Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,614
Wanabodi,

Kila nipatapo fursa, huwaletea mfululizo wa makala zangu elimishi za kuhamasisha uzalendo zinazoitwa "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo huwa ziko kwa mtindo wa maswali. Makala ya leo sio ya swali bali ni wito.

Tanzania ni nchi yetu sote, na imetokea sisi Watanzania tuko wengi na tumetapakaa duniani kote. Kutokana na kutapakaa huku, Watanzania tofauti tofauti tuna uwezo tofauti na exposure tofauti kutokana na experiences tofauti tofauti ya huku tulipo, lakini bado tunawajibu wa kuelekeza uzalendo wetu kwa nchi yetu, Tanzania yetu au Mama Tanzania, hivyo kama kuna mwenzetu yeyot, mwenye uwezo wowote wa kusaidia, asaidie, ama kama yuko kwenye nchi yoyote, yenye mazingira sawa na yetu, wenzetu huko kuna kitu wamefanya kikasaidia, na kitu hicho sisi tunaweza kufanya kikasaidia, then saidia nchi yako kwa kushauri, what should we do, ili kuisaidia nchi yako.

As the Corona situation ya maambukizi ya local transmissions is escalating, nimenote huku kwenye mitandao ya kijamii, baadhi yetu tumeanza kunyoosheana vidole vya kulaumu, kuwa hatukufanya hiki au kile ndio maana maambukizi yamefikia kiwango hiki, kwa hapa tulipo, badala ya kulaumu, nini hakukufanyika, toa ushauri wa kusaidia, lets share the best practices za nini kifanyike sasa kusaidia hapa tulipo before its too late.

Tangu kuibuka kwa janga hili la Corona Mwezi December mwaka jana, kila nchi ilichukua hatua za kuzuia na kujiandaa kukabiliana nayo ki vyake vyake. Sisi Tanzania pia kupitia serikali yetu nasi tulichukua hatua kivyetu. Ziko nchi za jirani zetu wao waliamua kuchukua hatua zao kwa copy and paste ya nchi nyingine walichofanya ikiwemo hatua ya lockdown, Tanzania tukaamua hatuigi, hakuna lockdown na rais wetu Magufuli kutuondoa wasiwasi kwa kusema Tusitishane, na kutuhimiza Watanzania tuendelee kuchapa kazi kwa kuzingatia maelekezo ya kitaalamu na kusema haka ka Corona ni ka ugonjwa kadogo, ni kashetani, tuka mkabidhi Mungu, na kwenye Mungu akatenda. Tatizo la Corona wa kulaumiwa ni Serikali kwa asilimia 100% - JamiiForums

Mwanzoni Mungu ametenda na mpaka sasa anaendelea kutenda, jana tumemaliza siku 3 za maombi ya kitaifa dhidi ya janga la Corona, hivyo tunamuomba Mungu huku tunajisaidia.

Kufuatia kuongezeka kwa kasi ya maambukizi ya Corona, huku kwenye mitandao ya kijamii, tunaanza kulaumiana na kunyoosheana vidole kuwa Corona inasambaa kwasababu hatukufanya abcd.

Hii ni mifano
Vifo na maambukizi ya Corona ni matokeo ya Serikali kushindwa.

Mwezi May watu wajiandae kuona umma unavyopukutika!

JokaKuu Pascal Mayalla tindo
Mkuu Nguruvi3 at this juncture, lets stand as one kusaidia. Je, Watanzania wenye uwezo wa kusaidia, jee tuisaidiaje serikali yetu ili ishindindwe?.

Kwa vile sasa ni April na umma haupukutiki bali unaambukizwa, na kwa vile umeishajua kuwa mwezi May umma utapukutuka, hivyo unashauri tujiandae kuona umma unavyopukutika!, kwanini usisaidie kuzuia umma wa Watanzania usipukutike?

Usaidizi huo, sio lazima uwe kama ule wa Rostam Aziz or Mo Dewji, bali hata kwa kuandika tuu humu jf na vyombo vyetu vya maamuzi watasoma na kufanya uamuzi wafuate au waache, ili itakapofika hiyo May, tutakapo anza kuona na kushuhudia jinsi watu wanavyopukutika, angalau tutasema, tuliona kabla, tukaonya, tukashauri, tukapuuzwa na sasa haya ndio matokeo.

Kwenye situation hii tuliofikia, swali langu hili
WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums

Pascal Mayalla , huwezi kumshauri mkaidi! Wacha nature to take its course. Let Darwin's theory of evolution take place, let Natural selection take its course, those fittest will survive the virus and those not well adapted will perish! OR Kuna kitu kinaitwa Herd immunity, ngoja hiyo May or some months to come at least 90% or more of Tanzanians will be infected and those fittest to survive will have acquired immunity and transmission interrupted!?
Mkuu Retired, if you can help, just help out, kama una ushauri mzuri wa jinsi ya kusaidia, wewe toa tuu huo ushauri, sasa issue ya kama ushauri wako utapokelewa utakubaliwa au utafanyiwa kazi au laa, hili sio letu, hili ni la ngazi za maamuzi, whether ushauri wako utatekelezwa au utapuuzwa, hili sio lako, wewe utakuwa umetimiza wajibu wako na huu ndio uzalendo wako kwa nchi yako.

Hitimisho
Nimalizie kwa kutoa wito, janga la Corona ni janga letu sote sisi Watanzania, haijalishi uko wapi na unaishi nchi gani, as long as wewe ni Mtanzania, hata kama umejilipua, lakini kwenu ni Tanzania, una wajibu wa kuisaidia nchi yako kwenye nyakati kama hizi. Huu sio wakati wa kulaumiana na kunyoosheane vidole vya we didn't do this and that, huu ni wakati wa kusimama pamoja, kushikamana na kusaidiani, kama unaweza kusaidia kwa lolote, chochote, hali na mali au hata ushauri tuu to help out the situation, please just do!, usisubiri uombwe, msaada na yeyote. Jitokeze tuu saidia!. Vinginevyo...Nyamaza!

Nawatakia Jumatatu Njema
Paskali
Rejea za Mandiko ya The Same Author Kuhusu Janga la Corona
  1. Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani? - JamiiForums
  2. Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa - JamiiForums
  3. Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best! - JamiiForums
  4. RC Makonda, Dar ni jiji la wote, vyama vyote. Mbowe sio mwanasiasa uchwara aliyefilisika, Zitto sio mshirikina. Tunakupenda, heshimu wote uheshimiwe - JamiiForums
  5. Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out! - JamiiForums
  6. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, azungumzia wajibu wa vyombo vya habari kuripoti janga la Corona - JamiiForums
  7. Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani!. Je Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika - JamiiForums
  8. Vita Janga la Corona: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho watakuwa live JLNH-Star TV - JamiiForums
  9. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Wazuri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile, Wanazungumzia Corona - JamiiForums
  10. Mungu ni Omnipresent. Kufuatia Local Transmission ya Corona. Je, Sasa Tushinikize Watu Wasalie Majumbani Mwao, ila Sadaka Ndio Itumwe Kwa M-Pesa? - JamiiForums
  11. Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!. - JamiiForums
  12. Kwa Kasi Sasa, Jee Tuendelee Ushujaa wa Ka-Corona, Tusitishane, Tuchape Kazi Tukiteketea, Au Sasa Tubadili Msimamo Tusitisishe Mikusanyiko Tuokoke? - JamiiForums
  13. TBC - Mjadala wa Role of The Media kwenye mapambano ya Corona, Je, Media Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  14. Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
  15. Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums
 
Mbona kama vitisho tena? Hii nchi ina uongozi kuanzia mjumbe wa nyumba kumi hadi mh Rais pale juu kabisa ya hierarchy, kwa hiyo kuliko kutishina tishana ni bora tuwaachie wao wafanye vile wanavyoona inafaa hata kama fyongo. Si ndio viongozi wetu?
 
Simba wamevamia kijijini, watu wakatangaziwa waingie majumbani na wafunge milango mpaka hao simba watakapodhibitiwa.

Kwenye kaya moja baba mwenye nyumba akasikika akijigamba kwamba hakuna kufunga milango kwani simba si chochote si lolote hawana la kuifanya kaya yake.

Ghafla simba wakaivamia nyumba na wakaingia mpaka ndani. Hapa na pale baba akafanikiwa kufunga mlango lkn tayari simba kadhaa walishaingia ndani na kuwadhibiti ni ngumu. Ndani kuna simba na nje kuna simba, wakajikuta wako kwenye dilemma maana hakuna pa kukimbilia.

