HIVI KUNA nchi nyingine yenye ritual/practice kama hii?

As far as I know ni sisi tu. Kama wapo labda wanaweza kutusaidia kuboresha ya kwetu haha. All jokes aside jamani do we still need this? Does it still hold the same purpose and goal they initially had for it? I think all this is Tanzanians holding on to the past simply because the founders started it. Kama ina maana fine kama at this day & age it does nothing for patriotism or anything like that then maybe its time to let go. Au wanaogopa waasisi wata fufuka na kulalama?
 
Mwenge nao ni ufisadi wa aina yake kwani imeshindwa kumuulika Mapapa sasa sijui kama inaweza kuona nyangumi mkubwa .Haina maana hata kidogo kwani ni upotezaji wa mda na kuaribu bajeti kwani watawala wanapeana vitengo. Bora waiweke kwenye kumbukumbu za Uhuru.
 
Mwenge hauna maana yoyote, ndio kwanza unazidisha gonjwa la ukimwi na anasa kwa watu, maana watu utakuta usiku kucha wanakesha eti mwenge ! Watu wazima serikalini kuhimiza watu kutoa michango kwa ajili ya mwenge ambao hauleti faida yoyote kwa jamii ya Kitanzania.
Ingekuwa bora zifanyike kampeni za kuchangia watu wasio na uwezo ambao hawajui mlo wao kwa siku itakuwa vipi au kusaidia skul zao hizo za serikali ambazo hazina hata desk na viti kwa ajili ya watoto kukaa.
Nilisitika sana nilipotembelea shule hizi za kata na kukuta watoto wanakaa chini. Huku serikali inafuja pesa kwenye mambo kama haya ya mwenge ambayo hayana hata umuhimu kwa Taifa.
 
SISI TUNATAKA KUWASHA MWENGE ..Mlima Kilimanjaro
Umulike nje ya mipaka yetu...ulete tumaini
pale ambapo hakuna matumani, upendo mahali ambapo pana chuki na heshima ambapo pamejaa dharau

Huo wimbo ulikuwa unaelezea madhumini ya kuwasha na kukimbiza mwenge!
Je kwa miaka yote zaidi ya 40, mwenge umekamilisha nini kati ya hivyo?
Maadam hayo ndio yalikuwa madhumuni ya kuwasha na kukimbiza mwenge nadhani yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwani hadi leo hii tunaishi KiMungu Mungu tu..yaani pale pasipo na matumaini tunapita, misaada inamwagwa...
Upendo pale penye chuki..heshima penye dharau kwani mnaona Mafisadi wote tunakula nao sahani...hakuna chuki bali heshima na upendo..

Tatizo sio mwenge isipokuwa sisi ndio tumepoteza mwelekeo na UHURU kwetu hauna maana tena..Na nafikiri ukimuuliza mtoto wa shule ya sekondari leo hii nini maana ya UHURU utapata majibu mia kidogo kwani maana halisi imekwisha potea..Hakuna tofauti kati ya kutawaliwa au kuwa huru maadam wananchi bado wako mikononi mwa watawala watunzi wa sheria..

Madhumuni ya mwenge wetu ni sawa na mwenge wa Olyimpic ambao mbali na kuashiria kuanza kwa michezo hiyo hutangaza matumaini, upendo, heshima na zamani ilikuwa mwisho wake kama sijakosea zamani mwenge ulikuwa ukihitimishwa na sikukuu ya Wakulima tukiita Sabasaba..Ilikuwa siku kubwa sana Tanzania nzima toka vijijini, wilayani hadi mikoani, pengine ikisherehekewa kuliko hata siku ya Uhuru wenyewe..

Hapo wakulima huonyesha mavuno yao na mashindano mengi ikiwa ni pamoja ngoma za kienyeji, costumes, ukubwa na uzito wa mazao, maonyesho ya mbegu mpya na kadhalika.. maadam siku hiyo ilikuwa furaha tupu kwa wananchi wote Tanzania utafikiri kweli Olympic ya Watanzania..Ni vigumu sana kumwelezea mtu ambaye hakuwepo miaka hiyo ya 60 na 70 kwani haya yote hayapo tena leo...
Tuliobadilika ni sisi sio mwenge na lawama zetu haziwezi kuwa na msingi wowote kwa sababu ya mwenge unaowashwa kwa mafuta ya taa kuwa sababu ya kupoteza fedha..
 
safi sana response hii, the point ya mwenge ilikuwa kumulike nchi in terms of kuwakumbusha watu wawe na Uhuru na kuwa na maisha ya kujitegemea...ni wananchi ambao wameshindwa kujikomboa, Mwalimu aliwaonya huyu msanii hafai lakini hamkusikia...na mkamchagua by 80% halafu leo mna-blame a symbol
 
mm naona swali la mwanzo la mtoa mada ni muhimu, mfano tazama waingereza wakati wanajua kuwa ufalme umekuwapo kati yao kwa karne na karne, walifika wakajiuliza kama kuna haja ya kuendelea kuwepo kwake. Hapa tunaulizana kuna umuhimu wa kuendelea kuwepo mwenge wa uhuru?
 
Julius,
Mkuu swali lako zuri sana na ndicho tumejiuliza sote kabla ya kutoa michango yetu.. Binafsi hilo swala la Uingereza na Malkia ni utamaduni wao, watajiuliza wao kwa kutazama faida za Usultan kwa sababu hadi leo hii mbali na nguvu ya Malkia, Uingereza inapokea fedha (royalties) kibao toka nje kama milki ya huyu Mama..
Swala kubwa kwao sii kuwepo kwa Malkia as a symbol ya utawala wao isipokuwa mfumo zima unaotukuza Usultan..
Tofauti na sisi tunahoji sana Mwenge wakati sisi wenyewe hatutekelezi yale yanayotokana na kuwepo kwa mwenge huo.. Yes naweza kusema hatuna haja ya kuwa na Mwenge wa Uhuru kwa sababu sisi wenyewe tumevua imani na itikadi zinazoambatana..
Ni sawa na Mkristu anayetaka kuvua mkufu wa msalaba kwa sababu haoni faida yake, lakini anashindwa kukubali kwamba imani yake ktk dini imepungua kutokana na kutohudhuria kanisani wala kufanya ibada zinazomtaka awe mkristu wa kweli..Avue msalaba asivue haiwezi kusaidia kitu maadam kinachopimwa ni imani yake..
 
Jamani me napenda kutoa dukuduku langu kuwa hivi kutembeza mwenge nchi nzima kuna umuhimu kweli kwa sasa? Hatuna zahanati za kutosha, Madarasa ya shule hayana viti wala vifaa vya kishule. Lengo la mwenge ilikuwa kujikumbusha UHURU WETU na kujenga umoja na mshikamano, Lakini ukiangalia tuna tarehe ya UHURU inatosha pia kama nikufikisha ujumbe kwa wananchi tunaweza kutumia TV, Magazeti na ziara za viongozi!!

Hili mnalionaje wana ThinkTanker!!
 
Mi mwenyewe sielewi maana yake, hasa kwa sasa hivi...Hapa Arusha two weeks ago mwenge ulilala mahali fulani panaitwa Mbauda, pana Ofisi ya sisiemu...Asubuhi yake wafagizi waliokota kondom ndoo moja...sasa sijui "do kavukavu ni wangapi!Mwenge unasambaza ukimwi zaidi kuliko ujumbe... ihate so much that misuse of kerosene and vehicles, especially these days, bora hata enzi za mwalimu watu walikuwa serious kidogo... puuuh!
 
Jamani me napenda kutoa dukuduku langu kuwa hivi kutembeza mwenge nchi nzima kuna umuhimu kweli kwa sasa? Hatuna zahanati za kutosha, Madarasa ya shule hayana viti wala vifaa vya kishule. Lengo la mwenge ilikuwa kujikumbusha UHURU WETU na kujenga umoja na mshikamano, Lakini ukiangalia tuna tarehe ya UHURU inatosha pia kama nikufikisha ujumbe kwa wananchi tunaweza kutumia TV, Magazeti na ziara za viongozi!!

Hili mnalionaje wana ThinkTanker!!

