Mwenge ni zilipendwa na wala hauna majibu ya changamoto tulizonazo hivi sasa. Ni vyema ukafutwa na fedha hizo zinazoteketezwa katika kuutembeza zipelekwe kwenye shughuli za maendeleo.

Hawa CCM hawatakaa hata siku moja kuliona jambo hili bali uongozi mpya wa Chadema chini ya Dr. Slaa ndiyo utafumbua hili fumbo la kijinga ambalo mwerevu ni lazima ataling'amua
 
Naomba kufaham jamani huu mwenge tunao uzungusha kila mwaka toka unaanza siku ya kwanza hadi kuzimwa una gharimu kiasi gani cha pesa???????
 
kama hatutaki kuuzima kwa kumuenzi Nyerere inabidi tuupe ratiba mpya, kila baada ya miaka mitano.
pesa ni nyingi harafu wanasema hawana pesa za kuwarudisha wanafunzi vyuoni.
 
sijui ni kiasi gani ila naimani kwa gharama inayo tumiwa tungeweza kujenga library moja kila mkoa kila mwaka wanao zunguka

Hivi wamesha wahi kujiuliza MWENGE UNACHANGIA KIASI GANI MAAMBUKIZI YA UKIMWI KWENYE MIKESHA YAKE?????
 
kumbe watz mmeanza kushtuka sasa! Safi sana...na mtaona mengine mengi sana! Tunataka serikali ya uwazi sasa!
 
Heshima kwenu wana JF.
Kuna jambo ambalo limekuwa likinisumba sana bila kupata jibu lake, kwa hiyo naombeni msaada.
Jambo lenyewe ni "Mwenge wa uhuru" kila mwaka kunakuwepo na michango kwa ajili ya mbio za mwenge, na mambo ambayo yanafanyika kipindi hiki cha mbio za mwenge ni kuzindua na kuweka mawe ya misingi kwenye miradi mbalimbali kama mashule na zahanati.
Nimekuwa najiuliza Gharama zote za kukimbiza huu mwenge ni zanini wakati miradi hiyo ingeweza kuzinduliwa na watu wengine tena kwa gharama ndogo tu.
Zamani tuliambiwa kazi ya mwenge ni kumulika wanyonyaji na wahujumu uchumi pia kulteta matumaini mapya kwa wananchi, lakini kwa sasa haya hayapo kwani Wanyonyaji - MAFISADI - ndo wameshaka hatamu, na yote wayatakayo ndiyo yanayotimizwa.


NAWAKILISHA
 
Michango ya Mwenge yazua manung`uniko Mbeya




Na Thobias Mwanakatwe



17th May 2011


email.png

B-pepe



printer.png

Chapa



comment_bubble.png

Maoni








Mwakipesile%20RC(9).jpg

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile



Mwenge wa Uhuru umezua kizaa zaa mkoani hapa baada ya serikali kutangaza kusitisha sherehe za kuuwasha mkoani hapa kama ilivyokuwa tangu mwaka jana ambapo watumishi wa serikali na wananchi wametaka warejeshewe fedha zao zaidi ya Sh.milioni 100 walizokuwa wamechangishwa kwa ajili ya kazi hizo.
Wakizungumza na NIPASHE jana kwa nyakati tofauti mjini hapa, walisema hawakubaliani na tamko la Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile kwamba fedha zilizokusanywa kwa ajili ya kazi hiyo zitawekwa benki ambapo zitatumika mwakani wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile juzi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake alisema Mwenge wa Uhuru hautawashwa tena mkoani hapa na badala yake utakwenda kuwashwa kijijini Butiama mkoani Mara kwa ajili ya kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Mwakipesile alisema hatua ya kuuwasha Mwenge huo kijijini Butiama inatokana na kwamba huu ni mwaka wa 50 tangu nchi ipate uhuru hivyo viongozi wa kitaifa wamekaa na kukubaliana kuwa ukawashwe kijijini kwa Baba wa Taifa ikiwa ni ishara ya kumuenzi.
Hata hivyo, watumishi wa serikali ambao waliomba majina yao yasitajwe walisema kwa kuwa Mwenge wa Uhuru hautawashwa tena Mbeya, serikali ya Mkoa wa Mbeya itumie busara kuwarejeshea fedha zao kwasaabu hawana imani kama kweli zitakuwa na usalama zikiwa chini ya viongozi waliopewa jukumu ya kuzikusanya.
“Tunachotaka turejeshewe fedha zetu hiyo hadhithi ya kwamba tutaziweka benki hatukubaliani nayo, hivi sasa serikalini ufisadi umetawala kila kona kwa hiyo tuna uhakika hata fedha zetu tulizochangishwa zitachakachuliwa,”alisema mfanyakazi mmoja kutoka Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambaye aliomba jina lake lisitajwe.



CHANZO: NIPASHE


0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni
 
Hizo ndizo pesa zisizo na oditor kila mtu anakula tu.

Mie nilijua baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza basi suala la mwenge limepigwa teke na kuratibiwa na Serikali tu.

Poleni sana
 
nini hekima na busara ya kuwa na mbio za mwenge,mtanzania wa leo anafaidika vipi na hizi mbio za mwenge, duu kazi tunayo , kumbe mwenge bado unaendelea....
 
Nini 'umuhimu wake?



Mshauri wa Mawasiliano wa Benki ya NBC, Bi. Robi Matiko-Simba (wa pili
kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shs milioni tano kwa Mkuu wa
Wilaya ya Mbeya, Bw. Evans Balama ikiwa ni sehemu ya mchango wa benki
hiyo kwa ajili ya mbio za Mwenge wa Uhuru katika makabidhiano
yaliyofanyika Mbeya hivi karibuni. Wengine pichani kushoto ni Meneja
wa NBC Kanda ya Nyanda za Juu, Bw. Ramadhani Lesso, Meneja wa benki
hiyoTawi la Mbeya, Bw. Salema Kileo (wa pili kulia) na Bw. Lazaro
Mwankenja, mmoja wa waratibu wa mbio hizo.
 
Ni utumiaji mbovu wa pesa, Hiyo pesa wangechangia elimu,afya au maendeleo mengine ya kijamii na sio kuchoma mafuta kuzunguka na magari. 2015 mwenge utapelekwa makumbusho
 
wafanyakazi wamekatiwa overtimes na wanatumikishwa kama punda kisa project 66 shame on you Mafuru
 
Nini umuhimu wa Mwenge wa uhuru?
Orodhesha faida tunazopata kwa kukimbiza "mwenge wa uhuru" nchi nzima (faida hizo lazima ziwe zile ambazo kama tusingekuwa na mwenge, zisingeweza kupatikana kwa mfano kufungua majengo ni faida lakini tunao viongozi rundo wanaoweza kufungua majengo bila kuongeza gharama kwa vile ni sehemu ya majukumu yao) pia kama una takwimu za gharama, tuwekee hapa ili tujue gharama kama inalingana na faida tunazopata.
 
faida za mbio za mwenge hzi hapa
1.inaongeza matumizi ya cndm
2.inaongeza ajira
3.unaongeza kipato
4. per diem za viongozi wa mwenge ndo csemi
5.wanadai unamlika hata nje ya mipaka ya tz
6. unaongeza air pollution, lakini wachoma mkaa wanaambiwa wanaharibu mazingira
 
Mwenge ni ishara ya mshikamano wa udugu wa kitaifa wacha watu wepete tu kama wewe huoni faidayake basi poa

mmmmhhhh! ishara ya mshikamano wa udugu wa kitaifa mi naona ni 'limbi la umaskini wetu unaotuzunguka'. gharama za mbio za mwenge
wangejenga walau kilomita kadhaa za lami kila mwaka, tusingekuwa na shida za usafiri hapa nchini
 
Back
Top Bottom