Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,503
- 113,614
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, nipatapo fursa, hupita huku na kule na kubadilishana mawazo na watu mbalimbali wa kada tofauti. Kwa takriban siku 3 zilizopita, nimepata fursa ya kutembelea mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambayo ndiyo inayo dorminate Kanda ya Kaskazini, kiukweli pande hizi CCM ina hali mbaya sana, huku CCM Imechokwa sana mpaka basi!.
Kama CCM Imechokwa, Mbona Bado Inachaguliwa na Inaendelea Kushinda?
Siku zote nimekuwa nikisema humu, kuwa kuna baadhi ya maeneo CCM imechokwa ila bado CCM imekuwa ikichaguliwa na wengi sio kwa sababu ya kupendwa au kukubalika au kuleta maendeleo, hapana!, CCM imekuwa ikichaguliwa na wengi kwa sababu ya mazoea tuu kutokana na CCM ndicho chama pekee kilichotapakaa nchi nzima, hivyo wengi wakiichagua CCM kwa sababu ndicho chama pekee kilichopo maeneo yao walichokifahamu tangu wamezaliwa, na wengine wakikichagua CCM kama asante ya kutuletea uhuru kupitia TANU, na idadi kubwa ya walio vijijini, wamekuwa wakiichagua CCM ama kwa uwepo wake pekee, ana kwa ignorance tuu ya elimu ya uraia!. Sasa wale wanaoichagua CCM kwa mazoea tuu kama asante ya kutupatia uhuru, kwa sasa ni oldguards, wamezeeka, wanazidi kupungua na wachache waliobakia their days are numbered!. Wale wengi waliokuwa wakiichagua CCM kwa ignorance, sasa wameanza kuerevuka na wameanza kuamka!, moja ya maeneo ambayo watu wameamka ni Kanda ya Kaskazini.
Tabia za Maeneo ya Stronghold za CCM na Stronghold za Opposition.
Stronghold ni eneo lenye nguvu ya chama fulani. Mfano CUF Stronghold yake ni Pemba, karata yake ni udini, Chadema Stronghold yake ni Kanda ya Kaskazini na maeneo ya mijini kwenye miji mikubwa karata yake ni utajiri wa kiuchumi, CCM inamiliki maeneo mengine yote kwa karata yake ya chama cha wanyonge, chama cha wakulima na wafanyakazi.
Tabia za maeneo wanayochagua wapinzani, ni maeneo yenye afueni za kiuchumi hivyo yana maendeleo, watu wake wanajiweza kidogo kiuchumi hivyo wamesoma na kuelimika, hawawezi kudanganyika kirahisi rahisi. Kanda ya Kaskazini, ndio inayoongoza kwa high literacy levels ikifuatiwa na Bukoba, Mbeya Mwanza na Iringa, majiji yote makubwa, yameshikwa na upinzani sababu watu wa mijini wana nguvu ya kiuchumi hivyo wameelimika na kufuta ujinga hivyo wamechagua upinzani. Hii inamaana kwa kadri Watanzania wengi wanavyozidi kuelimika na kufuta ujinga, ndivyo upinzani utakavyo zidi ku gain momentum na kugain grounds.
Maeneo ya Stronghold ya CCM, ni maeneo yote yenye umasikini uliotope na low literacy levels, hivyo ni rahisi kudanganyika na kuna wanaoichagua bila kujua wanachagua nini!. Hivyo CCM itazidi kuchaguliwa kwa kupata ushindi wa jumla as long as ujinga na umasikini uliotopea utaendelea.
Majaaliwa ya CCM Kanda ya Kaskazini
Kwa mujibu wa kada mbalimbali za wale niliozungumza nao, wamenithibitisha pasi shaka kuwa hakuna jinsi yotote wagombea wa CCM wa Kanda hii Kaskazini kama Ole Sendeka, Ole Medeye na Ole Nang'uro Ole Milya etc wataweza kusalimika, sehemu pekee salama mpaka sasa kwa CCM kwenye Kanda ya Kaskazini mpaka sasa ni Jimbo la Monduli tuu kwa sababu ya Lowassa!, na maeneo ya Tanga na upareni nako CCM bado ni salama kwa sababu ya umasikini uliotopea, lakini kungine kote, Kanda ya Kaskazini, CCM haina chake, CCM haipati kitu!.
Kama kasi ya upepo wa mwamko kama huu wa Kanda ya Kaskazini kuichukia CCM, utaingia kanda ya Ziwa kwa kasi hiyo hiyo, then amini usiamini, hakuna jinsi yoyote ya kuiokoa CCM isipigwe mwereka uchaguzi wa 2015, CCM inakwenda kupigwa chini!.
CCM Hili Wanalijua, Jee Itajikalia Tuu Kusubiria Kifo?.
Kwa vile hili CCM pia wanalijua, mtashuhudia juhudi za ziada kwa CCM kuelekeza nguvu nyingi na nguvu kubwa ya ziada kwenye kanda hii ya Kaskazini ili destabilize upinzani, na hata ikibidi kutumia ile 'universal language' ya "penye uzia penyeza rupia", then rupia zinaweza kupenyezwa!.
Kufuatia Kanda ya Kaskazini kuwa ni stronghold ya opposition na sasa kwenye Kanda ya Ziwa tayari kuna majimbo matatu yako chini ya Chadema, kama Chadema itaendelea kuyashikilia na kuongeza kasi ya Chadema kukubalika na kupendwa kanda ya Ziwa, kama ilivyokubalika Kanda ya Kaskazini, kiukweli kabisa, hiki ndio kitakuwa kifo na kaburi la kuizika CCM!. Hali hii itakuwa inaiweka CCM katika hali mbaya sana kisiasa na kuwa kwenye wakati mgumu kuwahi kutokea kwasababu Kanda ya Ziwa ndio Kanda determinant ya nani anakuwa rais wa Tanzania. Swali linabaki ni Jee CCM itakubali hili litokee?. CCM itakubali kujikalia tuu na kujiangalia kusubiria kifo wakati inakwenda machinjioni?, itakubali kufa kibudu ama ita kukuruka na kufurukuta kujitetea?.
Determinant ya Rais wa Tanzania ni Kanda ya Ziwa.
Determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii, ni wapiga kura wa Kanda ya Ziwa ambayo ndiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya watu!. Kati ya watu milioni 40 wa sensa ya mwaka 2002 kwa Tanzania yenye makabila 120, Wasukuma peke yao wako milioni 8 na Kanda ya Ziwa ina theluthi moja ya kura za urais!. Sasa ukiwajumlisha na Kanda ya Kaskazini, hata kama mikoa yote iliyobakia wataipigia kura CCM, bado kwa kanda hizo mbili pekee, zinatosha kabisa kuipiga chini CCM!, hivyo CCM kwa kulitambua hili, itatumia nguvu yake yote, all its mighty powers by all means, by hooks and crooks kuyakomboa majimbo haya matatu ya Kanda ya Ziwa, na naomba mshishangae, kama ili kujiokoa, uchaguzi mkuu wa 2015, CCM inaweza kabisa kutafuta mgombea wa urais kutoka kanda hii ya Ziwa ili kujiokoa kwa kuwahonga watu wa kanda ya Ziwa kwa hongo kubwa kabisa ya mgombea urais, hiyo watu kama John Pombe Magufuli, Andrew Chenge, Laurent Masha, William Ngeleja, Charles Kitwanga, are men to watch very closely!, hata kama mgombea huyo atakuwa hana sifa za kutosha kuwa rais bora, kwa CCM iko tayari kutupatia bora rais as long as atatoka Kanda ya Ziwa kuliko kuanguka huku inajiangalia!, kwa CCM kinachotakiwa ni ushindi na sio sifa za mgombea!, kwao, the end justifies the means!.
Mwelekeo huu ni uthibitisho kuwa ule ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania, sio ndoto tena, ni kitu ambacho kinawezekana kabisa kutokea kama upinzani utajitambua kwa kushikilia kwa makini kile kilicho mkononi na kuongeza juhudi za kuimililki kanda ya Ziwa, hivyo vita kuu ya kisiasa nchini Tanzania kuelekea 2015 ni nani ataimiliki Kanda ya Ziwa. Chadema ikifanikiwa, CCM inapigwa chini nzima nzima mazima!, ila CCM ikifanikiwa kuikomboa Kanda ya Ziwa, then 2015 ni CCM tena, na kitakacho fuatia kwa CCM post 2015 ni kuikomboa Kanda ya Kaskazini kwenye uchaguzi wa 2020, na kusema ukweli hii ndio itakuwa kazi ngumu kweli kweli, ila kama itatumika ile 'universal language', ya "penye uzia...", kuna msemo "hakuna mkate mgumu mbele ya chai", mkate hata uwe mgumu vipi ukiuchovya ndani ya chai, unalainika!".
Tuache Siasa za Ukanda na Ukabila, au Tuzidumishe Ili Mtu wa Kanda/Kabila Yetu Ndie Ashinde?.
Natoa mwito kwa Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu, tusiendekeze hizi siasa za Ukanda, zitajenga chuki za kukichukia chama fulani bila sababu za msingi ya chuki hiyo, au kukipenda na kukishabikia chama fulani kwa upenzi tuu, matokeo ya mwisho ya siasa hizi ni kujengeana chuki zisizo na sababu!. Tupingane bila kupigana, tutofautiane kisiasa bila kuchukiana bali tupingane kwa hoja huku tukipendana!.
Hata mimi uchaguzi wa Arumeru, nilisimama na Sioi, tumekutana na Nasari pale Bungeni Dodoma, tumekumbatiana, na kiukweli kutoka moyoni mwangu, sina chuki na Nasari, namkubali sana tuu kwa dhati na kupongeza kwa ushindi, huku nikiendelea kushikamana na Sioi kwa sababu ni rafiki!.
Wito Kwa Watu wa Kanda ya Kaskazini
Wito wangu kwa nyie watu wa Kanda ya Kaskazini, Kanda yenu ndio imependelewa sana, inaongoza kwa mashule na wasomi, inaongoza kwa mahospitali!, KCMC, Mawenzi, Kibongoto, Mt. Meru, Seliani, Dareda, etc, Inaongoza kwa vivutio vya utalii, Mt. Kilimanjaro, Mt. Meru, Serengeti, Ngorongoro, Seronera, Manyara, Inaongoza kwa barabara za lami hadi vijijini, inaongoza kwa umeme vijijini, inaongoza kwa maendeleo, inaongoza kwa kutoa wanawake wife material, ukioa mchagga umeoa maendeleo!, hivyo msiichukie hivyo CCM, kwani pamoja na mabaya yake yote ya CCM, kulea rushwa na ufisadi na kutuletea umasikini na kulea ujinga kwa kuutumia kama mtaji wake wa ushindi, pia kuna mema na mazuri yake mengi ambayo CCM imelifanyia taifa hili ikiwemo kutuletea maendeleo japo kiduchu, lakini pia imetuletea hazina ya amani na utulivu ambazo ni tunu kubwa kuliko maendeleo, hivyo tuichukie CCM kwa mabaya yake na kupenda kwa mema na mazuri yake!.
Wito Kwa Wa Kanda ya Ziwa.
Tusikubali kutumiwa kama ngazi ya wengine kupandia kisiasa, kwa vile na mimi ni mtu wa Kanda hii na sisi ndio determinant ya nani anashinda na kukikalia kile kiti cha ikulu yetu, tusikubali kuendelea kutumika tuu kama ngazi kwa wengine kupandia, au kuendelea kuwa na upendo wa mshumaa kumulikia wengine huku kwetu kunateketea, Kanda hii ndio Kanda yenye watu wengi, ndio Kanda yenye mijitu yenye nguvu inayokula na kushiba, ndio Kanda tajiri kuliko Kanda zote, ndio yenye madini ya dhahabu na almasi, ndio wenye Ziwa Victoria lenye samaki watamu Sato, tusikubali kutumiwa kama dodoki kuwasafishia wengine au dekio baada ya deki linatupwa kule, sisi tuna kila aina ya utajiri lakini very unfortunately watu wetu ni masikini wa kutupwa!. Angalia wenzetu wa Kaskazini mbona wameweza kulibwaga hili lidubwana na wanapata maendeleo, na sisi tuamue kulibwaga unless kama 2015 mpeperusha bendera wao, atakuwa ni mmoja wetu!.
Namalizia kwa kusisitiza, huu ni mtazamo tuu!
Wasalaam.
Paskali
Kirua Vunjo, Moshi Vijijini
Rejea
Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni ...
Tuhuma Za Ukabila: Wasukuma Sii Miongoni Mwa Makabila Yenye ...
Ni upuuzi kuwagawa watanzania kikanda,kikabila na kidini ...
Ni kweli kuna makabila yasiyotakiwa kutoa rais wa nchi? | Page 7 ...
Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini! | Page 42 ...