TBC - Mjadala wa Role of The Media kwenye mapambano ya Corona, Je, Media Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,616
Wanabodi,
Wale wenye access, naombeni muangalie TBC, kuna kipindi live cha majadiliano kikiendeshwa live kutoka Dodoma kikiongozwa Mtangazaji wa TBC Dodoma, Victoria Patrick akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dodoma, Habel Chidawali, ambaye pia ni mwandishi wa habari wa Mwananchi, huku mjadala ukichangiwa na watangazaji wa TBC Dar es Salaam.

Mjadala huu ni very healthy kipindi hiki cha janga la Corona,
Habel Chidawali ametoa changamoto ya msingi sana inayo vikabili vyombo vya habari katika kipindi hiki cha janga la Corona, amesema kuwa ingawa vyombo vya habari vya Tanzania vimekuwa mstari wa mbele kuripoti updates za ugonjwa wa Corona zinazotolewa na serikali, kitu kinachotakiwa zaidi na jamii ya Watanzania sio updates tuu ya wagonjwa wangapi, bali utoaji wa elimu ya kinga dhidi ya maambukizi, kwenye hili la elimu, vyombo vya habari, bado havijatimiza wajibu wake kikamilifu, hivyo jukumu hili linapaswa kushughulikiwa kikamilifu, kumtegemea tuu Mungu bila kujishughulisha kuokoa maisha ya watu wetu, no kumdhihaki Mungu!. Hivyo there is still so much to be done.

Pia Habel Chidawali amezungumzia changamoto ya maambukizi inayowakabili waandishi wa habari katika kipindi hiki cha janga la Corona. Amesema waandishi wa habari ni kama wahudumu wa afya wanaohudumia wagonjwa wa Corona, wenzetu wahudumu wanapewa kinga, kwenye media bado hakuna media inayowapa waandishi wake vifaa vya kujikinga, hivyo waandishi kujikuta wako kwenye hatari ya kuambukizwa, na kueleza hata hiyo ya social distancing ya kukaa umbali wa mita moja, kwa waandishi imeshindikana, ukifika tuu mahali ukijulikana ni mwandishi, watu wanakuzonga kwa karibu, bila media kusaidiwa na waandishi kukingwa, tutafika mahali waandishi wataanza kuchomoka ndipo wahusika watashtuka na wakati huo ukifika, it might be too little too late!.

Chidawali amevisisitiza vyombo vyote vya utangazaji kutumia mic za boom stick kwa waandishi wake, na waandishi wote wanapaswa kuvaa face mask wakati wote wawapo kazini.

My Take.
Kwa vile na mimi ni mwandishi, naomba nichangie kidogo.
  1. Kwanza nimpongeze Mkurugenzi wa TBC Dr. Ayub Rioba kwa mabadiliko chanya ya TBC Aridhio na kuipongeza TBC kwa mjadala huu, pili nimpongeze mtangazaji Victoria Patrick kwa kuongoza vizuri mjadala na kumpongeza Habel Chidawali kwa mchango mzuri.
  2. Pili nivipongeze vyombo vya habari kwa kazi nzuri ya uhabarishaji umma, na utoaji wa elimu ya jinsi ya kujikinga na Corona, na hapa naomba kutoa pongezi za ziada kwa jf, kama chombo cha pekee cha habari kinachoongoza kwa uhabarishaji umma na kutoa elimu ya kinga dhidi ya Corona.
  3. Niipongeze serikali yetu kwanza kwa ku limit watoa habari za update ya Corona, ni watu 5 tuu, Rais, VC, PM, Waziri wa Afya na Msemaji Mkuu wa Serikali, hapa naomba kutoa shukrani za pekee kwa Afisa Habari wa Serikali, Zamaradi Kawawa ndie husambaza zile updates za serikali, sijui kwa kipindi hiki huwa unalala saa ngapi, anaamka saa ngapi na anachoka vipi maana updates ni kila dakika!.
  4. Naomba kumpongeza kwa dhati kabisa, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas kwa kuwa reachable nakushiriki katika vipindi mbalimbali vya uelimishaji umma, pia kwa kunipatia access ya reaching out viongozi wowote wa serikali kutoa elimu kwa umma na alianzia kwa Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndugulile. Ujumbe kwa Dr. Abbas, pamoja na yote serikali yetu inayofanya kwenye janga la Corona kwa kutoa daily updates, hizi updates za kutajiana idadi ni muhimu kwa kanzi data lakini sio muhimu kwa Watanzania. Watanzania wanatakiwa waelimishwe na sio kutajiwa idadi ya maambukizi!. Mpaka sasa hakuna kipindi chochote popote cha uelimishaji umma kuhusu Corona zaidi ya hizo updates.
  5. Naomba kumpongeza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kwa daily update, hadi Corona ikimalizika, huyo Ummy atunukiwe tuu shahada ya udakitari wa pseudo MD, maana atakuwa tayari amehitimu udakitari kamili bado tuu kuingia internship, japo mimi binafsi siungi mkono political leaders kwenye uongozi wa key ministries zinazohitaji technical professionalism, kwangu Waziri wa Afya lazima awe daktari Bingwa!. Kumeweka Waziri layman halafu Naibu Waziri ndio pro, ni kama kumfunga mdomo huyu pro!.
  6. Pamoja na pongezi hizo zote, kwenye reaching out strategies, Tanzania as a nation bado, hakuna muongozo wowote wa kipindi chochote cha public information Programs ya elimu ya kinga dhidi ya Corona kwa umma. Matangazo yapo, lakini tangazo ni tangazo na utoaji elimu ni vitu viwili tofauti.
  7. Kwenye main stream media bado kuna kazi kubwa ya kufanywa katika utoaji elimu, media zinazotoa elimu ya kinga ni kwa media hizo kujitolea na sio obligation. Kwenye janga kama hili, jukumu la utoaji wa elimu ya kinga lisiachiwe kwa media pekee as option kwa kujitolea, bali jambo hili liwe ni obligation kwa Wizara ya Afya, kutoa a specific communication Strategy ya Covid 19 na kutengeneza vipindi vya elimu kwa umma kwa kuwatumia wataalamu wake, kisha vipindi hivyo visambazwe kwenye vyombo vyote vya utangazaji na vituo vyote Redio, TV na Online media vilazimishwe kurusha vipindi hivyo kwa lazima tena virushwe bure!.
  8. Makala elimishi kuhusu kujikinga na Corona, ziandaliwe na kusambazwa magazeti yote na magazeti yote kuamrishwa lazima makala hizo zipewe nafasi front page.
  9. Kwa vile Corona haina kinga wala tiba, dawa, Watanzania waelimishwe hicho kinachofanyika kwenye vituo vya Corona na wanachofanyiwa wagonjwa wa Corona ni kusaidiwa na vifaa maalum na huduma za tiba, ili wenye uwezo wafanye huduma ya kwanza toka majumbani. Na kwa vile sisi Tanzania kwa umasikini wetu, level za maambukizi zikizidi we can't cope, Watanzania sasa wafunzwe tiba mbadala, ukimuona mtu mwenye dalili zaidi ya kumripoti, watu wafunzwe jinsi ya kujitibia kwa tiba mbadala, tutasaidia wengi kulikokutegemea kuwaripoti tuu. Kuripoti, turipoti yes, lakini pia watu wajitibu, tiba mbadala kibao zipo na zinasaidia kupunguza vifo!.
  10. Tutake tusitake ili kuliokoa taifa letu, lazima tufanye uelimishaji umma na reaching out strategies.
  11. Productions houses zote tujitolee bure kutengeza vipindi vya uelimishaji umma kuhusu Corona, waandishi wa habari wakongwe turudi newsroom kujitolea kuandika makala za uendeshaji umma. Wasanii watunge nyimbo za kuelimisha umma, yale magari ya matangazo ya burudani na wakatikaji wa viuno sasa iwe ni kuhusu Corona, kila kitu ni kwa kujitolea.
  12. Hata wale dada zetu watoa huduma hizi na zile kipindi hiki cha Corona, nao pia waelimishwe, wavae mask, denda hakuna na katika kutoa huduma zao, ule mtindo standard style ya kifo cha mende ni style hatarishi, kwa vile huduma zao zinahitajika kama ilivyo kwa chakula, wafunzwe style muafaka ya kutumika kipindi cha Corona ni doggy style, ila nao pia wawe huruma kwa kupunguza bei, au nao pia wanaweza kujitolea kutoa huduma bure kwa baadhi ya wahitaji maana kiukweli kwenye Corona, pesa hakuna ni mwendo wa kujitolea.
  13. Matajiri wa Tanzania, mashirika, makampuni na Taasisi mbalimbali ziisaidie media ya Tanzania kwenye kutimiza hili kwa ku sponsor vipindi vya uelimishaji umma kuhusu janga la Corona.
  14. Kwa upande wangu mimi mwenyewe as an individual Pasco Mayalla, tayari ninafanya kazi ya uelimishaji umma kupitia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kinachorushwa na Star TV kila Jumamosi asubuhi. Ila mimi pia kama kampuni, PRR inaandaa Public Information Programs na kuvisambaza bure.
  15. Ila pia serikali nayo ifikirie kutoa stumulus package ya aina yoyote kusisimua uchumi maana hii bure bure kabisa mwisho wa siku badala ya wengi kufa kwa Corona, watu tutakufa njaa.
Paskali
Rejea
Rejea za Mandiko ya The Same Mwandishi Kuhusu Janga la Corona

  1. Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani? - JamiiForums
  2. Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa - JamiiForums
  3. Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best! - JamiiForums
  4. RC Makonda, Dar ni jiji la wote, vyama vyote. Mbowe sio mwanasiasa uchwara aliyefilisika, Zitto sio mshirikina. Tunakupenda, heshimu wote uheshimiwe - JamiiForums
  5. Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out! - JamiiForums
  6. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, azungumzia wajibu wa vyombo vya habari kuripoti janga la Corona - JamiiForums
  7. Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani!. Je Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika - JamiiForums
  8. Vita Janga la Corona: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho watakuwa live JLNH-Star TV - JamiiForums
  9. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Wazuri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile, Wanazungumzia Corona - JamiiForums
  10. Mungu ni Omnipresent. Kufuatia Local Transmission ya Corona. Je, Sasa Tushinikize Watu Wasalie Majumbani Mwao, ila Sadaka Ndio Itumwe Kwa M-Pesa? - JamiiForums
  11. Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!. - JamiiForums
  12. Kwa Kasi Sasa, Jee Tuendelee Ushujaa wa Ka-Corona, Tusitishane, Tuchape Kazi Tukiteketea, Au Sasa Tubadili Msimamo Tusitisishe Mikusanyiko Tuokoke? - JamiiForums
  13. TBC - Mjadala wa Role of The Media kwenye mapambano ya Corona, Je, Media Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  14. Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  15. Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums
  16. #COVID19 - Kama Taifa limekubali chanjo ndio maslahi ya Taifa, Viongozi wote wanakuwa Bind na A Collective Responsibility Clause. Must support, Shut up or quit!
  17. #COVID19 - Baada ya Kukubali Chanjo, na Rais Samia Kuchanja, Kiongozi yeyote anayepinga Chanjo hadharani ni 'Insubordination' na usaliti
  18. #COVID19 - Baada ya Kukubali Chanjo, na Rais Samia Kuchanja, Kiongozi yeyote anayepinga Chanjo hadharani ni 'Insubordination' na usaliti
  19. #COVID19 - Japo Chanjo ni hiyari, ila ni muhimu. Hupandi Ndege bila cheti cha Kupima COVID19. Kama unasafirisafiri, Chanjo ni Muhimu
  20. #COVID19 - Pascal Mayalla: Viongozi wa Umma wajitokeze kuchanjwa, wasiopenda wakae kimya
 
Wanabodi,
Wale wenye access, naombeni muangalie TBC, kuna kipindi live cha majadiliano kikiendeshwa live kutoka Dodoma

P
Siwezi kuangalia maana pale ni unafiki, hakuna atakayesema ukweli wake toka rohoni kuogopa serikali kumpoteza etc!
Media kwa kwetu haina kazi kabisa maana imekatazwa kusema mpaka ielekezwe nini cha kusema!
 
Kwa kiasi fulani wana habari mmefanya kazi kubwa; suala la kunawa mikono limeeleweka mpaka vijijini kabisa. Tuongeze nguvu kwenye mkusanyiko na tupunguze matumizi ya "SOCIAL DISTANCING" huenda hii lugha haieleweki kama "kunawa mikono" ilivyoeleweka.
 
Wajibu wa Media ni nini ?

To give information about current news.....

Sasa wewe mwenyewe jazilizia kama hizo information zinatoka au vipi au wanaziminya hadi kuleta taharuki na kuacha uongo uzagae kutokana na misinformation

Refer the Case ya Vifo vya ndugu zetu hapo hapo ndani na misinformation zilizotoka hadi kupelekea watu kusingiziwa vifo....
 
Labda wewe ndugu Pasco,waulize hao wa Tv yenu, mbona muda wote wanaweka vipindi,Kishindo awamu ya 5,Tunatekeleza,na vipindi vya kuabudu na kusifu mtu mmoja badala ya kuelimisha WANANCHI ambao kimsingi ndiyo wenye TV station yao?
 
WatUjuze nini kiliwakuta akina Lutengano?
Ndio nitaanza kuwaamini
Amiri jeshi mkuu anahamasisha kusali, waziri wa afya anahamasisha ushauli wa kitaalamu, Sasa wananchi wasiojitambua wamsikilize nani?, Ipi Sera ya taifa?, Watu hawataki kumwambia ukweli, magufuli afuate Sera ya wizara ya afya
 
Back
Top Bottom