Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,571
Anapaswa kuomba radhi JF huyu Mwakyembe , nyaraka zimewekwa kwenye uzi maalum
Hapo ktk red najipendekeza kwa nani na kwa kipi?Acha kujipendekeza wewe sijui unamaanisha nini kusema hivyo! JF ni jukwaa huru sio mali ya Chadema.
Nawewe una tatizo la kukariri kwanini usiseme ni cuf, Nccr, udp au chauma?
Nakubaliana na Mwakyembe alichokisema, maana hakuponda kwamba habari zote kwamba si za kweli bali ametoa kama angalizo si kila utajkalolipata JF basi ulichukulie kama ushahidi usio na shaka.
Kuna Memba humu anaitwa Jason bourne ukimuamini huyu habari zake basi ni lazima na wewe utaonekana hamnazo. tuchukulie hili la Mwakyembe kama changamoto watu waache kupost upuuzi na mods muwe faster kuondowa thread zote za kipumbavu ambazo haziendani na hadhi ya JF.
Nimemjibu kutokana alivyonijibu naona imekuuma.
Mimi nafikiri kungekuwa hakuna ubaya kama tu muuliza swali angesema chanzo cha habari hiyo ni jamiiforums, kinyume na hapo si sahihi. Angeweza kusema ni tatizo la kutegemea habari za mitandaoni. Hata hivyo nafikiri jibu sahihi ilikuwa kukubali au kukanusha ikifuatkiwa na maelezo kidogo. Bahati mbaya mawaziri wetu wanaleta mipasho/kejeli hata kwenye mambo nyeti kwa usalama na ustawi wa taifa.Alichosema ni kwamba "...hilo ndio tatizo la kutegemea sana JamiiForums"; binafsi sioni ubaya wa kauli hii kwani mbali ya kupata habari JF au chanzo kingine chochote, ni vizuri to verify na vyanzo vingine kabla haujawa na uhakika na unachokisema.
mh mwakyembe ameikejeli JF wakati akijibu swali la Wenje.
Amesema ukitegemea sana JF unaweza kuwa na hbr ambazo uhakika ni mushikeri
Mkuu Mungi, kauri ya Mwakyembe haikuwa na nia nzuri juu ya JF. Mh. Wenje alinukuu taarifa za hotuba ya kambi rasimi ya upinzani kuuliza swali lake, sasa Mwakyembe alijuaje kuwa hotuba hiyo ilikuwa na taarifa kutoka JF?Mwakyembe hajaikejeli Jf, bali kasema ukweli. Kuna baadhi ya members humu wana tabia ya kutoa taarifa za uwongo
Katika hatua za mwisho za kupitisha bajeti ya Miundombinu, Wenje alisimama na kusema kuwa ana taarifa za kuwepo vikao vya kuipa kampuni fulani bandari(sijaimaki vizuri) ikiwa ni namna ya kulipa deni la ATCL ambalo ni kubwa mno.
Mwakyembe amejibu kuwa kama kuna mtu anafanya hiyo mipango bila kumjuza yeye aendelee.
Lakini katika hali isiyo ya kawaida akamwambia Wenje, kuwa ana wasiwasi na taarifa zake, na akamalizia..."Ndiyo shida ya kutegemea habari za JamiiForums hiyo!
Mwakyembe Anaichkuliaje Jf huyu?
Ni mara ngapi?na ni data zipi ziliwekwa jamii forum ni za uongo??