Mtuhumiwa ma mauaji ya Mwangosi afikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali

hakika vyote watafanya lakini siku zote hukumu hutolewa na mungu sio binadamu kama wanavyofikiri, kwa hiyo wafanye usanii wao lakini chini ya jua hili haki itatendeka kwa wote walihusika na ukatili huu juu ya binadamu mwenzao, mungu tusaidie dua zetu zipokee na uwaangamize wote kwa umoja wao waliohusika na ukatili huu nawasilisha dua zangu kwako..... Amen
 
September 12, 2012

BREAKING NEWssssssssMTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI AFIKISHWAMAHAKAMANI LEO IRINGA




Baadhi ya wanahabari wakitoka mahakamani


Askari anayetuhumiwa kumuua Daudi Mwangosi leo amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya mkoa wa Iringa na kusomewa mashitakata yake. Huku akiwa chini ya ulinzi mkali ambao ulifanya wanahabari waliofika mahakamani kujitahid kupata picha kwa ugumu.

Akisoma mashtaka mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya Daines lymo mwendesha mashtaka ameeleza kuwa mtuhumiwa Pacificus Cleophase Simon (23

HABARI KAMILI ITAKUJIA HIVI PUNDE





Maasikini Cleophasi ur too young to comit that offence......ur future is at stake just coz of silly order.
 
Shahidi wa kwanza ni RPC wa Iringa!

ILEJE ndugu yangu unapotosha ukweli RPC siyo shahidi wa kwanza bali ni mshitakiwa namba moja na huyo aliyepelekwa mahakamani ni aliyepokea amri toka kwa RPC Michael Kamuhanda na akaitekeleza kama utakumbuka vizuri RPC alifuatwa ili amuokoe marehemu Mwangosi lakini alikataa kwa kuwa alikuwa ameshamhukumu kifo toka ukumbini alipokuwa anamuuliza maswali yaliyomshinda kuyajibu, na ili asitoe siri nyingi huyo kijana naye utashangaa anakufa hukohuko mahabusu uzoefu unaonyesha hivyo rejea kesi ya ACP ZOMBE
 
Sasa msiliongelee tena hili swala maana lipo mahakamani
swali
iweje ifikishwe mahakamani hata uchunguzi haujakwisha? Je kulikuwa na haja ya kuwa na kamati ya uchunguzi?
 
Ndugu zangu wanajamvi. Sidhani sana kama mahali hapa ni salama. Naomba ndugu wa karibu na huyu muuaji mtoto cleophas aongee na Cleophas na amshauri awe makinin na mkweli kwa Mungu kwa sababu hata yeye hana uhakika na maisha yake. Historia imethibitisha hivyo.



Maasikini Cleophasi ur too young to comit that offence......ur future is at stake just coz of silly order.
 
Haya sasa nyie askari inapokea amri hata ikiwa ya kipuuzi yamemkuta huyu mwenzenu,lakn nataka aanze huyu RPC Kamuhunda maana bwana mdogo kapewa order je mtoa order mbona yupo yupo tuu mtaani? au hiyo tuloambiwa huyu bwana analindwa ili astaafu vzr?
 
washtakiwe wote hao wanane walimzunguka. wameshiriki kumuua, walienda kumuua tu huyu mwandishi wa habari na wala siyo kutuliza ghasia. Kama askari wanane pamoja na askari kanzu wana kuwa na mtu mmoja tu halafu useme kulikuwa na fujo hapo? Kichaa cha mbwa kabisa!
 
Hao askari wengine watano ukiacha huyo muuaji hawataingizwa hatiani kwa sababu ya huyo RPC, ukiwaingiza hao hatiani ni kwamba hata RPC ataingia hatiani automatically kitu ambacho hakikubaliki na serikali hii dhalimu. Utawala wa sheria Tanzania bado ni ndoto za alinacha.
 
Yule askari polisi mtuhumiwa wa mauaji ya mwangosi,amepelekwa leo mahakamani kwa VX,Tofautina watuhumiwa wengine.nawasilisha.Source ITV.
 
Katika taarifa ya habari wameonesha jamaa ambaye anatuhumiwa kumuua mtangazaji wa chanel ten DAVID MWANGOSI, amefikishwa mahakamani.

Kwa watu ambao wamechunguza kwa makini wakati jamaa akipelekwa kusomewa mashtaka alikuwa amezungukwa na maaskari wengi huku akiwa amezibwa sura asifahamike wala aschukuliwe pcha,UNAJUA HII INA TAFSIRI GANI?

Wamefanya kumfikisha mahakamani ili kuwaridhsha watu ambao wamepga kelele nyingi awajbishwe ila ataachiwa huru kwani hakuna mtu yeyote ambaye atakuwa anamfaham kwa sura.HII NI DANGANYA TOTO KWA WATU WAZIMA. MBAAYAAA
 
siyo yale mazingaombwe ya kuchukua mahabusu na kuwageuza watekaji wa dr. Uli?
wewe ndiye umesema, sasa kwanini wamfiche kama ni mtuhumiwa wa kweli hayo ni maagizo hakuna cha mtuhumiwa hapo na ndiyo mwisho wa kesi upelelezi utaendelea hadi march 2056
 
hii ndo tanzania,anakuwa charged with manslaughter,kweli??that is right away first degree murder..
 
Huyu ni kafara. Walioua ni CCM, Kikwete, Nchimbi na Mwema. Wao ndiyo waliotoa amri kwa polisi kwenda kuvuruga mikutano ya CDM. Hakuna haja ya kumnyonga mbwa wakati aliyemfuga na kumtuma yupo. Heri polisi wengine wangejifunza kuwa wanatumiwa kisiasa na kula njama ya kukataa upuuzi huu.
 
Yule sio mhusika kabisa. Maswali nnayojiuliza.

1. Kwann ameficha sura
2. Kwann Polisi wamezuia asipigwe picha.
3. Lile VX lililompeleka Mahakamani ni la nani.
4. Kwann Polisi wamevaa kiraia woote.

Hili changa la macho kama ilivyo kwa Ulimboka.
 
Katika taarifa ya habari wameonesha jamaa ambaye anatuhumiwa kumuua mtangazaji wa chanel ten DAVID MWANGOSI,Amefikishwa mahakamani.kwa watu ambao wamechunguza kwa makini wakati jamaa akipelekwa kusomewa mashtaka alikuwa amezungukwa na maaskari wengi huku akiwa amezibwa sura asifahamike wala aschukuliwe pcha,UNAJUA HII INA TAFSIRI GANI?,wamefanya kumfikisha mahakamani ili kuwaridhsha watu ambao wamepga kelele nyingi awajbishwe ila ataachiwa huru kwani hakuna mtu yeyote ambaye atakuwa anamfaham kwa sura.HII NI DANGANYA TOTO KWA WATU WAZIMA.MBAAYAAA

Lengo ni kuhakikisha swala hili linauawa kwa mtindo wa liko mahakamani, hivyo no maandamano, no hotuba, no what, liko mahakamani.
 
Back
Top Bottom