Maundumula
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 7,553
- 3,071
Baada ya kuwalazimisha Madaktari kurudi kazini, hali ikawa hivyi
Daktari: Karibu mgonjwa unasumbuliwa na nini?
Mgonjwa: Asante Daktari, najisikia homa, viungo vyote vinauma, usiku na tetemeka kwa baridi
Daktari: Ohh pole sana inaonekana huo ni uchovu tu, labda kama kungekuwa na vifaa tungeangalia kwa makini tatizo ni nini, lakini kwa sasa kapumzike nyumbani utapona tu
Mgonjwa: nitaponaje kwa kupumzika?
Daktari: nani daktari kati yangu na wewe?
Mgonjwa: ni wewe, lakini si uniambie ninaumwa nini?
Daktari: Unaumwa uchovu, kapumzike
:israel:
Hapo sasa huyo daktari atakuwa mwehu maana huyo mgonjwa ndio analipia hiyo 900,000 na ndio kodi yake imemsomesha daktari bure.