Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,399
Mimi sioni haja ya kuendelea kuwa na hizi mbio za Mwenge.
Hauna faida yoyote zaidi ya kueneza ujinga kwamba nchi ina amani na utulivu, huku watu wanaibiwa kodi na misaada ambavo vinaliwa au kutumiwa vibaya.
Penye mahali popote penye amani na utulivu panatakiwa pawe pameneemeka kiuchumi, kisiasa na kijamii na watu wote wana furaha, ukakika wa milo mitatu kwa siku, elimu, afya.
Mwenge kwa sasa naufananisha na mdundiko, na mkole mambo ambayo yanaleta ushawishi wa ngono, ulevi na watu kuwa wajinga zaidi.
Kuwe kampeni ingine kabisa mbadala ya kuhamasisha wananchi wawe wanawaza maendeleo bila kuwepo vizuizi visivo lazima, urasimu na UFISADI ambao ni watu wachache ndio wanafaidi Tanzania ya leo.
Ni juzijuzi tu ndio tunasikia eti hospitali ya Muhimbili ndio kwa mara ya kwanza yangu uhuru ndio imefanya upasuaji wa moyo! Hii ni aibu.
Mwenge ukiishakimbizwa mwaka huu iwe ni mara ya mwisho na uwekwe jumba la makumbusho, kwani una miaka 47 sasa na umeshikwashikwa sana, inatosha jamani!