Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 56,542
- 93,149
September 12, 2012
BREAKING NEWssssssssMTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI AFIKISHWAMAHAKAMANI LEO IRINGA
Askari anayetuhumiwa kumuua Daudi Mwangosi leo amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya mkoa wa Iringa na kusomewa mashitakata yake. Huku akiwa chini ya ulinzi mkali ambao ulifanya wanahabari waliofika mahakamani kujitahid kupata picha kwa ugumu.
Akisoma mashtaka mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya Daines lymo mwendesha mashtaka ameeleza kuwa mtuhumiwa Pacificus Cleophase Simon (23
HABARI KAMILI ITAKUJIA HIVI PUNDE
BREAKING NEWssssssssMTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI AFIKISHWAMAHAKAMANI LEO IRINGA
Askari anayetuhumiwa kumuua Daudi Mwangosi leo amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya mkoa wa Iringa na kusomewa mashitakata yake. Huku akiwa chini ya ulinzi mkali ambao ulifanya wanahabari waliofika mahakamani kujitahid kupata picha kwa ugumu.
Akisoma mashtaka mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya Daines lymo mwendesha mashtaka ameeleza kuwa mtuhumiwa Pacificus Cleophase Simon (23
HABARI KAMILI ITAKUJIA HIVI PUNDE
Yule asikari aliyemuua David mwangosi kafikishwa mahakamani Iringa chini ya ulinzi mkali.
Mshitakiwa huyo katambulika kwa jina la PACIFICUS CLEOPHACE SIMON miaka 23.
MY TAKE.
Inatakiwa wote walikuwepo sehemu ya tukio wafikishwe mahakamani. kwa huyu mmoja kaonewa sababu walikuwa wengi akiwemo aliye mwamulisha. mia
na Mwandishi wetu
ASKARI polisi aliyefyatu bomu lililomlipua na kumuua kinyama mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, David Mwangosi (40), amefikishwa katika mahakama ya kijeshi na kuvuliwa uaskari.
Vile vile, askari huyo mwenye cheo cha PC anatarajiwa kufikishwa
katika mahakama za kiraia kujibu mashitaka yanayomkabili.
Habari kutoka ndani ya jeshi hilo mkoani Iringa zilimtaja askari huyo kuwa ni PC Pacificus Cleophace Simon (23), mwenye namba G2372. Ni askari wa FFU Iringa, na hajafikisha miaka mitatu kazini.
Inaelezwa kuwa askari huyo ambaye anadaiwa kukiri kuua bila kukusudia, ameshakula kiapo cha ungamo mbele ya mlinzi wa amani.
Kufikishwa katika mahakama ya kijeshi kwa askari huyo, kumekuja baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa awali ambao umebaini kuwa bomu alilofyatua ndilo lililosababisha kifo cha Mwangosi.
Kwa mujibu wa habari hizo, askari huyo kwa sasa anashikiliwa na polisi mkoani Iringa na anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya kiraia wakati wowote.
Hata hivyo, habari zaidi zinasema kuwa askari huyo huenda akapanda kizimbani baada ya tume iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema na Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, kukamilisha kazi zao ndani ya siku 30.
Hadi tunakwenda mitamboni, Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Michael Kamhanda na IGP Mwema hawakupatikana kuthibitisha taarifa hizo.
Picha zilizopigwa kwenye tukio la mauaji ya Mwangosi, zilionyesha askari wakiwa wamemzingira na kumpiga, baadhi yao wakiwa na virungu, na wengine bastola. Mmoja miongoni mwao, ameshikilia bunduki na kuielekeza tumboni.
Vile vile, baadhi ya askari wamemtaja mwenzao aliyemlipua Mwangosi, wakataja na mahali anakoishi mjini Iringa.
Askari waliokuwepo siku ya tukio, walilieleza gazeti hili kwa sharti la kutotaja majina yao kwamba aliyemlipua Mwangosi na kumuua papo hapo yuko chini ya ulinzi tangu siku ya tukio akiwa na askari wengine walioonekana wakimpiga mwandishi huyo.
Mwangosi aliuawa Jumapili iliyopita katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi, mkoani Iringa wakati akiripoti habari za ufunguzi wa tawi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), huku polisi wakiwazuia kufanya kazi yao ya kisiasa.
Bomu lililomlipua Mwangosi lilimjeruhi askari polisi aliyetambulika kwa jina la Aceli Mwampamba, aliyekuwa amekumbatiwa na mwandishi huyo wakati akishambuliwa na kundi la polisi.