Umelichukulia hili jambo kwa wepesi sana, kutekeleza ilani ya CCM? Ina maana ilani ya CCM imeanza kutekelezwa Makonda alipoteuliwa kuwa katibu mwenezi? Kama ndio hivyo basi Chadema wanasema ukweli, kwamba CCM mpo mpo tu hamjui mnalolifanya wala kusimamia.

Halafu wewe, sio kila anaeuliza jambo kuhusu CCM basi yeye ni Chadema.
 
Umesahau kuandika namba yako ya simu leo. Au una red eyes?
 
Si Wapendi CCM, Simkubari Makonda kwa historia yake...!

Ila nakubaliana na anachokifanya, tena nilitamani angepata nafasi ya juu zaidi....!

Kama anaweza kuwafikia Wananchi na kuwasikiliza, hilo binafsi ni Muhimu sana, sisi hohehahe ndo tunataka, mtu atusikilize, pale tunapofukuzwa kwenye office za Umma, pale tunapoambiwa kama hujatoa kitu kidogo, kiwanja chako kinaenda kupotea, halafu anakuja mtu ananambia nieleze matatizo yako ntakusaidia, sisi tutampenda huyo....!

Kama nafasi yake haitambuliki kikatiba, hiyo sisi sio juu yetu, kama yeye sio kitu mbele ya Waziri ki cheo ama mbele ya Katibu Mkuu, hilo sisi hatujari, sisi tunajua kuna mtu ana nafasi huko CCM, anapita nchi nzima kujaribu kutatua changamoto zetu masikini...!

Hata kama kwa namna yoyote mkamwondoa, tutaendelea kuomba siku moja aje apatikane kiongozi kama yeye ambaye atatusikiliza...!

Kama anavunja Sheria hiyo sisi haituhusu, coz hata wanaofata sheria hawataki kutusikiliza...!

Makonda wewe ni Wapoti wangu, japo mimi sikukubari wewe kwa historia yako.... Ila piga kazi hivyo hivyo, mradi kuna Masikini wenzangu wanasaidika....!!!!
NI wazi wewe huna ufahamu wa kutosha kuhusu majukumu ya chama na serikali katika utaratibu wa uongozi wa nchi. Msikilize Fatma Karume labda kuna jambo utaambulia pale.
 
Ufahamu huo baki nao wewe...!

Mimi sio Mwana siasa...!

Kilichofanya Maghufuri apendwe na Raia wa kawaida wa nchii hii, ni kwa sababu alikua anawasikiliza, alichofanya Maghufuri hata kingefanywa na PM, baada ya Maghufuri kufariki, angepata nafasi mioyoni mwa wananchi masikini.

Nkizulumiwa kiwanja nikaenda Mahakani nikashindwa kesi, baadaye nikaja kuambiwa ukiendelea mbele, tutaitoa roho yako, then kesho kuna kiongozi akaja akanisikiliza, Nikarudishiwa Kiwanja changu, hayo mambo ya Sheria na utawala Bora yatanisaidia nini....!?

Kama nilipewa Tenda na Minispaa na leo ni maka 10 nawadai hawataki kunilipa, hakuna office sijawahi kwenda mpaka mkoani, na hakuna msaada, then Mkurugenzi ananambia coz unapeleka malalamiko mpaka kwa mkuu wa mkoa, basi hutokaa ulipwe.... Then kesho anakuja Kiongozi kama Maghufuri ama Makonda, ananisikiliza, anatoa amri nilipwe, na kweli kesho yake nalipwa.....! Aaah...! Hayo mambo ya Sheria na Utawala bora baki nayo kwenye makaratasi....!

Wananchi masikini wanataka mtu wa kuwasikiliza na kutatua changamoto!

Ukitaka ku win mioyo ya Masikini, Wasikilize then tatua changamoto zao.... Simple!

Otherwise njoo na mambo yako uone kama sisi masikini tutakuelewa.

Mfumo mzima wa utawala nchii hii ulishaferi, na Viongozi hawana mawazo ya maana, ndo utakumbuka mawazo ya Mwanasheria mkuu mbele ya Rais, mawazo yasio na tija yoyote, Viongozi wa umma hawatimizi majukumu yao....!

Ni bora twende hivi tunaenda, ndo maana natamani Makonda angekua hata PM kwa faida ya Masikini.
 
