Mtuhumiwa ma mauaji ya Mwangosi afikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali

Huyu bwana hakutok nyumbani kwake kwa dhamira ya kwenda kuua bali aliitwa na mkuu wake kufanya kazi aliyoifanya. Kwa bahati mbaya majeshi yetu hufuata amri ya aliyekuzidi cheo. Kumshtaki kama muuaji nakataa ila inatakiwa waliomtuma wakamatwe kwani asingefanya alichoamriwa kufanya angekitia kitumbua chake mchanga. SERIKALI IACHE UONEVU IJUE INATENDA DHAMBI KWA KUTOMKAMATA KAMHUNDA, OCD NA YULE ASKARI ALIYEKUWA AMEVALIA KIRAIA. Mtaendelea kutoa kafara watoto wa wenzenu hadi lini!!
 
Kamuanda ameachwaje sasa kwenye hili wakati yeye ndio aliwakodi kutoka mbeya na iringa???
 
Upepelezi gani ambao haujakamilika?? wapeleke haraka kwenya mahakama yenye uwezo wa kusikiliza kesi hiyo..then ni muhimu kwa wliokuwepo kwenye duara kushtakiwa
 
you gotta be shitting me!!!!you feel what?this punk is a cold-blood killer i wonder how many have died by his hands...eye for an eye tooth for tooth,kill the killer godamit..

This boy was acting basing on orders. He is just a scape goat like others that we have seen.
 
ukweli mpaka sasa sijaamini kama aliyepelekwa mahakamni ndiye mhusika maana ccm na polisi kwa fake wako juu sana wanaweza kuchukua jamaa tu na kumweka pale ili kupoteza lengo
 
Chagonja ndie shaidi namba moja hasa baada ya kutoa taarifa ya kuwa Marehemu alipigwa na kitu kilichorushwa
 
This boy was acting basing on orders. He is just a scape goat like others that we have seen.
mkuu bosi wako akikwambie ule mavi nina uhakika utakaa..what is wrong is wrong and right is right,..pouring syrup on a shit doesn't make it a pancake!!!
 
HATIMAYE yule askari Polisi, PC Pacificus Cleophas Simon (23) anayedaiwa kufyatua bomu lililomuua kinyama mwandishi Daudi Mwangosi wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, amefikishwa mahakamani leo na kusomewa mashitaka ya mauaji.

Askari huyo mwenye namba za kipolisi 2573, alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, Lymo na kusomewa mashtaka ya kumwua Mwangosi bila kukusudia, Septemba 2 mwaka huu.

Mwendesha Mashtaka, Michael Lwena, aliiambia mahakama kuwa upelelezi kuhusiana na tukio hilo bado unaendelea. Mshitakiwa PC Simon hakutakiwa kujibu lolote kwani mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza mashauri ya mauaji. Hakimu Lymo aliiahirisha kesi hiyo hadi Septemba 26 mwaka huu.

Wakati akiingizwa na kutolewa kwenye viwanja vya mahakama, mshitakiwa Simon alikuwa akilindwa vikali na polisi wenzake ambapo kundi la askari zaidi ya saba walimzingira na kuzuia asipigwe picha na waandishi wa habari.

Habari zaidi zinasema, Askari wote walioonekana kwenye ushahidi wa picha wakimshambulia marehemu Mwangosi, walikamatwa.

Marehemu Mwangosi aliuawa kwa bomu Septemba 2 wakati akiripoti tukio la polisi kuwazuia wafuasi wa Chadema waliodaiwa kuandamana kinyume cha sheria kwenye tukio la ufunguzi wa tawi la chama chao kijiji cha Nyololo wilayani Mufindi mkoani Iringa. Mlipuko wa bomu katika tukio lililomuua Mwangosi ulidaiwa pia kumjeruhi vibaya askari polisi anayetajwa kwa jina la Aceli Mwampamba.

Jana, wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam waliandamana kulaani mauaji ya Polisi dhidi ya mwenzao, Mwangosi. Maandamano hayo yalifanyika kuanzia katika kituo cha Channel Ten na kumalizikia kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam. Katika maandamano hayo ya waandishi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, alilazimika kuondoka baada ya waandishi 'kumtimua' kwa kudai kwamba hawajamualika.

Source: wavuti - wavuti


My Take!
Kaua bila kukusudia na wakati kauli ya kwanza ya viongozi wa serikali ni kua hakuuawa na Police bali kitu kilichorushwa kwa nia ya kudhulu police. Pia kwa kua swala hili limefika mahakamani basi zile tume zisitishe ufuatiliaji( Kwa mujibu wa KAULI ZA BUNGENI DODOMA)
 
September 12, 2012

BREAKING NEWssssssssMTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI AFIKISHWAMAHAKAMANI LEO IRINGA




Baadhi ya wanahabari wakitoka mahakamani


Askari anayetuhumiwa kumuua Daudi Mwangosi leo amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya mkoa wa Iringa na kusomewa mashitakata yake. Huku akiwa chini ya ulinzi mkali ambao ulifanya wanahabari waliofika mahakamani kujitahid kupata picha kwa ugumu.

Akisoma mashtaka mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya Daines lymo mwendesha mashtaka ameeleza kuwa mtuhumiwa Pacificus Cleophase Simon (23

HABARI KAMILI ITAKUJIA HIVI PUNDE




Mkuu kwa msimamo wangu huyo askari hakujituma kunawatu walitoa amri ya kufanya hayo mauwaji mbona hawajakamatwa???? Huyo RPC Iringa si aliambiwa kuna mwandishi napigwa akafunga vioo vya gari na kuondoka eneo la tukio badala ya kuzuia kabla hajauwawa, hapo huoni vijana walikuwa wanatekeleza amri ya kamanda???? Huyo RPC, OCD, IGP wanatakiwa wapelekwe mahakamani watachujana hukohuko kila mtu atasema alitumwa na nani, who commandeered the operation to kill??? ICC haiwezi kukamata dagaa ikaacha big fish!!!
 
Huu ni mwanzo angalau hawa jamaa wataacha kutumia silaha ya moto hata kama wamepata amri toka kwa mkuu wao, zamani ilikuwa mtu hapigwi bunduki mpaka kuangalia aina la kosa hata kama atatoroka chini ya ulinzi lakini siku hizi imekuwa kawaida hata ukihisiwa ni jambazi ukaonekana kutaka kukimbia au kujaribu kukimbia unatunguliwa tena kichwani au tumboni wakati enzi hizo inapigwa juu mara 2 usipotii unalengwa mguuni (watu wanakimbia sometime kwa kuwa wanaogopa kipondo cha police kwani kwa police hakuna mtuhumiwa bali unaonekana ni mhalifu)
 
Nilitegemea hawa askari sita (ningemuondoa huyo mmoja aliyemkumbatia Mwangosi) wote wangeshitakiwa kwa mauaji ya Mwangosi pamoja na RPC Kamuhanda. Lakini serikali ya ccm imeamua kuwatukana watanzania kwa kumshitaki mmoja wao.
huyo mwenye kofia ya kiraia na t-shirt ya blue bahari(samawati)angalia hiyo suruali aliyovaa ni kama kombati za TISS, angalia kwa makini hiyo suruali ni tofauti na zile za jwt.Inawezekana kuna wahusika zaidi ya jeshi la polisi.
 
mkuu bosi wako akikwambie ule mavi nina uhakika utakaa..what is wrong is wrong and right is right,..pouring syrup on a shit doesn't make it a pancake!!!

Hey man sihalalishi kuuwa kwa mwandishi wa habari na wala sijawahi kufanya hivyo. My sadness to the boy is because he has been set up in a trap that he can't get out. Remember 23 yrs ni mdogo sana na nijuavyo mimi ni rahisi sana kutumiwa vibaya kwa vigezo vya utii kwa amri za makamanda.
 
Na kuanzia sasa hairuhusiwi kulizungumzia tukio la kifo cha Mwangosi....kesi ipo mahakamani!
Hii kitu ya kumbebesha kijana wa miaka 23 zigo la uovu wa polisi halikubaliki.....
 
Sikubaliani kabisa na kesi hii ni batili, Wanaharakati wote wanapaswa kuipinga hii kesi maana ni kuwafanya Watanzania ni wapumbavu kuliko maelezo.

Daudi-Mwangosi.jpg

Kati ya hao kwenye picha,ni yupi aliyefikishwa mahakamani?
 
Rpc anyogwe jamani mana kama asingetoa maamuzi kuwa auwawe asingeuwawa arpc ni mchawi mkbwa kwanza hata sura tu inaonyesha jamani mbona wanatuumiza mioyo yetu? Dahaa
 
Rpc anyogwe jamani mana kama asingetoa maamuzi kuwa auwawe asingeuwawa arpc ni mchawi mkbwa kwanza hata sura tu inaonyesha jamani mbona wanatuumiza mioyo yetu? Dahaa

Jamani mbona mnachakachua picha ambayo pembeni yake kulikuwa na gari la RPC. Dogo kaonewa RPC ashitakiwe. Waandishi wa habari mpaka leo hii mlitakiwa muwe na jina la mtu aliyetoa amri dogo alipue. Lile gari alikuwepo nani
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom