Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!

Hii taarifa ya PASCO ina mtego sana huyu pasco si mwema kwa Makamanda kwani anabagua kanda kitu ambacho kwa cc wadanganyika kamwe tusikukubali
 
I am sorry to say this, you seem to be discriminatory. You think change can came as a result of dividing this country into sections of tribes and regions. I am not sure which political party stands for such dirty politics as you've displayed in your thread. At no single time in history of our country we have ever conducted any census categorizing people according to their tribes. The lake zone as you have put in your thread is inhabited by a large number of tribes, probably the only country section lived by a more diverse community than any other part of our country. To say that Sukumas are 6 million is a skewed opinion made purposely to propagate your tribalistic thinking. I will be very sorry if there is any political party sympathizing with such politically corrupt inclinations nor strategies to effect change in this country by dividing it on tribal sections. Any political party thinking this way will be hastening its demise.

True political change in this country will only came through independent voters (who are more in numbers than a total sum of all citizens with membership in the existing political parties). These are people who sway instantaneously, they are strongly influenced by current issues and reality on the ground during the material time. These include the young and elderlies, men and women of all classes and ages from all geographical areas of this country. Many who voted in the recent by-election were elderlies and the opposition side won. So discriminating our population on bases of gender, age, etc. is immaterial. If a political party lacks support in certain sections of the country the reason isn't because of the predominant age or tribe residing there. Rather it may be due to the fact that the political party in question hasn't done its homework there. Ref to the Chadema Operation Sangara in Lake zone prior to 2010 election. Such and other more creative strategies will improve voters/civic education. We need to see more of that rather than your cheap tribal sentiments you have put across.

We jamaa wewe dah...
Hiyo Lugha mi siipendi kama nini.
 
Pasco hayo unayoyaona yanachagizwa na tamko la UVCCM la Pwani kuwa rais hatatoka Kaskazini. Kanda ya Kaskazini ni kama wanasema ngoja tuone, usije shangaa madiwani wengi kama si wote wa Arusha, Kilimanjaro na Manyara kuisusa CCM.
Mtazamo wangu ni kuwa hatakama tangazo hilo lililotolewa na UVCCM Mkoa wa Pwani liliwakera lakini hao ndugu zetu hawajaonyesha uvumilivu hebu angalia toka tumepata uhuru nchi hii Mikoa hiyo miwili Arusha na Kilimanjaro imetoa Mawaziri Wakuu 4 tena katika Jimbo moja tu wametoka 2,Marehemu Edward Sokoine na Edward Lowasa, Frederick Sumaye katoka Manyara lakini bado ilikuwa sehemu ya Arusha na David Msuya katoka Kilimanjaro tena huyu Msuya alitoa kauli za kebehi kwenye Bunge lakini hao ndugu zake hawakumkemea kwa kuwa alikuwa wa kwao hivi mbona sehemu nyingine katika Tanzania watu walikuwa watulivu? Madaraka katika Nchi hii ni ya kugawana wao hawana hati miliki na uongozi pekee yao wasituchafulie hali ya hewa!
 
Leo Pasco nadhani ulitulia wakati unazipanga point zako,
Uchambuzi wako ni makini na ninakubaliana na wewe licha ya uswahiba wako na Lowasa sidhani kama umemdefend kuhusu jimbo la Monduli ni kweli Lowasa pale amejenga mizizi na ni yeye ndiye mwenye ushawishi mkubwa wa kumu endorse next Mp kama yeye Lowasa hatogombea tena ubunge

Kuhusu CCM kuchokwa hili wala halihitaji uwe Political Analyst na uzuri wake hata viongozi waandamizi wanalifahamu hili na ndio maana sasa chama kinajiendesha katika mfumo wa Auto Pilot.

Nikiangalia kuhusu kanda ya , Hii mikoa ya Mara, Shinyanga na Mara hapa somo limeshaeleweka na hasa watu wa Mara wala hawahitaji hamasa maana wao walishaamuwa siku nyingi kwamba CCM sas basi.

Katika kanda ya Ziwa sehemu ambayo nadhani inapaswa kufanyika kazi ya ziada ni mkoa wa Tabora, hawa wanyamwezi hata siwaelewi elewi akili zao zimekaaje!!

Ukija mkoa wa Kagera hapa napo somo limeeleweka ila bado kuna kazi inatakiwa kufanyika, mfano hai ni Jimbo la Bukoba Mjini matokeo ya Urais aliongoza Dr Slaa, lakini Ubunge akashinda wa CCM Balozi Kagasheki, kwa maono yangu Chadema inaweza kuscore vizuri sana kanda ya ziwa next Election.

Tatizo lililopo mpaka sasa hivi ni huu ukanda wa umakondeni na uzaramoni, huku ndiko kunapaswa kuwaweka sawa wazawa wa maeneo hayo hili waunge mkono na mbaya zaidi CUF hizi ndio ngome zake, maana hakuna siri kwamba sehemu hizo wanaamini kabisa kwamba CUF ni chama cha waislamu na jamii kubwa ni waislamu katika hayo maeneo.

Sasa jamani ktk mkoa wa Shinyanga, kuna jimbo Moja tu ambalo inabidi kweli sisi wana harakati na wale tunao toka maeneo ya usukumani tuwaelishe wazee wetu, jimbo la SOLWA linaloongozwa na CCM, kule wazee hawajui kabisa ni nini kinachoendelea na wao wanaambiwa ukichagua mageuzi kutatokea vita, tofauti na vijana, ila wazee na akina mama msasa zaidi unahitajika. CCM ni jimbo moja tu hilo ambalo wanajivunia. Ila kwa sasa kuna kijana mdogo wetu na mwenye elimu kubwa tayari alishaanza harakati za kuelimisha pamoja na kufungua matwi mengi ya CDM kila kona ya hilo jimbo. Ameanza na Mungu na atamaliza na Mungu
 
Mkuu Pasco tuko pamoja kwa hilo ila umekosea kitu kimoja hata kule kusini M4C ni kubwa mno sema CDM waliibiwa kura mno!!!but am sure kuna mabadiliko makubwa ya ajaabu,time ll tell
 
wanaichukia ccm kwa sababu tanzania inarudi nyuma -ve development.eg mtoto kafaulu darasa la 7 hajui reading,writting
Katika mambo mabaya ya ccm yanayoniudhi kuliko yote ni hili, halafu waziri husika hajaingizwa katika kundi la G8 ya mwaka huu. Hii ni mbaya kulika hata wakati wa ukoloni. kwa mfano matokeo ya kidato cha nne yaliyopita, Daraja la kwanza hadi la tatu 9% daraja la nne na sifuri 91% halafu tunatarajia nchi iwe na maendeleo chanya kwa takwimu za namna hii? sipendi uongozi tulionao kwa vile hili hawalizungumzii, hata kambi ya upinzani bungeni sijasikia wakikemea hili, tunajenga Tanzania ya namna gani? nimekasirika kidogo tu ningetukana lakini kwa bahati nzuri sijalelewa hivyo kama kibajaji.:embarrassed1:
 
Pamoja na mtazamo wako,kosa la Kanda ya Kaskazini kuichukia CCM ni lipi?
Watu wa Kanda ya Kaskazini ni wachapa kazi CCM ingefanyakazi vizuri kusingekuwa na tatizo!:tongue:
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, nipatapo fursa, hupita huku na kule na kubadilishana mawazo na watu mbalimbali wa kada tofauti. Kwa takriban siku 3 zilizopita, nimepata fursa ya kutembelea mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambayo ndiyo inayo dorminate Kanda ya Kaskazini, kiukweli CCM Imechokwa mpaka basi!.

Siku zote nimekuwa nikisema humu, CCM imekuwa ikichaguliwa na wengi sio kwa sababu ya kupendwa au kukubalika sana, bali kwa mazoea tuu wengi wakiwa ndicho chama pekee walichokifahamu tangu wamezaliwa, na wengine wakikichagua CCM kama asante ya kutuletea uhuru kupitia TANU, na idadi kubwa ya walio vijijini, wamekuwa wakiichagua CCM kwa ignorance tuu ya elimu ya uraia!. Sasa wale wanaichagua CCM kama asante ya kutupatia uhuru, ni oldguard, wanazidi kupungua na wachache waliobakia they days are numbered!. Wale wengi waliokuwa wakiichagua kwa ignorance, sasa wameamka!.

Kwa mujibu wa kada mbalimbali nilozungumza nao, wamethibitisha kuwa hakuna jinsi Ole Sendeka, Ole Medeye na Ole Nyaguro wataweza kusalimika, sehemu salama mpaka sasa ni Jimbo la Monduli tuu!.

Kama kasi ya upepo wa mwamko kama Kanda ya Kaskazini, utaingia kanda ya Ziwa kwa kasi hiyo hiyo, then hakuna jinsi yoyote ya kuiokoa CCM isipigwe mwereka uchaguzi wa 2015!.

Determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii, ni wapiga kura wa Kanda ya Ziwa ambayo ndiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya watu!. Kati ya watu milioni 40 wa sensa ya mwaka 2002 kwa Tanzania yenye makabila 120, Wasukuma peke yao wako milioni 6!. Sasa ukiwajumlisha na Kanda ya Kaskazini, hata kama mikoa yote iliyobakia wataipigia kura CCM, bado kwa kanda hizo mbili pekee, zinatosha kabisa kuipiga chini CCM!.

Mwelekeo huu ni uthibitisho kuwa ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania, sio ndoto tena, ni kitu ambacho kinawezekana!.

Natoa mwito kwa Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu, tusiendekeze hizi siasa za chuki za kukichukia chama fulani bila sababu za msingi ya chuki hiyo, au kukipenda na kikishabikia chama fulani kwa upenzi tuu, matokeo ya mwisho ya siasa hizi ni kujengeana chuki zisizo na sababu!. Tupingane bila kupigana, tutofautiane kisiasa bila kuchukiana bali tupingane huku tukipendana!.

Hata mimi uchaguzi wa Arumeru, nilisimama na Sioi, tumekutana na Nasari pale Dodoma, tumekumbatiana, na kiukweli kutoka moyoni mwangu, sina chuki na Nasari, namkubali kwa dhati japo namhurumia Sioi kwa sababu ni rafiki!.

Nyie watu wa Kanda ya Kaskazini, msiichukie hivyo CCM, kwani pamoja na mabaya yake, pia kuna mema mengi imelifanyia taifa hili!.

Namalizia kwa kusisitiza, huu ni mtazamo tuu!

Wasalaam.

Pasco
Arusha.

Hapo kwenye nyekundu, naona busara imeanza kuingia akilini mwa wanachama. Nitafurahi kama hayo maneno yangekuwa yanatolewa kwenye hotuba za viongozi baada ya maandamano. Nchi hii ni yetu wote na tusikubali kugawanyika kwa chuki na vurugu maana zikianza hazitachugua chama, sote tutaathirika. Nilikuwa na rafiki yangu kutoka Kenya week-end iliyopita akawa anasema huwa wanafuatilia sana siasa za TZ lakini cha kutia moyo ni pale aliponiambia kwamba wengi wanatuombea kusitokee ghasia kama zilizotokea Kenya wakati wa uchaguzi huko kwao. Siasa za matusi na midomo huanzisha vita.
 
Ukombozi wa kweli upo mioyoni mwa watu wote wa Tanzania kutoka Kusini hadi Kaskazini na Mashariki hadi Magharibi.
Yaliotokea Kanda ya Ziwa, Nyanda za Juu Kusini na siku za nyuma kule Pemba, si Kaskazini. Pasco Usligawe Taifa, kote wamechoka ni fursa hajawafikia vichwani mwao na kuamua ila siku za aja Tanzania nzima na watu wake wataushangaza ulimwengu ktk maamuzi yao ktk UKOMBOZI WA KWELI ktk FIKRA UCHUMI na kumiliki raslimali zao.

Mungu Ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania Mungu Ibariki CDM!!!!!!
 
Hii taarifa ya PASCO ina mtego sana huyu pasco si mwema kwa Makamanda kwani anabagua kanda kitu ambacho kwa cc wadanganyika kamwe tusikukubali

Mkuu kweli yanyojitokeza kote Tanzania si ya Ukanda tena watu wameshatambua uhaini wao wakutugawa na kutudandanya. Viva M4C a road 2 2015!
 
Mkuu Pasco,

Tafadhali badilisha tittle ya huu uzi, Iwe Watanzania wameichoka CCM kuanzia Kusini hadi Kaskazini, Mashariki hadi Magharibi.

Maana huko kulikobaki CCM mimi sijui ni wapi... Labda tu wale wenye maslahi binafsi na wageni wa Nje wanaonufaika na Rasilimali zetu ndiyo wanaopigania CCM iendelee kuongoza.
 
Mtazamo wangu ni kuwa hatakama tangazo hilo lililotolewa na UVCCM Mkoa wa Pwani liliwakera lakini hao ndugu zetu hawajaonyesha uvumilivu hebu angalia toka tumepata uhuru nchi hii Mikoa hiyo miwili Arusha na Kilimanjaro imetoa Mawaziri Wakuu 4 tena katika Jimbo moja tu wametoka 2,Marehemu Edward Sokoine na Edward Lowasa, Frederick Sumaye katoka Manyara lakini bado ilikuwa sehemu ya Arusha na David Msuya katoka Kilimanjaro tena huyu Msuya alitoa kauli za kebehi kwenye Bunge lakini hao ndugu zake hawakumkemea kwa kuwa alikuwa wa kwao hivi mbona sehemu nyingine katika Tanzania watu walikuwa watulivu? Madaraka katika Nchi hii ni ya kugawana wao hawana hati miliki na uongozi pekee yao wasituchafulie hali ya hewa!
Naona wewe una mawazo ya uongozi wa kupewa kutokana na sehemu unayotoka,
hata kama wangetoka eneo moja kinachotakiwa ni uwezo.
 
Mtazamo wangu ni kuwa hatakama tangazo hilo lililotolewa na UVCCM Mkoa wa Pwani liliwakera lakini hao ndugu zetu hawajaonyesha uvumilivu hebu angalia toka tumepata uhuru nchi hii Mikoa hiyo miwili Arusha na Kilimanjaro imetoa Mawaziri Wakuu 4 tena katika Jimbo moja tu wametoka 2,Marehemu Edward Sokoine na Edward Lowasa, Frederick Sumaye katoka Manyara lakini bado ilikuwa sehemu ya Arusha na David Msuya katoka Kilimanjaro tena huyu Msuya alitoa kauli za kebehi kwenye Bunge lakini hao ndugu zake hawakumkemea kwa kuwa alikuwa wa kwao hivi mbona sehemu nyingine katika Tanzania watu walikuwa watulivu? Madaraka katika Nchi hii ni ya kugawana wao hawana hati miliki na uongozi pekee yao wasituchafulie hali ya hewa!

Hemedi Maronda,

..Sokoine na Lowassa wametokea Monduli ambako bado ni ngome ya CCM.

..Sumaye anatokea Hanang ni jimbo lake sasa hivi limeshikwa na Mary Nagu wa CCM.

..Cleopa Msuya anatokea Mwanga, jimbo lake limeshikwa na Prof.Jumanne Maghembe wa CCM.

..hii hoja kwamba wananchi wa Hananga,Monduli,na Mwanga, wameikataa CCM kwa misingi ya ukanda inatoka wapi??

..mimi nanachoona kinaendelea huko ni kwamba wananchi wanachagua mgombea bora wanayeona atawaletea maendeleo.

..chama chochote kile kinachofikiria kina hati miliki na majimbo ktk mkoa wa Arusha au Kilimanjaro kinafanya makosa makubwa sana.

..nikupe mfano wa jimbo la Hai anakotoka Freeman Mbowe. Mwaka 1995 Mbowe aligombea na kushindwa na Makidara Mosi wa NCCR. mwaka 2000 Freeman Mbowe akagombea tena na kushinda. Mwaka 2005 jimbo likarudi CCM, na 2010 jimbo limerudi tena Chadema.

..Jimbo lingine ni lile la Rombo kwa Basil Mramba. CCM wamepoteza jimbo hilo kutokana na kuendekeza kwao UFISADI na kumsimamisha Mramba ambaye amechafuka kwa kashfa ya matumizi mabaya ya ofisi. Katika mazingira kama hayo kwanini muwalaumu wananchi wa Rombo kwa kumkataa mgombea wa CCM mwenye kesi ya ufisadi mahakamani??

..CCM wameboronga, sasa badala ya kurekebisha makosa yao wanazua mambo ya UDINI na UKANDA. Hivi wananchi wa Same,Mwanga,Monduli,Arumeru Magharibi,Ngorongoro,Hanang, na maeneo mengine ya Kilimanjaro na Arusha ambako wameichagua CCM wakisikia hizi hoja zenye kuwabagua na kuwaita "Wakaskazini" mnafikiri watajisikia namna gani??
 
Naombeni nijibu baadhi ya hoja nikianzia na hili la ubaguzi wa ukanda, ukabila na udini.

Facts are sturbon things na huu ni ukweli mchungu ambao Watanzania lazima tuukubali, tuumeze ndipo tusonge mbele!.

Unamaanisha Chadema wakijipanga watazoa kura Pemba?. Jee unazijua sababu zinazopelekea CCM kushindwa kupata hata kiti kimoja Pemba?. Kwa hiyo Chadema wakijipanga watavuna majimbo Pemba!.

Hivi unayo taarifaa kama sio Nyerere kufuta mitihani ya Cambridge kwa pass mark moja nchi nzima, shule zote za sekondari na vyuo vyote vingejaa watu wa makabila fulani fulani tuu?!. Na kuna makabila fulani fulani wangeishia shule za msingi tuu! Utake usitake sababu zipo na ni facts!. You can't deny facts!. Jee hizo sababu ni za kipuuzi?.

Sisi sote ni Watanzania na nchi yetu ni moja, jee unajua kuna watu wa dini fulani fulani wamepata fursa za kujiendeleza kielimu kuliko dini fulani fulani?. Unazijua sababu?. Sababu hizo ni facts!. Jee nazo ni upuuzi?.

Unajua moto nyikani huanza vipi?. Siku zote moto wa nyika huanzishwa na cheche moja tuu na kuenezwa na upepo. Unajua cheche ikianzia upande tofouti na upepo unavyovuma moto huo huzimika papo hapo!.

Kwenye siasa kuna kitu kinaitwa ngome. Ngome ndipo pale ambapo umeota mizizi na unapoanzishia cheche ya moto wa nyika yako ambapo utasambaa!.

CUF wana ngome yao na mtaji wao waliowekeza na ndio maana wanavuna walichopanda!. CDM nao wana ngome yao na mtaji wao ni watu. CCM kwa vile kilikuwa chama tawala chenyewe kote ni ngome zake na mtaji wake ni mtandao wake ulioenea hadi vijijini. Ili kuleta mageuzi ya kweli ni lazima waokombe huo mtaji wa CCM na ili kuukomba lazima moto wako ukauanzishie kwenye ngome yako ndipo usambae kote!.

Kubali kataa siasa za ukabila zipo ndio maana kuna makabila fulani hawawezi kuukwa urais wa nchi hii no matter how good they are!.

Huu sio uongo ni bitter truth ambazo lazima tukabiliane nazo kwa kuzi face na sio ni deny kwa kukanusha as if they don't exist!.

Lets face the bitter truth kwa kumeza the bitter pill ili kuutibu huu ugonjwa wa ukanda, udini na ukabila!.

Mimi binafsi ni muumini wa ukweli na hivyo naamini ukanda, ukabila na udini, upo kwenye siasa za Tanzania na dawa yake ni to set a thief to catch a thief, tuutumie ukabila huo huo, udini huo huo na ukanda huo huo kuutibu ugonjwa huo huo!.

Pasco!.
 
Pasco,

..Pemba imekuwa ngome ya CUF kutokana na Wapemba kubaguliwa na kunyimwa nafasi za uongozi ktk CCM. haya yamefanyika kwa muda mrefu na kutokana na ukiritimba wa vyombo vya habari wakati wa mfumo wa chama kimoja hamkuwa na habari nayo. hivi hujasikia zile kauli na kejeli kwamba "Wapemba hamkupindua"??

..kuhusu masuala ya kufutwa kwa mitihani ya Cambridge na kuletwa kwa quota system, mimi sidhani kama hatua hizo zimesaidia kuleta equality ktk upatikanaji wa elimu. Tulichotakiwa kufanya ni kuboresha elimu ktk maeneo ya pembezoni na siyo kuwadanganya kwa kuwapa pass mark ndogo ili waweze kuendelea. mimi namjua jamaa mmoja wa "kaskazini" alitumia jina kama lako la ubini kukwepa quota system ya Mwalimu Nyerere!!!

..hoja za kusema watu wa maeneo fulani hawastahili uongozi wa nchi hii ni mufilisi. inasikitisha sana msomi kama wewe kuzishabikia ktk Tanzania ya leo. Inawezekana tulikuwa huko, but I dont think we want our kids to grow up with such mindset.

..tuachane na hizo hoja za ukabila,ukanda na udini, zinabomoa hazijengi. tukianza kuhalalisha na kujenga mazoea ya kufikiria na kutazama kila jambo kwa "miwani na darubini" ya udini,ukabila,na ukanda, muda si mrefu nchi hii itasambaratika.
 
Naombeni nijibu baadhi ya hoja nikianzia na hili la ubaguzi wa ukanda, ukabila na udini.

Facts are sturbon things na huu ni ukweli mchungu ambao Watanzania lazima tuukubali, tuumeze ndipo tusonge mbele!.

Unamaanisha Chadema wakijipanga watazoa kura Pemba?. Jee unazijua sababu zinazopelekea CCM kushindwa kupata hata kiti kimoja Pemba?. Kwa hiyo Chadema wakijipanga watavuna majimbo Pemba!.

Hivi unayo taarifaa kama sio Nyerere kufuta mitihani ya Cambridge kwa pass mark moja nchi nzima, shule zote za sekondari na vyuo vyote vingejaa watu wa makabila fulani fulani tuu?!. Na kuna makabila fulani fulani wangeishia shule za msingi tuu! Utake usitake sababu zipo na ni facts!. You can't deny facts!. Jee hizo sababu ni za kipuuzi?.

Sisi sote ni Watanzania na nchi yetu ni moja, jee unajua kuna watu wa dini fulani fulani wamepata fursa za kujiendeleza kielimu kuliko dini fulani fulani?. Unazijua sababu?. Sababu hizo ni facts!. Jee nazo ni upuuzi?.

Unajua moto nyikani huanza vipi?. Siku zote moto wa nyika huanzishwa na cheche moja tuu na kuenezwa na upepo. Unajua cheche ikianzia upande tofouti na upepo unavyovuma moto huo huzimika papo hapo!.

Kwenye siasa kuna kitu kinaitwa ngome. Ngome ndipo pale ambapo umeota mizizi na unapoanzishia cheche ya moto wa nyika yako ambapo utasambaa!.

CUF wana ngome yao na mtaji wao waliowekeza na ndio maana wanavuna walichopanda!. CDM nao wana ngome yao na mtaji wao ni watu. CCM kwa vile kilikuwa chama tawala chenyewe kote ni ngome zake na mtaji wake ni mtandao wake ulioenea hadi vijijini. Ili kuleta mageuzi ya kweli ni lazima waokombe huo mtaji wa CCM na ili kuukomba lazima moto wako ukauanzishie kwenye ngome yako ndipo usambae kote!.

Kubali kataa siasa za ukabila zipo ndio maana kuna makabila fulani hawawezi kuukwa urais wa nchi hii no matter how good they are!.

Huu sio uongo ni bitter truth ambazo lazima tukabiliane nazo kwa kuzi face na sio ni deny kwa kukanusha as if they don't exist!.

Lets face the bitter truth kwa kumeza the bitter pill ili kuutibu huu ugonjwa wa ukanda, udini na ukabila!.

Mimi binafsi ni muumini wa ukweli na hivyo naamini ukanda, ukabila na udini, upo kwenye siasa za Tanzania na dawa yake ni to set a thief to catch a thief, tuutumie ukabila huo huo, udini huo huo na ukanda huo huo kuutibu ugonjwa huo huo!.

Pasco!.

Tone hii inamaanisha umeshikwa Pasco. asante pia kwani wengi tu humu haya ni mageni kwao! Pole wa ng'wa faza!!
 
Pasco,

..Kigoma ndiyo mkoa wa kwanza kuchagua mbunge toka upinzani, Dr.Walid Amani Kaborou alipokuwa CDM.

..pia mkoa huo umeendeleza rekodi yake ya kuchagua wabunge wa upinzani ktk kila uchaguzi.

..kinachonishangaza ni kuona kwamba Kigoma hawaandamwi kwa kuikataa CCM, kama inavyotokea kwa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

..kwanini hatusikii shutuma za "Wakigoma/Ukigoma" au "Umagharibi" bali tunasikia "Ukilimanjaro" na "Ukaskazini"??

NB:

..Pasco anatetea na kushabikia ubaguzi akidai kwamba ni "facts"!!
 
... kuhusu masuala ya kufutwa kwa mitihani ya Cambridge na kuletwa kwa quota system, mimi sidhani kama hatua hizo zimesaidia kuleta equality ktk upatikanaji wa elimu. Tulichotakiwa kufanya ni kuboresha elimu ktk maeneo ya pembezoni na siyo kuwadanganya kwa kuwapa pass mark ndogo ili waweze kuendelea. mimi namjua jamaa mmoja wa "kaskazini" alitumia jina kama lako la ubini kukwepa quota system ya Mwalimu Nyerere!!!

Mkuu JokaKuu,

Hapo kwenye red na nimeongezea mkolezo, Prof. Malekela wa Kitivo cha Elimu pale UD (sijui kama bado yupo) aliwahi kufanya utafiti kuhusu quota system elimu ya sekondari. Anasema alikutana na vituko vingi sana: Kuna wanafunzi unakuta ana sir name inayotambulisha kwamba anatokea kabila fulani, lakini ukimuuliza anakuambia yeye ni kabila jingine. Wako watu kibao walikuwa wana majina kiislam lakini ni wakristo. Katika utafiti alikuja akagundua kwamba wanafunzi wa ukanda fulani wakimaliza shule na kutochaguliwa kwenda sekondari, walikuwa wakihamia shule za msingi za ukanda mwingine na kwenda kurudia darasa 6 au 7 kwa kutumia majina ya wanafunzi walio drop out kwenye ukanda huo and finally anakuja kuchaguliwa kwenda sekondari.

Quota system in a way haikuwa effective kama walivyotarajia na pia imesaidia kunyima fursa wanafunzi wenye uwezo darasani na wengine kucheleweshwa kwa kupita njia ndefu za kwenda kurudia shule za mikoa mingine.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom