Mambo ya Ukanda yaliasisiwa Kaskazini na yameenda kuota mizizi Ziwa Victoria. Walaumiwe sana CHADEMA!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,028
Waasisi wa mambo ya Ukanda ni Chadema ambao walijikita kanda ya Kaskazini hasa Uchaggani na Arusha

Baadae Ukanda ukahamia Pwani ya Tanga hadi Mtwara

Sasa Ukanda umeota Mizizi Ziwa Victoria ukichombezwa zaidi na CCM

Wasiwasi wangu Kanda ya Ziwa ndio watakuwa wanaamua Nani awe Rais wa JMT kuanzia kwenye NEC ya CCM

Nawatakia Dominica Njema 😀

cc: Pambalu, Wenje, Dr Mashinji
 
Population yao inawaruhusu. Watu wakishakuwa wengi katika nchi, mkifuata demkorasia watawaamulia sana viongozi wa kisiasa. Kanda ya ziwa nao wamejua umuhimu wa kuja pamoja. Walikuwa hawajui. Wameonja sasa umuhimu wa kuwa na umoja. Waliona wanapuuzwa, wakaamua kutumia uwingi wao.
Labda wasiwe na mgombea ndani ya NEC.
 
Wasiendekeze ukanda bila kutumia akili nyingi na kutazama mustakabali wa taifa.Wakikengeuka hayo wataleta viongozi vichaa na wajinga halafu wao nao wamuabudu kama "Che Guavara" wa kisiwa cha Honolulu!
 
Waasisi wa mambo ya Ukanda ni Chadema ambao walijikita kanda ya Kaskazini hasa Uchaggani na Arusha

Baadae Ukanda ukahamia Pwani ya Tanga hadi Mtwara

Sasa Ukanda umeota Mizizi Ziwa Victoria ukichombezwa zaidi na CCM

Wasiwasi wangu Kanda ya Ziwa ndio watakuwa wanaamua Nani awe Rais wa JMT kuanzia kwenye NEC ya CCM

Nawatakia Dominica Njema 😀

cc: Pambalu, Wenje, Dr Mashinji
Tz wananchi hawaamui nani awe Rais mnaamuliwa na wote mnafuata tu
 
M
Population yao inawaruhusu. Watu wakishakuwa wengi katika nchi, mkifuata demkorasia watawaamulia sana viongozi wa kisiasa. Kanda ya ziwa nao wamejua umuhimu wa kuja pamoja. Walikuwa hawajui. Wameonja sasa umuhimu wa kuwa na umoja. Waliona wanapuuzwa, wakaamua kutumia uwingi wao.
Labda wasiwe na mgombea ndani ya NEC.
Mkuu,umesema vizuri hasa hapo kwenye wingi na maamuzi. Sasa nina swali dogo kwako mkuu;

Je,ni kusudio kuu la serikali ya CCM kuweka siasa mpaka kwenye elimu ili waandae na kupata wajinga wengi ambao baadae kwa wingi wao watuamrie na kutuchagulia viongozi wajinga kutoka kwenye kundi lao?
Asante mkuu.
 
Leta kwanza ushahidi tujue kama kwenye elimu kuna siasa. Isitoshe, hii ni mada tofauti.
 
Tz wananchi hawaamui nani awe Rais mnaamuliwa na wote mnafuata tu
Pia ungewauliza swali dogo tuu, raisi wa sasa anatokea wapi? Mnaweza kuwa wengi kwenye kura ila Mungu akaamua kuwapa wale wachache. Waarabu ni wengi sana, ila Muisrael anawaamulia hadi wanapoteana. Muisrael wa nchi yetu unamjua?
 
Waasisi wa mambo ya Ukanda ni Chadema ambao walijikita kanda ya Kaskazini hasa Uchaggani na Arusha

Baadae Ukanda ukahamia Pwani ya Tanga hadi Mtwara

Sasa Ukanda umeota Mizizi Ziwa Victoria ukichombezwa zaidi na CCM

Wasiwasi wangu Kanda ya Ziwa ndio watakuwa wanaamua Nani awe Rais wa JMT kuanzia kwenye NEC ya CCM

Nawatakia Dominica Njema 😀

cc: Pambalu, Wenje, Dr Mashinji
Siasa za uwoga ndio hupelekea watu waanze kutafuta kukubalika kwa Kanda.Nauona udhaifu huo kwa sasa uwingi wa watu wa Kanda ya ziwa sio kigezo Cha kupata viongozi Bora na Wala sio turufu ya kisiasa ni vile tumekuwa na viongozi wanaoanza kuusahau sahau misingi ya kiuongozi iliyowekwa na ambayo imelillinda taifa
 
Population yao inawaruhusu. Watu wakishakuwa wengi katika nchi, mkifuata demkorasia watawaamulia sana viongozi wa kisiasa. Kanda ya ziwa nao wamejua umuhimu wa kuja pamoja. Walikuwa hawajui. Wameonja sasa umuhimu wa kuwa na umoja. Waliona wanapuuzwa, wakaamua kutumia uwingi wao.
Labda wasiwe na mgombea ndani ya NEC.
Wako wengi kivipi?
Tanzania tuko wangapi na wao wako wangapi?

Huu ujinga mnautoaga wapi?
 
Waasisi wa mambo ya Ukanda ni Chadema ambao walijikita kanda ya Kaskazini hasa Uchaggani na Arusha

Baadae Ukanda ukahamia Pwani ya Tanga hadi Mtwara

Sasa Ukanda umeota Mizizi Ziwa Victoria ukichombezwa zaidi na CCM

Wasiwasi wangu Kanda ya Ziwa ndio watakuwa wanaamua Nani awe Rais wa JMT kuanzia kwenye NEC ya CCM

Nawatakia Dominica Njema 😀

cc: Pambalu, Wenje, Dr Mashinji
Kimsingi siasa za makundi na ukanda wameziasisi CCM kwa faida zao za muda mfupi bila kuona madhara ya jambo hilo kwa Taifa in a long run. Sasa mbegu hiyo imeshaota na imekomaa ndani ya hicho chama. Mfano mzuri ni hili la Makonda na sukuma gang, Kimaadili huyu Makonda hakustahili kupewa nafasi ya inayobeba image ya Chama au serikali kutokana na yale aliyowatendea watu huko nyuma hata kama yalikuwa na baraka ya mfumo. Inaonekana wenye mamalaka wameamua kucheza karata ya kuwateka kanda ya ziwa kwa kutumia mtu asiye na maadili huku ndani ya chama na serikali unaona kabisa kuna viongozi wengine wakiwa wapo kwenye mshangao kwa yanayoendelea (maana utadhani kuna vyama viwili ndani ya chama kimoja).
Katika hili linaloendelea, mwenyekiti anajisikia kuwa na utulivu katika nafasi yake kama kiongozi nchi (japo itakuwa kwa muda mfupi tu) kwasababu Bashite anawakeep busy Watanzania na matukio yake ya kikomedikomedi kitu ambacho huoni kama kuna sustainability wala harmonisation ya kiuongozi katika chama na serikali pia. Na msipoangalia kwa jicho la kiintelejensia hii kanda itasumbua taifa huko mbeleni. Kwa behaviour zao wanaweza hata kugawa nchi japo hili linaweza lisionekane kwa sasa. Au wanaweza kumeguka na kusapoti chama kingine vilevile kwa kuwa sasa hivi Taifa letu limeacha miiko na misingi ya uongozi bali unaweza kufanya vyovyote ili uwe kiongozi.
 
Kanda ya ziwa kuna Population kubwa ya watu, ikichochewa na Wasukuma. Wasukuma ndio kabila lenye idadi kubwa ya Watu kuliko makabila yote Tanzania.

Hiyo ya Makonda ni mission au mbinu ya kwenda kuchota Kura za mama samia mwaka 2025. Tuliosoma Cuba hii mbinu tunaijua. Lakini kwa sababu wewe ni zwazwa unaona ni ukanda. CCM haijawahi kuwa na ukanda hata siku moja, wale jamaa wana mipango buku jero.

Baada ya Magufuli kufariki, CCM walipata shida sana kanda ya ziwa na wasukuma wengi wakaanza kupoteza Imani na CCM. Na CCM walilijua hilo wakaangalia nani anayeweza kurudisha Imani ya CCM kanda ya ziwa. Kutizama Mafaili wakaona Makonda ndio anayeweza kuvaa hivyo viatu.

Hii anayoifanya Makonda, ni kuwateka Wasukuma na makabila ya ukanda huo, kuwarudisha CCM. Hizi ni mbinu za kivita, zinatumiwa sana hata na mataifa makubwa Duniani kupata kura za Veto kwenye Umoja wa mataifa. Ndio maana unaona Africa inatembelewa sana na viongozi wa kibeberu kutoka kila kona ya Dunia. Unaweza hisi ni ukanda kumbe ni mbinu.

CHADEMA wanafeli kwa sababu hawajui kucheza na takwimu, hawajuhi kupiga kwenye mshono. Kipindi Magufuli anafariki walitakiwa kuweka efforts kubwa kanda ya ziwa ili kuwanyakuwa wasukuma ambao walianza kupoteza Imani na CCM, kampeni za Chadema zote baada ya Magufuli kufariki zingeelekezwa Kanda ya ziwa wangepiga kwenye mshono, kwa sababu Kanda ya ziwa ina Idadi kubwa sana ya Raia. Na huku ndiko kura zilipo, na sio huko Dar es salaam au Arusha
 
Waasisi wa mambo ya Ukanda ni Chadema ambao walijikita kanda ya Kaskazini hasa Uchaggani na Arusha

Baadae Ukanda ukahamia Pwani ya Tanga hadi Mtwara

Sasa Ukanda umeota Mizizi Ziwa Victoria ukichombezwa zaidi na CCM

Wasiwasi wangu Kanda ya Ziwa ndio watakuwa wanaamua Nani awe Rais wa JMT kuanzia kwenye NEC ya CCM

Nawatakia Dominica Njema 😀

cc: Pambalu, Wenje, Dr Mashinji
Mambo ya ukanda kiini chake ni siasa za mtandao, zilizombagua Salim Ahmed Salim asigombee urais mwaka 2005. Kikwete na kundi lake ndio walioingiza huo ushenzi wa siasa za kiswahili za kuunda kundi kubwa la mtandao ndani ya CCM.

Yeye alikuwa mwanafunzi wa siasa za uungwana za Mwalimu Nyerere aliyemlea kisiasa lakini malipo yake akaanzisha siasa za usisi na unyinyi ndani ya CCM.

Chadema tunapenda sana kuwanyooshea kidole kwa matatizo yaliyo ndani ya CCM yenyewe.
 
Waasisi wa mambo ya Ukanda ni Chadema ambao walijikita kanda ya Kaskazini hasa Uchaggani na Arusha

Baadae Ukanda ukahamia Pwani ya Tanga hadi Mtwara

Sasa Ukanda umeota Mizizi Ziwa Victoria ukichombezwa zaidi na CCM

Wasiwasi wangu Kanda ya Ziwa ndio watakuwa wanaamua Nani awe Rais wa JMT kuanzia kwenye NEC ya CCM

Nawatakia Dominica Njema

cc: Pambalu, Wenje, Dr Mashinji
Mbowe na Lisu wana laana ya kushangilia kifo cha Magufuli
 
..kuna namna mbalimbali za ku-counterpunch mikakati ya CCM ktk kanda ya ziwa.

..ukichukua kanda ya ziwa kuwa ni mikoa ya Geita, Mwanza, Simiyu, na Shinyanga, unapata jumla ya watu milioni 11,059,276.

..wapinzani wanaweza kujikita ktk mikoa ya D'Salaam, Morogoro, Arusha, na Mbeya, ambapo idadi ya watu ni milioni 13,280,841.

..mkoa wa D'Salaam peke yake una idadi ya watu milioni 5,388, 728. kwa hiyo ni mkoa muhimu sana kwa wapinzani kuhakikisha wanapata kura nyingi. tatizo la mkoa wa D'Salaam ni idadi ndogo ya majimbo ukilinganisha na huko kwingine.

..Data zangu nimezitoa ktk chanzo hiki hapa chini.

cc Erythrocyte , Nguruvi3, Mhaya, Lord denning
 
Kanda ya ziwa ina mikoa ifuatayo:-
1. Mwanza
2. Mara
3. Kagera
4. Geita
5. Simiyu
6. Shinyanga.

Kwenye hesabu zako jumlisha na idadi ya watu wa mikoa ya Mara na Kagera ambayo hujaiweka hapo halafu linganisha idadi yake na mikoa uliyoitaja ya Dar, Mbeya, Morogoro, na Arusha.

Kumbuka vyama vya sias wakienda kufanya kampeni kanda ya ziwa wanatembelea mikoa yote niliyotaja hapo juu na wanakuwa na kauli mbiu moja.

Pia watu wa Kanda ya ziwa wametapakaa katika mikoa ya Tabora, Rukwa, Katavi, Morogoro na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Mbeya.

Taarifa zinaenea haraka, kama ukiwaweza watu wa Kanda ya ziwa, basi na watu wa Tabora, Rukwa, Katavi, Morogoro na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Mbeya utakuwa umewaweza.
 
Wasiwasi wangu Kanda ya Ziwa ndio watakuwa wanaamua Nani awe Rais wa JMT kuanzia kwenye NEC ya CCM
Mkuu Yohana Mbatizaji, johnthebaptist , usiwe na wasiwasi kabisa kuhusu Kanda ya Ziwa, ni Kanda determinant kwa sababu ndio inapiga kura inayoitwa a decisive votes kutokana na hii ndio Kanda kubwa zaidi na yenye idadi kubwa ya wapiga kura.

Hili la ukanda angalia sisi hili tuliliona lini Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni Dhana Tuu?." na tukashauri nini!.

Saa hizi ndio wenzetu mnaliona, na baada ya Samia, akiisha ingia mwingine, ndio lile jingine la akiwa Mkristo ni lazima awe... ndilo nalo mtaliona!.

P
 
Waasisi wa mambo ya Ukanda ni Chadema ambao walijikita kanda ya Kaskazini hasa Uchaggani na Arusha

Baadae Ukanda ukahamia Pwani ya Tanga hadi Mtwara

Sasa Ukanda umeota Mizizi Ziwa Victoria ukichombezwa zaidi na CCM

Wasiwasi wangu Kanda ya Ziwa ndio watakuwa wanaamua Nani awe Rais wa JMT kuanzia kwenye NEC ya CCM

Nawatakia Dominica Njema 😀

cc: Pambalu, Wenje, Dr Mashinji
We huna akili, kaskazini hawana ukanda wowote wala ziwa, ni Pwani na Zanzibar ndiyo wana udini
 
Back
Top Bottom