Wewe naona uko gizani afadhali ungekaa kimya usijibu. Umelichukulia hili jambo kwa wepesi sana, kutekeleza ilani ya CCM? Ina maana ilani ya CCM imeanza kutekelezwa Makonda alipoteuliwa kuwa katibu mwenezi? Kama ndio hivyo basi Chadema wanasema ukweli, kwamba CCM mpo mpo tu hamjui mnalolifanya wala kusimamia.

Halafu wewe, sio kila anaeuliza jambo kuhusu CCM basi yeye ni Chadema.
CCM na viongozi wa CCM hawafanya kazi kwa mazoea. Acha kufanya vitu na kukalili vitu .badilika. CCM ipo hapo ilipo kwa sababu ni chama ambacho hakiendeshwi kwa mazoea unayoyataka wewe na kukalili.

CCM haitabiliki jambo moja ambalo CCM Unaweza ukakalili ni kuwa CCM Ni mtetezi wa mtanzania wakati wote.CCM ndio Sauti ya watanzania na muda wote imekuwa mstari wa mbele kumsemea mtanzania.
 
Niite jina lolote, lakini mimi ni mojawapo ya watu ambao huwezi hata kabisa kunishawishi kwamba hii nguvu na mbwembwe ambazo Makonda amekuwa akizionyesha zinatokana na kuwa kwake na cheo cha katibu mwenezi wa CCM. Tusidanganyane hapa.

Makonda sio katibu mwenezi wa kwanza CCM, na wamekuwapo wengine huko nyuma, lakini ni mara ya kwanza tunapata katibu mwenezi wa CCM ambae anaonyesha kujiamini kupita mamlaka yanayostahili ya katibu mwenezi wa CCM.

Leo hii katibu mwenezi awapigie simu mawaziri, amkebehi mwanasheria mkuu wa serikali, awaamrishe wakuu wa mikoa, ma-RPC, eti kwa sababu yeye ndie msemaji mkuu wa chama, hilo tu? Haiwezekani.

Leo hii katibu mwenyezi apewe bajeti, misafara ya magari, kuliko inavyokuwa kwa makamu mwenyekiti wa CCM au katibu mkuu wa CCM, kwa sababu gani? Kwamba katiba ya CCM imebadilishwa kisiri na hawa wote wameambiwa kuanzia sasa bosi wenu ni katibu mwenezi wa CCM? Pamoja na mawaziri? Wakuu wa mikoa? Mwanasheria Mkuu? Wenyeviti wa CCM wa mikoa?

Sote tunajua msemaji mkuu wa chama chochote anasema yale chama kilichoamua katika vikao vyake rasmi. Kuwa msemaji wa chama haina maana wewe ndio unakuwa unakisemea chama, hata siku moja. Kuwa katibu mwenyezi sio katika mpangilio wa vyeo vya chama, ni nafasi tu. Huwezi hata kusema katibu mwenezi wa CCM ni mkubwa kuliko mwenyekiti wa CCM wa mkoa. Lakini sio hivyo kwa Makonda. Yeye amejipa madaraka ambayo nadhani yanazidi hata ya kuwa makamu mwenyekiti wa CCM, au katibu mkuu wa CCM. Kujiamini huko kunatoka wapi? Mamlaka haya yanatoka wapi? Kwamba siku zote hatukujua kuwa katibu mwenezi wa chama ni mtu mkubwa namna hii? Ni kweli?

Nyie watu wa CCM, nyie mawaziri, nyie wakuu wa mikoa, tuambieni ukweli. Kinachowafanya muufyate Makonda akiunguruma ni nini hasa, Ukatibu mwenezi wa CCM? Na kwa nini sasa wenye akili tukiwauliza mbona mambo yako hivi, mnaishia kutabasamu tu bila kusema lolote? Kuna kitu gani msichotuambia?

Na niwaambie wazi nyie watu wa CCM. Kama nguvu ya Makonda sio ya kikatiba ndani ya CCM, kama kuna chanzo kingine kisicho rasmi kinampa nguvu na kujiamini kiasi hiki, basi anguko la CCM liko karibu sana!
Sasa kuna nguvu gani zaidi ya aliyemteua? Mbona amekuwa akimtaja kila mara?
 
Kuna kapicha flani hivi, kila nikikakumbuka nafunga mdomo.
 
Labda walikaa kikao wakaambiwa je nani atakeenda kuwakosoa wote wasiofanya kazi walizopewa na badala yake wamelala tu au hakuna la maana wanalofanya?
Wakaona asie na haya ni huyo
Au kaambiwa wewe unafaa kuwa na cheo kikubwa serikalini ambapo wengine kimewashinda hebu tuonyeshe kidogo sarakasi zako
 
Back
Top Bottom