Polisi aliyekodi majambazi kumuua mumewe akamatwa, hawara ni miongoni mwa wahusika

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Siku moja baada ya taarifa za mkaguzi msaidizi wa polisi kituo cha USA River Mkoani Arusha, Demetrida Sweethbert Thadeo kuanikwa kupitia mtandao wa Jamii Forums akidaiwa kukodi majambazi ili kumuua mumewe, hatimaye jeshi hilo limemkamata na yupo mahabusu imefahamika.

Taarifa za uhakika zimedai kwamba Demetrida amekamatwa mapema leo akituhumiwa kukodi majambazi ili wamuue mume wake Daud Thomasi Ayo ambaye wamekuwa na migogoro wa kifamilia kwa muda mrefu.

Miongoni mwa majambazi wanaohusishwa na mpango huo yumo mwanaume mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Ombeni(anatafutwa na polisi ametoroka) anayedaiwa kuwa hawara wa askari huyo .
IMG-20240103-WA0004.jpg

Daud Thomas Ayo​
IMG-20240103-WA0003.jpg

Demetrida Sweetbert Thadeo​

Taarifa zimedai kwamba tayari namba ya askari huyo imenyofolewa na kutumwa makao makuu ya jeshi hilo kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu.

Demetrida Mkazi wa Momela anatuhumiwa kukodi majambazi waliomjeruhi kwa mapanga mumewe Daud Thomasi Ayo kutokana na ugomvi wa kifamilia.

Daudi amekuwa akimtuhumu mkewe huyo kwa usaliti wa ndoa na mahusiano ya kimapenzi yasiyofaa.
Jambo linaloweza kuchangiwa na hawara kushiriki njama za kumuua ili wawe huru na mahusiano.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani za jeshi hilo na kuthibitishwa na Mumewe, tukio hilo lilitokea usiku wa Desemba 24, 2023 nyumbani kwao Momela ambapo watu wasiojulikana walimvamia akiwa anaingia nyumbani kwake akijaribu kufungua geti ndipo watu wanne walijitokeza na kuanza kumkatakata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Inadaiwa kuwa siku chache kabla ya tukio hilo Lemetilda alionekana akiharibu mfumo wa kamera za nyumbani kwao (CCTV Camera)na mumewe alipomuuliza kwanini anazima kamera hakuweza kutoa majibu ya maana ila alisema anarekebisha.

Taarifa zinasema kuwa wanandoa hao ambao wamebahatika kuwa na watoto wawili akiwemo mchanga wa kunyonya, Mume amekuwa akimtuhumu kujihusisha na mahusiano yasiofaa na mara nyingi tangia amejifungua alikuwa hamnyonyeshi mtoto ipasavyo na wakati mwingine amekuwa akilala nje ya ndoa na kurejea asubuhi.

Ayo ambaye amelazwa katika hospitali ya ALMC, jijini Arusha, alithibitisha kutendewa unyama huo na mkewe kutokana na ugomvi wa Mara kwa mara ndani ya familia na kwamba kati ya majambazi wanne waliomvamia siku hiyo mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Agustino anashikiliwa katika kituo hicho cha polisi na upelelezi unaendelea.

Hata hivyo taarifa zimedai kuwa baada ya mtuhumiwa kuhojiwa na polisi, alikiri kuhusika na tukio hilo na kueleza kuwa yeye na wenzake walitoka Dar es salaam baada ya kuahidiwa na askari huyo ujira wa sh. milioni 3 na tayari walikabidhiwa kitita cha sh. 500,000 kama malipo ya awali kwa ajili ya kumuua mumewe.

"Hawa vijana aliwakodi kutoka Dar ili wamuue mume wake na siku ya tukio huyo mkewe (Askari) alikuwemo ndani ila alizima CCTV CAMERA na mumewe alipokuja majira ya saa nne usiku vijana hao walimvamia baada ya kuteremka kwenye gari na kuanza kumkatakata na alipoanguka chini walijua amekufa na wote walitoweka" kilisema chanzo ndani ya jeshi hilo.

Daudi alipotakiwa kuongelea tukio hilo mara ya kwanza alikubali na kuahidi kutoa ushirikiano lakini baadaye alipoitwa kutoa maelezo kituo cha polisi aliomba asiongee na mwandishi wa habari kwa madai kwamba amekatazwa na polisi baada ya kuahidiwa, kumchukulia hatua za kinidhamu kwa mkewe.

Baadhi ya askari polisi kituoni hapo wamesikitishwa na tukio hilo wakidai kwamba mara kadhaa mumewe amekuwa akija kituoni hapo kwa mkuu wa kituo afande ODC, kulalamika kuhusu tabia na mwenendo wa mkewe.

Baba mzazi wa Daudi, Thomas Ayo alikiri kuwa ndoa ya wawili hao ina mgogoro wa mara kwa mara na amesikitishwa sana na tukio hilo na mwanaye alimwambia aliyehusika ni mkewe ila polisi wamemzuia asiongee kwa waandishi wa habari kwani jeshi hilo limemwahidi kumfukuza kazi mkewe.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo alipoulizwa alisema bado hajapata taarifa ila aliahidi kulifuatilia kwa wasaidizi wake na kulitolea ufafanuzi.

"Ndo nalisikia kwako ila ngoja nifuatilie nitakupa taarifa"

Hata hivyo ndugu na jamaa wamelalamikia hatua ya askari huyo kutochukuliwa hatua ikiwemo kufukuzwa kazi kwani kwa kuwa anakabiliwa na tuhuma nyingi ambazo jeshi hilo linazifumbia macho, ikiwemo kashfa ya usagaji..

Ends......

