Mwanamke najiamini kwa avatar ya ukweli

Status
Not open for further replies.
Umeona husifiwa sio kwa sura wala jina ukaona isiwe taabu, ngoja nijisifu mwenyewe, lol, kisiketi ulichovaa kimekupendeza
 
Kwahiyo wanawake tu ndiyo wasioona huo UREMBO wangu? Mbona wanaume wote WANANISIFIA? Hapa kuna tatizo.
wasifie nini cheki vimikono kama fito? wallah mpenzi wako ana shida hana hata sehemu ya kushika,umekauka kau ukipita karibu na moto si unaanza kuwaka inabidi uwe unatembea na kaportable fire extinguisher kwa usalama wako
 
Halafu eti wanawake tunalilia haki sawa na wanaume. Haki sawa itatoka wapi kama sisi wenyewe hatupendani? Mtu kama ni mzuri basi nipeni haki yangu.

Sasa wewe mpendwa, kama ni mzuri ni poa sana.Sisi wanawake wenzako tukusifie au tukupende ili iweje?Sisi pia wazuri tena kukuzidi sasa unataka tuseme nini ilhali tumekuzidi viwango vyote? Post zilizo makini, urembo,ulimbwende,utanashati, uzuri wa sura, umbo na tabia...all round.
Ulishaona mwanaume kaanzisha thread ya kipuuzi kama yako humu na wanaume wenziwe wakamsifia?
Tukikusifia mwisho utasema tushakuwa wasagaji.

Wewe endelea kujipigia promo, upate PM nyingi zaidi maana nimepitia baadhi ya posts zako nikaona unashabikia sana PM.Wenzio tuko kupata na kutoa habari na maarifa zaidi.
Good luck mamii!
 
wasifie nini cheki vimikono kama fito? wallah mpenzi wako ana shida hana hata sehemu ya kushika,umekauka kau ukipita karibu na moto si unaanza kuwaka inabidi uwe unatembea na kaportable fire extinguisher kwa usalama wako

Unajiongelea jinsi ulivyo au unaiongelea sura yangu? Sijakuelewa kabisa.
 
Kuna mtu amesema u are arrogant, I agree. Kama ulitaka kuwajulisha watu kuwa kwenye avatar that is the real Radhia its ok, ila huko kwenye sifa ungewaachia wenyewe wa'judge kama mzuri au la! Ni Hayo Tu

Kama unajiamini haukatazwi
 
wasifie nini cheki vimikono kama fito? wallah mpenzi wako ana shida hana hata sehemu ya kushika,umekauka kau ukipita karibu na moto si unaanza kuwaka inabidi uwe unatembea na kaportable fire extinguisher kwa usalama wako

Kha! Hii too much sasa, punguzeni munkari.
 
Najua kitawakera sana mashostito lakini kiufupi nimethubutu na nimeweza kutumia picha yangu halisi kama avatar yangu. Si kingine ila ni urembo wangu wa sura ulionifanya nijiweke hadharani kama nilivyo tofauti na vifidodido vinavyojipa majina makubwa lakini sura mbayaaaaa. Mwanamke kujiaminiiiiii.........

Mwe!!! Kwa hiyo wenzio wa humu ndani ni wabovu?
 
Kama unajiamini haukatazwi

Unajua maana ya kujiamini?

Hebu jisome hapa ulivyoandika utumbo:

Najua kitawakera sana mashostito lakini kiufupi nimethubutu na nimeweza kutumia picha yangu halisi kama avatar yangu. Si kingine ila ni urembo wangu wa sura ulionifanya nijiweke hadharani kama nilivyo tofauti na vifidodido vinavyojipa majina makubwa lakini sura mbayaaaaa. Mwanamke kujiaminiiiiii.........

Hao wanawake wenye majina makubwa lakini sura mbaya ndio wanaojiamini.Kujipa jina kubwa ni bora kuliko kuchukua picha ya mtu mwingine google photos ukaanza kuota kuwa wewe ndivyo ulivyo.Au unataka tukuumbue zaidi?

Kujiamini ni pamoja na kuwaacha wengine wakusifie au kukutukuza.
Kutokujiamini ni pamoja na kujinadi na kujitangaza kuwa wewe ni mzuri na kuiba picha ya mtu mwingine kisha ukajifanya ni wewe!
IN SHORT THIS POST IS ABOUT LOW SELF ESTEEM FOR A WOMAN.
Grow up!

Najua kitawakera sana mashostito lakini kiufupi nimethubutu na nimeweza kutumia picha yangu halisi kama avatar yangu. Si kingine ila ni urembo wangu wa sura ulionifanya nijiweke hadharani kama nilivyo tofauti na vifidodido vinavyojipa majina makubwa lakini sura mbayaaaaa. Mwanamke kujiaminiiiiii.........

Wee Radhia weee! Wewe ni mtanzania au? Kuwaita wanawake walio humu JF vifidofido vilivyojipa majina makubwa lakini sura mbayaaaa, ni ukosefu mkubwa wa adabu ya kitanzania. Unawafahamu wanawake wote wa JF kiasi cha kusema hivyo? Ni watani wako? Nina uhakika baadhi ya wanawake hapa Jf kama si mamazako ni dadazako wakubwa saaana tu.Ningekushauri kama mwanaJf mwenzio uombe radhi. Au ndo unalipiza kisasi kama ulivyosema kwenye thread moja?
 
Unajua maana ya kujiamini?
Kujiamini ni pamoja na kuwaacha wengine wakusifie au kukutukuza.
Kutokujiamini ni pamoja na kujinadi na kujitangaza kuwa wewe ni mzuri!
IN SHORT THIS POST IS ABOUT LOW SELF ESTEEM FOR A WOMAN.
Grow up!

huna sura babuuuu.....makelele ya nini
 
wasifie nini cheki vimikono kama fito? wallah mpenzi wako ana shida hana hata sehemu ya kushika,umekauka kau ukipita karibu na moto si unaanza kuwaka inabidi uwe unatembea na kaportable fire extinguisher kwa usalama wako
mamaaaa aisee.....tehe tehe teeh
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom