Mshahara wa TShs 900,000 hautoshi kabisa

Baada ya kuwalazimisha Madaktari kurudi kazini, hali ikawa hivyi
Daktari: Karibu mgonjwa unasumbuliwa na nini?
Mgonjwa: Asante Daktari, najisikia homa, viungo vyote vinauma, usiku na tetemeka kwa baridi
Daktari: Ohh pole sana inaonekana huo ni uchovu tu, labda kama kungekuwa na vifaa tungeangalia kwa makini tatizo ni nini, lakini kwa sasa kapumzike nyumbani utapona tu
Mgonjwa: nitaponaje kwa kupumzika?
Daktari: nani daktari kati yangu na wewe?
Mgonjwa: ni wewe, lakini si uniambie ninaumwa nini?
Daktari: Unaumwa uchovu, kapumzike
:israel:

Hapo sasa huyo daktari atakuwa mwehu maana huyo mgonjwa ndio analipia hiyo 900,000 na ndio kodi yake imemsomesha daktari bure.
 
Kwa yeyote ambaye anaishi Tz huo mshahara kwa madr ni mdogo!
Tuache ushabiki na simaanishi wapewe 3.5mil cha msingi wakae meza moja na serikali then come up with the way forward!
Hii inchi ni yetu sote msianze leta suala la kukomoana apa!
 
Mgomo wa madaktari unasababishwa na mambo mengi sana. Kwani hata ukiangalia wakija kupewa hiyo 3.5 bado takehome ni kama 2.XX. Cha msingi hapa serikali ingalie haya mambo kuanzia mbali ikiwa ni pamoja na kushusha PAYEEE. Jamani PAYEE inaumizaaaaaaaaa.
 
we fuso yaonesha unaakili ka za mamba yani unataka kutuaminisha hapa kuwa kila doctor ana hospital yake/ kweli wewe kafara tupu
 
2hell kama 5m sio kitu katibiwe india

Madaktari ni kama Walimu. Ni wazalendo na si kama kada zingine. Tofauti yao na waalimu ni ugumu na risk za kazi ya doctors kuwa kubwa. Lakini mhasibu hata ukimwambia unamlipa elfu 50 si ajabu akafanya kazi kwa kuwa ataiba tu. Waheshimuni sana doctors jamani. Jaribu kufikiria wewe ulivyokimbia masomo ya sayansi kwa kuogopa ugumu wake. Doctors na engineers hawakufanya hivyo. Wapewe sifa hawa watu.
 
Nakubaliana na wewe unavyosema mi shida yangu ni kwamba kwa nini tushabikie huu mgomo? yaani tukishabikia then wakafanya ndo shida zitakua zimeeisha? huo mfumo unaotaka ubadilike si dhani kama utabdilishwa na huu mgomo? unakumbuka pale mwanzo serikali ilipokubaliana kukaa na ma dr kuna mtu mwingine aliendelea kulalamika? fikiria zaidi broda. tunahitaji kitu zaidi ya hapo

mgomo ni njia bora kabisa kwa mtu asiyesikilizwa! Bila mgomo huu nani angejua ubovu wa maslahi ya ma dr.
Martin luther King Jr. Aliwahi kusema "riot is the voice of the unheard". We subiri huo ni mwanzo tu!
 
Hapo sasa huyo daktari atakuwa mwehu maana huyo mgonjwa ndio analipia hiyo 900,000 na ndio kodi yake imemsomesha daktari bure.
mkuu hivi nani kawaambia madactari wanasomeshwa bure????????????????????????? mbona watu wanarudisha hizo pesa nawashangaa sana nakusema eti bure! kuna kitu cha bure?
 
Wamelupiwa na serikali hizo shule .matatizo ya elimu ya bure

Siri ya mtungi aijuaye kata.....hakuna shule ya bure, ule mkopo wanakatwa kila mwezi karibia 60000 wengine mpaka 70000
 
Wakuu
Viongozi watanzania wamezoa kudanganywa kwa TAKWIMU...hili neno ni kama UMRI yaani kila sekunde inapopita umri unaongezeka na mabo mengine yanabadilika mwilini.hivyo pia mshahara wa miaka mitatu nyuma haiwezi kuwa sawa na ya leo hii kwani kuna mabadiliko mengi katika gharama na bei halisi za kuishi humu duniani hivyo ili kumantain hali hiyo ya maisha lazima kiwango cha pesa kiongezeke japo matumizi ni yaleyale

laki tano ya mwaka juzi kiuhalisia sio sawa na laki tano ya leo...kwa kupata mahitaji yaleyale utahitaji walau 1.2m hivyo hata kama umepandisha mshahara from laki tano to laki tisa bado kiuhalisia unaweza kuwa hata umeshuka level kadhaain comparison to value..i mean ongezeko hilo lingefanyika mwajka juzi lingekidhi lakini kwa sasa sio ongezeko tena ila ni mtiririko kama ule wa UMRI..

ningeelewa ungesema laki tano ya mwaka juzi ni sawa na milioni na laki 2 ya leo hivyo ukiongeza kiwango unaongeza from 1.2 kwenda juu itamake sense..
Vinginevyo ni TAKWIMU tu ambazo obviously zinapanda lakini mshahara unadidimia