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
 
Siku moja baada ya taarifa za mkaguzi msaidizi wa polisi kituo cha USA River Mkoani Arusha ,Demetrida Sweethbert Thadeo kuanikwa kupitia mtandao wa Jamii Forum akidaiwa kukodi majambazi ili kumuua mumewe,hatimaye jeshi hilo limemkamata na yupo mahabusu imefahamika.

Taarifa za uhakika zimedai kwamba Demetrida amekamatwa mapema leo akituhumiwa kukodi majambazi ili wamuue mume wake Daud Thomasi Ayo ambaye wamekuwa na migogoro wa kifamilia kwa muda mrefu

Miongoni mwa majambazi wanaohusishwa na mpango huo yumo mwanaume mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Ombeni(anatafutwa na polisi ametoroka) anayedaiwa kuwa hawara wa askari huyo .

Taarifa zimedai kwamba tayari namba ya askari huyo imenyofolewa na kutumwa makao makuu ya jeshi hilo kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu.

Demetrida Mkazi wa Momela anatuhumiwa kukodi majambazi waliomjeruhi kwa mapanga mumewe Daud Thomasi Ayo kutokana na ugomvi wa kifamilia.

Daudi amekuwa akimtuhumu mkewe huyo kwa usaliti wa ndoa na mahusiano ya kimapenzi yasiyofaa.
Jambo linaloweza kuchangiwa na hawara kushiriki njama za kumuua ili wawe huru na mahusiano.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani za jeshi hilo na kuthibitishwa na Mumewe,tukio hilo lilitokea usiku wa desemba 24,2023 nyumbani kwao Momela ambapo watu wasiojulikana walimvamia akiwa anaingia nyumbani kwake akijaribu kufungua geti ndipo watu wanne walijitokeza na kuanza kumkatakata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Inadaiwa kuwa siku chache kabla ya tukio hilo Lemetilda alionekana akiharibu mfumo wa kamera za nyumbani kwao (CCTV Camera)na mumewe alipomuuliza kwanini anazima kamera hakuweza kutoa majibu ya maana ila alisema anarekebisha .

Taarifa zinasema kuwa wanandoa hao ambao wamebahatika kuwa na watoto wawili akiwemo mchanga wa kunyonya,Mume amekuwa akimtuhumu kujihusisha na mahusiano yasiofaa na mara nyingi tangia amejifungua alikuwa hamnyonyeshi mtoto ipasavyo na wakati mwingine amekuwa akilala nje ya ndoa na kurejea asubuhi.

Ayo ambaye amelazwa katika hospitali ya ALMC,jijini Arusha,alithibitisha kutendewa unyama huo na mkewe kutokana na ugomvi wa Mara kwa mara ndani ya familia na kwamba kati ya majambazi wanne waliomvamia siku hiyo mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Agustino anashikiliwa katika kituo hicho cha polisi na upelelezi unaendelea.

Hata hivyo taarifa zimedai kuwa baada ya mtuhumiwa kuhojiwa na polisi ,alikiri kuhusika na tukio hilo na kueleza kuwa yeye na wenzake walitoka dar es salaam baada ya kuahidiwa na askari huyo ujira wa sh,milioni 3 na tayari walikabidhiwa kitita cha sh,500,000 kama malipo ya awali kwa ajili ya kumuua mumewe.

"Hawa vijana aliwakodi kutoka Dar ili wamuue mume wake na siku ya tukio huyo mkewe (Askari) alikuwemo ndani ila alizima CCTV CAMERA na mumewe alipokuja majira ya saa nne usiku vijana hao walimvamia baada ya kuteremka kwenye gari na kuanza kumkatakata na alipoanguka chini walijua amekufa na wote walitoweka" kilisema chanzo ndani ya jeshi hilo.

Daudi alipotakiwa kuongelea tukio hilo mara ya kwanza alikubali na kuajidi kutoa ushirikiano lakini baadaye alipoitwa kutoa maelezo kituo cha polisi aliomba asiongee na mwandishi wa habari kwa madai kwamba amekatazwa na polisi baada ya kuahidiwa, kumchukulia hatua za kinidhamu kwa mkewe.

Baadhi ya askari polisi kituoni hapo wamesikitishwa na tukio hilo wakidai kwamba mara kadhaa mumewe amekuwa akija kituoni hapo kwa mkuu wa kituo afande ODC, kulalamika kuhusu tabia na mwenendo wa mkewe.

Baba mzazi wa Daudi,Thomas Ayo alikiri kuwa ndoa ya wawili hao ina mgogoro wa mara kwa mara na amesikitishwa sana na tukio hilo na mwanaye alimwambia aliyehusika ni mkewe ila polisi wamemzuia asiongee kwa waandishi wa habari kwani jeshi hilo limemwahidi kumfukuza kazi mkewe.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo alipoulizwa alisema bado hajapata taarifa ila aliahidi kulifuatilia kwa wasaidizi wake na kulitolea ufafanuzi.

"Ndo nalisikia kwako ila ngoja nifuatilie nitakupa taarifa"

Hata hivyo ndugu na jamaa wamelalamikia hatua ya askari huyo kutochukuliwa hatua ikiwemo kufukuzwa kazi kwani kwa kuwa anakabiliwa na tuhuma nyingi ambazo jeshi hilo linazifumbia macho,ikiwemo kashfa ya usagaji..

Ends......

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
DUNIA INA MAMBO
 
Miongoni mwa majambazi wanaohusishwa na mpango huo yumo mwanaume mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Ombeni(anatafutwa na polisi ametoroka) anayedaiwa kuwa hawara wa askari huyo .

Sent using Jamii Forums mobile app
Hatufanyahi hivyo amekosea sana Ilikuwa swala. Lamkupeleka moto usiku mchana hadinkitumbua kiive mwenyewe anaapeleka ombi la talaka
 
Back
Top Bottom