Muda wa kuomba mkopo HESLB kwa kozi zilizoongezwa Januari 3, 2024 uongezwe ili kuruhusu kukamilisha maombi

Jimmy the Doctor

New Member
Sep 30, 2023
1
1
Habari, Naomba tujadili hili ni sawa?

Tarehe 3 January 2024 bodi ya mikopo ilitangaza kuongeza KOZI mpya tatu zitakazonufaika kwa mikopo diploma na kueleza kuwa maombi ya mikopo yataanza tokea siku hiyo. Katika taarifa hiyo Bodi ya mikopo HESLB haijataja deadline au siku ya kufunga dirisha la mikopo ni lini.

Hivi Sasa wengi walikuwa hawafahamu dirisha litafungwa lini na kwakuwa taarifa ilitoka jumatano. Nilijaribu kupiga Simu kuuliza jumamosi Ila hazipokelewi nikauliza nikaambiwa huwezi ukapiga simu jumamosi Wala jumapili maana ukipiga huwa hazipokelewi kwasababu sio siku za kazi.

January 8 Jumatatu asabuhi nilipiga Simu kuuliza utaratibu nikapewa Majibu na mtoa huduma kuwa mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 11 January 2024 lakini taarifa hiyo haikuwekwa kwenye tovuti ya Bodi ya mikopo HESLB.

Nikaanza utaratibu wa kuomba mkopo Mimi na wenzangu tukafanikiwa kulipa gharama zinazohitajika. lakini hatua zinazofuata inabidi upate namba ya uhakiki baada ya kuhakiki cheti Cha kuzaliwa RITA pia na cheti Cha kifo kwa wengine waliofiwa na wazazi. Kwa Utaratibu wa RITA mbaka upate cheti Cha kuzaliwa unasubiri siku 3 mbaka siku saba ndipo upate cheti kilichohakikiwa. Sasa tokea nimeomba kuhakikiwa siku saba ndo zimeisha Leo hii Jumatatu tarehe15 ndo Nmepewa namba ya uhakiki.

Cha kushangaza dirisha limefungwa hatuwezi Tena kufanya mambi ya mkopo na kwa maelezo Yao dirisha limefungwa Alhamis tarehe 11 January 2024, Kiuhalisia Kwa KOZI mpya zilizoongezwa hatujapewa muda wa kutosha kukamilisha maombi ya mkopo na ukweli wengi wenye Nia ya kuomba mkopo wamekwamishwa na muda wa maombi.

Muda uliopo hautoshelezi kabisa. Sasa sijui kwanini bodi ya mikopo HESLB hauoni Kama Kuna haja ya kuweka muda ambao utaendana na uwezo wa RITA kuhakiki vyeti, maana RITA wanakamilisha uhakiki siku 3 mbaka siku 7 na ukipiga hesabu dirisha limefunguliwa tarehe 3 na limefungwa tarehe 11 ni muda wa siku 10 tu. Kitu ambacho hakiendani na uhalisia . Hakika Kuna watu wapo vuuoni wanalia wakiamini wangepata Msaada lakini muda hautoshi. Naomba viongozi mlione hili, Kuna watu tulishalipia kabisa lakini RITA hawajakamilisha uhakiki Sasa sisi wanafunzi tufanyaje?

Ukipiga Simu hawapokei wikend sio siku za kazi na hizo wikend nazo zinahesabika ndani ya siku hizo hzio 10 zilizotolewa na bodi ya mikopo kufanya maombi. Viongozi tusaidieni hili muda wa kufanya maombi kwa KOZI ZILIZOONGEZWA January 3, 2024 UONGEZWE tafadhali ili kusaidia vijana Wenye uhitaji vyuoni.
 

Attachments

  • Screenshot_20240115-151505.png
    Screenshot_20240115-151505.png
    38.1 KB · Views: 7
Mimi naombeni kujua nawezaje kufahamu kiwango cha mkopo niliokwisha rejesha. Nilikuwa naingia online ila kwa sasa hata hazifunguki. Naombeni kwa mwenye kujua
 
Back
Top Bottom