Wakati haya yanatokea baba alikuwa nyumba ya uani huku akiwa amefunga milango yote na maagizo akiyatolea dirishani.

Mpaka sasa kijiji kinahoji kulikuwa na haja gani ya kusubiri simba waingie ndio tufunge milango? Sababu kwa vyovyote vile ilikuwa lazima milango ifungwe, iwe simba wakiwa wameshaingia ama kabla hawajaingia. Sasa wanakijiji wanajiuliza kwa nini hii familia ilisubiri mpaka simba wamewavamia ndio wafunge milango?

Unforgetable
 
Tumekusikia mkuu.

mchango wangu kwa sasa ni kuishauri serekali iache kwa muda kutumia kodi zetu kwenye miradi ya matrilioni (SGR, Stiegler's Gorge, etc) na badala yake zielekezwe kwenye:

1) kununua/kutengeneza mobile testing kits za COVID-19 ili kuwezesha mass testing

2) uimarishaji/ujenzi wa isolation centres

3) gawio kwa kaya zitakazokuwa zimeathirika zaidi
 
Watu wametoa ushauri sana lakini haujazingatiwa, vyama vya siasa pia vimetoa ushauri lakini hawaeleweki sembuse watoa ushauri wenye akaunti zilizoficha identy yake?

Haya mi nashauri wale wote wanaotoka Dar na Zanzibar kwenye maambukizi mengi wakienda Mikoani wafanyiwe karantini kwa siku 14 kabla hawaajenda kwenye mashughuli yao ili wasieneze mikoani. Na Kwenye vyombo vya usafiri wahakikishe kila abiria anavaa mask na wapimwe joto.
 
Mkuu Nguruvi3 at this juncture, lets stand as one kusaidia. Jee Watanzania wenye uwezo wa kusaidia, jee tuisaidiaje serikali yetu ili ishindindwe?.
Pascal Mayalla , mimi narudia, huwezi kusaidia mtu ambaye for sure 100% hasikilizi la mtu. Tunachoweza kufanya ni kumlaumu na kukusanya tuhuma zetu for future reference na kumwajibisha mtu aweye yoyote kwenye hili janga la Corona! Uttachaje upinzani kwenye ishu kama hii, angalau Waziri Kivuli wa Upinzani...
 
Huu sio wakati wa kutafuta mchawi tena, kama "mistake" ilishatokea, now lazima tusonge mbele, kupoteza muda mwingi kulaumu hakutasaidia chochote tena.

Tukicheza tutawapoteza mpaka wapendwa wetu, hakuna haja kufika huko, huu ni wakati wa kuwa wamoja kupambana na hili gonjwa, na sio kuendelea kumfikiria mtu mmoja, kumbuka yeye anaweza akabaki, wewe na wenzako mnaweza kuondoka msipochukua tahadhari.

Ukisema huipendi CCM, kumbuka kuna marafiki na jamaa zako wako huko huko CCM, na ukisema huipendi CHADEMA, pia kuna marafiki na jamaa zako wako huko usipopapenda.

Wote kwa pamoja tusingependa kuwapoteza marafiki na jamaa zetu, huu ni wakati wa kujilinda, kushauri, na kufarijiana, ili sote kwa pamoja tuvuke salama kipindi hiki.

Pole kwa wote walioondokewa na ndugu, marafiki, na jamaa zao kutokana na huu ugonjwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye hii ishu ya corona kuna watu hasa wapinzani wataaibika sana.

Kuna watu sasa hivi wanatamani waanze kuona watu maelfu wanakufa ili wapate cha kusema.

Bahati mbaya sana hili suala litapita bila madhara makubwa, alafu sikilizia watu watakapo pokea kichapo cha mbwa koko ikifika oktoba mwaka huu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla , mimi narudia, huwezi kusaidia mtu ambaye for sure 100% hasikilizi la mtu. Tunachoweza kufanya ni kumlaumu na kukusanya tuhuma zetu for future reference na kumwajibisha mtu aweye yoyote kwenye hili janga la Corona! Uttachaje upinzani kwenye ishu kama hii, angalau Waziri Kivuli wa Upinzani...
Kwa hiyo kumbe shida yako ni upinzani?

Hili suala litapita bila hayo unayoyafikiria kutokea. Na mniandae kwa aibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom