El Roi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 263
- 502
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, sherehe nyingi za kitaifa za nchi hii, zilianza kusherehekewa kwa mtindo wa kubana matumizi katika awamu ya Tano ya utawala wa nchi yetu.
Ni muda Sasa sherehe hizi zinasherehekewa kwa namna nyingine na siyo tulivyokuwa tumezoea, Gwaride la kitaifa na mambo mengi kedekede ikiwemo mialiko ya wakuu wa nchi nyingine, ukiachia mbali gharama kubwa za uandaaji wa hizo sherehe.
Mantiki ya kubadilisha namna tulivyokuwa tunafanya ilikuwa kulinda upotevu wa fedha nyingi zilizokuwa zinaenda kwenye shughuli ya siku Moja, badala yake walitaka kuwekeza pesa hizo katika mambo ya msingi zaidi yanayodumu.
Binafsi napendezwa kabisa na mfumo wa Sasa wa sherehe hizi. Umeokoa pesa nyingi na unatufanya kama wananchi kuwa wepesi.
Kinachonishangaza Sasa, ambacho nadhani nakosa majibu, kwa nini mbio za mwenge wa uhuru zimeachwa kuendelea?
Kwanza, kubadilisha namna ya kusherekea uhuru wenyewe na kuacha by product yake kuendelea kuadhimishwa, ni kutotenda haki kwa huo uhuru wenyewe.
Unamwadhimisha mtoto, kwa gharama ya kumdharau mama aliyemzaa. Hii haikai sawa.
Lakini kama mantiki ni gharama, kwa Nini tunaharibu pesa ambayo ingeingizwa kwenye mambo muhimu, kukimbia na mwenge ambao mama yake, hatumwadhimishi tena inavyofaa?
Mwenge unatumia gharama na pesa nyingi sana kukimbizwa nchi hii, achilia gharama nyingine za uharibifu wa kimaadili na kijamii, zinazosababishwa na mbio hizi.
Wakati tunatunza uchumi na kuelekeza pesa katika mambo muhimu kwa kuepuka sherehe kubwa za uhuru, mwenge uharibu uchumi wa watu na hasa wafanyakazi wa serikali, kada ya wafanyabiashara, na hata wanafunzi mwenge huu unapokimbizwa.
Wafanyabiashara huombwa michango ya mwenge kwa nguvu, wafanyakazi hukatwa pesa mapema kutoka kwenye mapato ya. na mishahara yao, na wanafunzi huacha masomo Ili kujipanga kuhusherekea huo mwenge.
Maombi yangu, busara iliyotumika kutafuta namna ya kuokoa pesa kwa kuacha kufanya sherehe rasmi za uhuru, itumike pia kuacha kukimbiza mwenge Tena Kila mwaka, ambayo kimsingi hutumia mapesa mengi achilia mbali maana hasa kwa Nini unakimbizwa.
Kama ni lazima sana mwenge huu kukimbizwa, basi serikali ingeona utaratibu mwingine usiogharimu nchi kiasi hiki.
Vinginevyo, kama serikali namna ya kuacha ukimbizaji wa mwenge kwa mtindo huu wa Kila mwaka, basi walau wakimbize huu mwenge mara Moja Kila baada ya miaka mitano.
Utakuwa umeokoa mafedha ya kutosha kwa miaka minne, na maadili na shughuli nyingine za kijamii zitasitawi walau hiyo miaka minne ya ukimya wa kutokuwa na mbio hizo!
Kuna watu wanashauri, mwenge uwe unawashwa na kupelekwa mlima Kilimanjaro Moja kwa Moja, kama slogan yake ilivyo, " sisi tunauwasha mwenge na kuweka juu ya mlima Ili uwaangazie nchi".
Nashauri busara iliyotumika kubadilisha namna ya kuadhimishwa kwa siku ya uhuru na sherehe nyinginezo za kitaifa, itumike Tena kuacha hizi mbio za mwenge ambazo ukweli ni costly, kiuchumi, kijamii na hasa kimaadili.
Tukishindwa Hilo, tusilalamike watu wakituita wachawi tunaokimbiza moto Ili kutambika nchi kwa Miungu tusiowajua.