Magamaba hutumia takwimu kuhadaa...yaani hata mtoto lazima akue hawezi kubaki vilevile kila siku
 
Mshahara wa Mbunge 2.5 Milioni, Madakatari wanataka 3.5Milion, Haiwezekani nawashauri wafanye analysis kama inawezekana, Kama kusoma Miaka 5 Hata lawyer wanasoma Miaka hiyo na mishahara mmewazidi, Halafu kama unasomei kitu ili kikulipe somea kitu kinacholipwa hakuna mtu aliyelazimishwa kusomea Udaktari,
Halafu mtueleze Madaktari Secta ya afya inaongoza kwa Rushwa na Wizi wa Madawa na Kuwaelekeza wagonjwa kwenye Maduka yenu mtalimalizaje hilo sion tu mnataka Mishahara mikubwa hamsemi yakwenu mtamalizaje

Kumbe Mkw.ree amepata wafuasi humu. Hoja ya madaktari sio mshahara kama serikali invyotaka wajinga waelewe. Jaribuni kutafuta hoja zao zote mzisome mtajua kuwa kuna mengi ya msingi kwa sisi tunaogua kila uchao na kukosa huduma bora kwa ajili ya kuboresha afya zetu. Acheni kuwehuka na jinsi serikali livyojikita kwenye hoja moja tu kati ya nyingi zilizowasilishwa mbele yao!
 
Hii tabia kwa watanzania sijui itaisha lini na inaonesha bado tuna safari ndefu sana.Madaktari wanailalamikia serikali iboreshe mazingira yao ya kazi then wanasimama fani zingine mbona sisi tunapewa hivi! Kitu kama hakikuhusu ni bora ukae kimya na kama nawe unahitaji kuboreshewa subiri wakati wako nawe udai kwa nafasi yako.Asipoongezewa Daktari hizo hela unadhani utapewa wewe mhasibu ama mwalimu ama askari. Tuache utoto na tukue kimawazo.Nawakilisha!!!
 
lets be honest mshahara wa laki 9 hautoshi kwa namna yoyote ile kwa graduate yoyote yule let alone daktari nadhan hata wengi tunaochangia hapa tunalijua hilo! na tusichanganye madesa eti kutakua na tofauti kubwa na watumishi wengine je mnajua mishahara ya agency za serikali kama tra, bot, nssf, nhc, tanesco, bandari etc ni mikubwa kwa iyo na madaktari hata kulipwa mil 3.5 si kikubwa hata kidogo so wakaze uzi walimu wao walishajikubalia kufa kisabuni basi ndio ule msemo wa jesus waachae wafu wawazike wafu wenzao lakini madaktari wametake right step!
 
Waliosomeshwa na serikali, wasiosomeshwa na serikali wote, mantanyanga, kukatwa PAYE kupo pale pale, kwa Tanzania mwenyenafuu ni aliejiajiri kwasabb atakwepa kwepa kodi.

Huu ukoloni wa mshahara 900,000/= kodi laki 200,000 ulikuwa wa cheap labour kumbuka history cheap lablour... unadanganya mshara ni mil. 20 kodi mil. 17,

Rubbish
 
Hivi kweli madaktari bongo wanalipwa laki tisa?Yaani hata wale wanaojiita mabingwa?
 
mkuu hivi nani kawaambia madactari wanasomeshwa bure????????????????????????? mbona watu wanarudisha hizo pesa nawashangaa sana nakusema eti bure! kuna kitu cha bure?

hao ndio wanaccm wasiojua lolote,na pengine shule hamna hapo
 
Mkuu, Mshahara wa sh 955,000/- ikishakatwa PPF na PAYE inabaki Sh. 720,000/- na sio Laki tano na nusu.
Kimsingi sikubaliani na Mbunge kulipwa 10,000,000/- kwa wiki4 alafu daktari analipwa asilimia 10% ya mshahara wa mbunge.

Kwa walimu ndiyo kituko, mwalimu anayefundisha chuo cha ualimu anapokea mshara TGTS E kama mshahara wa kuanzia,lakini mwalimu yuleyule wa masomo yale yale anaanza na TGTS D.Mfano wapo walimu wamesoma BED wapo sekondari wanalipwa kwa ngazi ya TGTS D wakati wale wa Vyuoni wanalipwa ngazi ya TGTSE.

Eti watu hawapandishi madaraja hata kama muda wao wa kupanda daraja umefika kwa kisingizio wanaogopa madeni hali wakijua fika kwakufanya hivyo unamwibia mtumishi kiutumishi hasa wale wanao karibia kustaafu kwani wanaweza kustaafu wakiwa katika daraja lisilo stahiki.Ni heri kutoa barua mtumishi adai kuliko kumpunja kiutumishi.

Kitendo cha kutopandisha vidato katika mshahara kama vile TGTS C1,C2,C3 nk kinawafanya watumishi walioanza kazi zamani na wa karibuni kuwa na mishahara sawa jambo ambalo si sahihi.
 
Back
Top Bottom