Nani kuwa Katibu Mkuu Mpya wa CCM?

habari zako za kiitelijensia ni feki...JK kama anampenda sitta alikuwa wapi kumuacha akapigwa chini uspika...hivi nyie mnafikiria kweli au mnaandika andika tu

wewe subiri uone mambo yatakavyoenda.
vuta subra ndugu lengo la jk ni kuacha heshima kabla hajangatuka.
 
Mzigo mzito mpe mnyamwezi...hawezi kuunda chama upya maana kimeoza toka matawini...Huku juu ni ulaji tu


Mhhh, nimeipenda hii lakini
Nami nasema "Kimeoza kwanza kwenye mizizi", matawi ni matokeo tu !!
 
source: habari za kiintelijisia
habari kutoka watu wa karibu wa mhe jk zinasema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa aliyekuwa spika wa bunge la 9 kuukwaa ukatibu mkuu wa ccm kutokana na mvuto na imani amani ambayo wananchi wengi wanayo kwake. kutoka chanzo hicho cha habari, kupewa sitta ukatibu mkuu itakuwa pigo kubwa kwa vyama vya upinzani hususani chadema kutokana na kukubalika sana kwa sitta kwa wananchi na wasomi wengi wa nchi hii.

Itakuwa salama ya CCM ya ukweli na siyo ile ya mafisadi hakuna cha CHADEMA wala CCM wazalendo wote wamenia mamoja regardless of their political affiliations. Nakama hili litakuwa itakuwa habari njema kuelekea kwenye democracy ya kweli maana Six bila CHADEMA ni white elephant same as CHADEMA bila wazalendo wa CCM! Mafisadi wamekamatika no way out and I still thank my God the mighty one of Israel kwa ushindi wa raia wa Tanzania.
 
Kumpa Sitta ukatibu mkuu wa CCM maanake JK atakuwa ameamua kuachana moja kwa moja na wakina R.A na Lowassa, jambo hilo siyo rahisi. Kutokana na hulka yake JK hupenda kuuma na kupuliza.

hili kaka halina mjadala kama ni hivyo usemavyo ni kweli basi jk angelizuia lowasa kupukutishwa kutoka uwaziri mkuu.
 
Itakuwa salama ya CCM ya ukweli na siyo ile ya mafisadi hakuna cha CHADEMA wala CCM wazalendo wote wamenia mamoja regardless of their political affiliations. Nakama hili litakuwa itakuwa habari njema kuelekea kwenye democracy ya kweli maana Six bila CHADEMA ni white elephant same as CHADEMA bila wazalendo wa CCM! Mafisadi wamekamatika no way out and I still thank my God the mighty one of Israel kwa ushindi wa raia wa Tanzania.

chadema wanaomba mungu JK asikubali sitta kuwa katibu mkuu kwani huo utakuwa ndio mwisho wa sera yao kubwa.
 
Bora watoto wakusinzia kuliko wasomi wa chuo kikuu ambao wanasomeshwa kwa kodi zetu kufundishwa kuzomea na Dr Slaa nao wanakubali! Useless!
Nilikuwa natafuta jina linalokufaa kulingana na hoja zako wewe umenisaidia, USELESS
 
chadema wanaomba mungu JK asikubali sitta kuwa katibu mkuu kwani huo utakuwa ndio mwisho wa sera yao kubwa.

Kwahiyo sera yao itatekelezwa na Six siyo ama? Hivi angewaambia anaenda upinzani kama hana maelewano nao jaribu kuacha ushabiki na kuona ukweli kwa macho ya nje ya box. Six kama individual anaweza asiwe na uhusiano wowote na wapinzani lakini Six kama instituion iliyoamua kusimamia misingi ya kitaifa hawezi kuacha kuwa na wapinzani wanaosimamia misingi ya kitaifa hayo ni maoni yangu tu naweza kuwa optimistic. We unafikiri yeye JK haogopi Six kuwa katibu mkuu ama? Angalia hapo some body is in a very big dillema.
 
No wonder waliahirisha bunge Ijumaa kumbe matumbo yalikuwa yanaharisha. But, Seriously, JK atapata nani msafi na mwenye akili timamu ambaye ni mwanachama wa ccm kwa sasa anayeweza kuwa katibu mkuu wa ccm?

Kama mafisadi wataendelea kubaki ndani ya ccm ni nani ndani ya ccm anaweza kuwadhibiti?

Katibu mkuu mpya gani anaweza kufanya kazi na timu ya mawaziri wa sasa ambao wengi ni mafisadi? Je, alitakiwa pia avunje baraza la mawaziri?

Amefanya uamuzi mzuri kuvunja Secretariat, lakini hata wapambanaji ndani ya ccm ni mafisadi, ni viwango tu

Ni bora tu angevunja chama chenyewe kuliko kufanya cosmetic surgury ambayo itakuja kuumuka kama pua ya marehemu Michael Jackson.

Update:
Hii thread hadi sasa imepata zaidi ya post 70 lakini hajapatikana mwana ccm mwadilifu, asiye fisadi, mwenye elimu, mchapakazi.

Kama JK angekuwa anategemea kupata ushauri hapa basi labda atafute wajumbe nje ya ccm au hata nje ya nchi

Amrudishe Mangula
 
habari za kuaminika toka ndani ya chadema sinasema kwamba chama hicho kinapanga kufanya uchaguzi mkuu wake mwaka 2013. Kwa mujibu wa katiba wa chama hicho mbowe na dr slaa watakuwa wamefikia kikomo cha muda wa kugombea nafasi wanazoshikilia sasa.

Ni wazi kwamba mbowe hawezi kushuka chini kwa kuwa ameshashikilia nafasi ya juu zaidi ya uenyekiti. Dr slaa ana nafasi ya kupanda kwa kuwa alishuka toka umakamu na kuwa katibu mkuu hivyo ana nafasi ya kupanda kuwa mwenyekiti.

Vyanzo vya habari vinasema dr slaa amekubali kwa shingo upande kuwa mwenyekiti kwa kuwa dhamira yake ilikuwa ni kuachana na utumishi wa chama kuwapisha vijana.

Hata hivyo ametoa sharti kwa chama hicho kumteua kijana bora wa kufanya naye kazi kama katibu mkuu wa chama.

Swali, ni nani anafaa kuwa katibu mkuu wa chama hicho kikuu cha upinzani?

......ndiyohiyo

atakua makamba, si hana ajira au?
 
....................ni heri kuwa mjumbe wa shina la CCM kuliko kuwa katibu wa CCM Taifa kushika nafasi iliyoachwa wazi na mwl. wa grade A....ama kweli ukatibu mkuu kama injini ya chama imerahisishwa....hata mwanafunzi wa darasa la saba anazosifa za kuwa Katibu wa CCM Taifa kama katibu aliyeenguliwa alipata kushika wadhifa huo nyeti..
 
".....Taarifa kutoka ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu jana usiku mjini hapa zilidai kuwa Wilson Mkama ndiye aliyepewa jukumu la Ukatibu Mkuu wa CCM huku msaidizi wake kwa upande wa Bara akitajwa kuwa ni Abdulrahman Kinana, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa Fedha na Uchumi, Zakia Meghji na Katibu wa Oganaizesheni, Dk Rehema Nchimbi.! source : Mkama, Kinana watajwa kubeba jahazi la CCM
 
Back
Top Bottom