Mwakyembe apuuza data za JamiiForums!

Status
Not open for further replies.
Acha kujipendekeza wewe sijui unamaanisha nini kusema hivyo! JF ni jukwaa huru sio mali ya Chadema.
Hapo ktk red najipendekeza kwa nani na kwa kipi?
Hapo ktk blue nani kasema JF ni mali ya chadema?
Kila member humu unafikiri ni mwanachama wa chadema?

Akiri yako ni zao la mfumo mbovu wa elimu ya serikali ya ccm (shule za kata).
 
Kipenzi wa jf ama kama walivomuita kamanda hatarini kugeuka adui.
Vigeugeu vya humu ni tatizo sugu
 
Hawa ndio Old School hawaendi na wakati. African spring itawapata with pants down. Muda si mrefu.
 
Nakubaliana na Mwakyembe alichokisema, maana hakuponda kwamba habari zote kwamba si za kweli bali ametoa kama angalizo si kila utajkalolipata JF basi ulichukulie kama ushahidi usio na shaka.

Kuna Memba humu anaitwa Jason bourne ukimuamini huyu habari zake basi ni lazima na wewe utaonekana hamnazo. tuchukulie hili la Mwakyembe kama changamoto watu waache kupost upuuzi na mods muwe faster kuondowa thread zote za kipumbavu ambazo haziendani na hadhi ya JF.
 
Last edited by a moderator:
JF tuna maadui wengi sana wengine wanatukimbiza kimya kimya wengine ndio hao wanapiga mayoweee cha MUHIMU NI KUSIMAMA KWENYE UKWELI TU
 
Nakubaliana na Mwakyembe alichokisema, maana hakuponda kwamba habari zote kwamba si za kweli bali ametoa kama angalizo si kila utajkalolipata JF basi ulichukulie kama ushahidi usio na shaka.

Kuna Memba humu anaitwa Jason bourne ukimuamini huyu habari zake basi ni lazima na wewe utaonekana hamnazo. tuchukulie hili la Mwakyembe kama changamoto watu waache kupost upuuzi na mods muwe faster kuondowa thread zote za kipumbavu ambazo haziendani na hadhi ya JF.

Nashukuru ndugu yangu Matola kwa kuliweka sawa jambo hili mie nimejaribu kusema kidogo hatimaye nimeshambuliwa binafsi...

JF Daima.
 
Last edited by a moderator:
Alichosema ni kwamba "...hilo ndio tatizo la kutegemea sana JamiiForums"; binafsi sioni ubaya wa kauli hii kwani mbali ya kupata habari JF au chanzo kingine chochote, ni vizuri to verify na vyanzo vingine kabla haujawa na uhakika na unachokisema.
Mimi nafikiri kungekuwa hakuna ubaya kama tu muuliza swali angesema chanzo cha habari hiyo ni jamiiforums, kinyume na hapo si sahihi. Angeweza kusema ni tatizo la kutegemea habari za mitandaoni. Hata hivyo nafikiri jibu sahihi ilikuwa kukubali au kukanusha ikifuatkiwa na maelezo kidogo. Bahati mbaya mawaziri wetu wanaleta mipasho/kejeli hata kwenye mambo nyeti kwa usalama na ustawi wa taifa.
 
mh mwakyembe ameikejeli JF wakati akijibu swali la Wenje.
Amesema ukitegemea sana JF unaweza kuwa na hbr ambazo uhakika ni mushikeri

ttz liko wapi hapo, we unaona sawa waziri akitegemea JF 100% (ategemee sana JF)
 
..Mwakyembe amejuaje kwamba Wenje ametoa data zake jamii forums?

..huyu mtu majuzi alikuwa mgonjwa mahututi, leo amepona tayari anajaa KIBURI,KEJELI na DHARAU.

..MWAKYEMBE KIBURI SI MAUNGWANA.

NB:

..ripoti ya Tume ya Mwakyembe ipo JF na inapatikana kwa kila mtu.

..sidhani kama ripoti hiyo inapatikana kirahisi mahala pengine.

..sasa ktk mazingira kama hayo ni vipi Dr.Mwakyembe atoe kauli za kuidharau JF??
 
Credibilty ya JF haiwezi kutegemea mtu mmoja Mwakyembe peke yake. Jamii ndiyo itakayoamua ubora wa chombo chochote cha habari ikiwemo JF. Mtu mwenye hulka kama ya Mwakyembe chombo kikimsifu hata kama ni kwa uwongo atakisifia pia lakini kikisema habari kinyume cha anavyotaka yeye atakiponda, hii ni hulka ya watu wote wapenda sifa na majigambo kama yeye.
Pili katika sera ya JFmwanachama wa JF atawajibika kwa taarifa yoyote atakayotoa (Soma disclaimer ya JF).
 
Mwakyembe hajaikejeli Jf, bali kasema ukweli. Kuna baadhi ya members humu wana tabia ya kutoa taarifa za uwongo
Mkuu Mungi, kauri ya Mwakyembe haikuwa na nia nzuri juu ya JF. Mh. Wenje alinukuu taarifa za hotuba ya kambi rasimi ya upinzani kuuliza swali lake, sasa Mwakyembe alijuaje kuwa hotuba hiyo ilikuwa na taarifa kutoka JF?
 
Katika hatua za mwisho za kupitisha bajeti ya Miundombinu, Wenje alisimama na kusema kuwa ana taarifa za kuwepo vikao vya kuipa kampuni fulani bandari(sijaimaki vizuri) ikiwa ni namna ya kulipa deni la ATCL ambalo ni kubwa mno.
Mwakyembe amejibu kuwa kama kuna mtu anafanya hiyo mipango bila kumjuza yeye aendelee.
Lakini katika hali isiyo ya kawaida akamwambia Wenje, kuwa ana wasiwasi na taarifa zake, na akamalizia..."Ndiyo shida ya kutegemea habari za JamiiForums hiyo!
Mwakyembe Anaichkuliaje Jf huyu?

Ni dhahiri kuwa Mwakyembe naye ni Member wa Jf. Tatizo id anayotumia. Au Pj ndiye Mwakyembe?
 
mmmh, itabidi PWC au Ernest & Young waajiriwe hapa kwa ajili ya ku-verify data ili ziwe zinatumiwa bungeni.

Sio lazima azikubali kama haziamini.
 
Kumbe ni JF iliyomdanganya mpaka akaenda kuomba ulinzi wa Polisi alipopata ile ajali.........lol
 
Mtu makini hapaswi ku dismiss kiurahisi taarifa yoyote. Uongo na uzushi upo kwa kweli lakini huwezi kujua kabla hujaufanyia kazi.

Fanya uchunguzi unaweza kuku lead kwenye ukweli.
 
Status
Not open for further replies.
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom