MPIGA ZEZE
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 2,539
- 2,296
Napata wasi wasi kama kweli mtu aliyeshtakiwa ndiye muuaji !!! Jina gani hili "PACIFICUS CLEOPHACE SIMON"full Eurocentric, kama la kutengezwa vile, halina ubini wa kibantu. Labda ndio maana hakuwa na roho ya utu !!! Lakini kwa kuwa atakuwa amesoma shule yo yote Taanzania na kuishi naye mtaani, atakuwa anafahamika. Kwa kuwa JF ni mwisho wa yote, naomba yeyote ambaye anakumbuka kukutana na jina la namna hiyo katika maisha yake aniondoe wasi wasi.
Sawabho, pengine hili limekupiga chenga kidogo ama hufatilii dynamics za utamaduni wa Bongoland. Wazazi walio wengi wa zama hizi za sasa wameibuka na mtindo mpya wa kutopenda kuwapa watoto wao utambulisho wa ubini wa kibantu. Ni mtindo unaozidi kushika kasi. Ni aibu na ni bahati mbaya. Sababu za uhakika hazijulikani lakini ninahisi ni kuwakwepesha wasihusishwe na makabila (unajua ubini wa kibantu unatambulisha kabila la mhusika) wakati tulipaswa kujivunia urithi huo ambao ndio nguvu ya taifa. Hata hivyo kitu ambacho hakitakwepeka na ninatabiri kitaendelea kulisumbua taifa ni utambulisho wa udini kupitia majina hayo hayo. Kumbe kama tungechukua mkondo wa kutumia utambulisho wa ukabila badala ya udini, ingekuwa neema zaidi yanayokuja!! Hii ndio Bongoland - tumechanganyikiwa!!