Mwenge hauna maana yoyote, basi kwa sababu watu wanatafuta kazi ya kufanya na night allowance inabidi wa uweke.Nina imani hata viongozi hawaoni maana yake kwa sasa hivi ila nani atamfunga paka kengere?
Kiongozi gani atasema kuwa mwenge sasa basi.Mimi nitawasaidia watafute nafasi pale mnazi mmoja wautundike pale mtu akitaka kuoona aende pale kwa mda wake, au wauweke jumba la makumbuusho haina haja yoyote kwa sasa kukimbiza mwenge.Nikupoteza muda.
 
Zamani mwenge ulihimiza watanzania Kushiriki maendeleo ya wanainchi na kuchangia maendeleo yao, leo Mwenge unatapanya ukimwi na kama ni michango wana CCM hawategemei mwenge bali ni mafisadi wanawajaza pesa
 
Nilipokuwa shule ya msingi,tulikuwa tunaacha masomo na kwenda kuupokea mwenge wa uhuru.
I feel hii ilikuwa brainwashing ya kutupwa.
Kama wewe ulishiriki kukimbiza huu mwenge ,tuambie faida zake!
 
Nilipokuwa shule ya msingi,tulikuwa tunaacha masomo na kwenda kuupokea mwenge wa uhuru.
I feel hii ilikuwa brainwashing ya kutupwa.
Kama wewe ulishiriki kukimbiza huu mwenge ,tuambie faida zake!

Posho kwa wakubwa, maambukizo ya ukimwi, kulazimishana michango na mambo mengine wenzagu wataengeza.
 
Nilipokuwa shule ya msingi,tulikuwa tunaacha masomo na kwenda kuupokea mwenge wa uhuru.
I feel hii ilikuwa brainwashing ya kutupwa.
Kama wewe ulishiriki kukimbiza huu mwenge ,tuambie faida zake!

Mwenge wa uhuru na aida kubwa sana, angalia ujumbe wake:
Ssisi tumekwishauwasha mwenge na kuuweka Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pasipo na atumaini, upendo mahali palipo na chuki,
na
Heshima palipojaa dharau!!!!!!!!!!!!!!

Hakika ni mwenge wa uhuru ndio mkombozi kwa mtanzania. Wote wanaopiga kelele leo juu ya ufisadi, wanateteta maudhui ya ujumbe wa mwenge wa uhuru. Na naamini kuwa kama ccm itaangushwa siku moja madarakani, basi itaangushwa na mwenge wa uhuru.

Tatizo la watanzania wanakimbiza mwenge kama kibatari na wanasahau kuwa mwenge ni ujumbe! Tena sikuhizi wameupa mwenge jumbe nyingine zaidi ya ujumbe wake wa asili wakati hata ujumbe wake bado kueleweka vyema.

Nilitegemea kuwa mwenge wa uhuru ungeimarishwa hata nje ya mipaka yetu hasa kwenye nchi zenye migogoro ili kupeleka uko mwanga , matumaini na heshima angalau kwa kuanza na nchi za jumuia ya afrika mashariki, lakini wameutelekeza jeshini na kugeuza kilelel chake kuwa kumbukumbu ya mwl nyerere hivyo kila ujumbe katika sku ya killele hmhusu mwal nyerere! Makosa makubwa kabisa ya kiufundi!

Mwenge wa uhuru ni chombo cha kisiasa hivyo kukipeleka jesjhini ambako hakuruhusiwi siasa ni kosa kubwa sana la kiufundi linalotugharimu hai wa siasa zetu, siku za usoni natarajia kulipigia sana kelele suala hili

Mungu ibarki Tanzania.
 
Kuna mwaka fulani katika mkoa mmoja wa Pwani,baada ya mkesha wa mwenge asubuhi ziliokotwa ndoo mbili zimejaa kondomu zilizotumika, wanaume walikesha haswa!
 
Kuna mwaka fulani katika mkoa mmoja wa Pwani,baada ya mkesha wa mwenge asubuhi ziliokotwa ndoo mbili zimejaa kondomu zilizotumika, wanaume walikesha haswa!

ndio makosa ya kuukabidhi mwenge jeshini! ulitakiwa uachiwe wanasiasa waukimbize
 
Wanakijiji wa wawili wa Kijiji cha Masqaroda Wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara wamekamatwa kwa kuhoji matumizi ya michango ya fedha za mwenge.
Mwenge mwaka huu utawashwa Mkoani Manyara

______________________________________
Democracy is the government of the people, by the people, for the people

Abraham Lincoln
 
Back
Top Bottom