Mshahara wa TShs 900,000 hautoshi kabisa

Natalia KUWA SERIOUS WALE KULE KAIRUKI, IMTU WANASOMESHWA BURE UMESOMA WEWE KWELI MADACTARI WOTE WANASOMESHWA NA SERIKALI?

NAKUULIZA Natalia,Huwa natoa mifano ya kweli nauhalisia, nina kaka yangu anasoma KAIRUKI udactari analipa ada 5,000,000 per year na anajilipia mwenyewe ada *5yrs =25,000,000/tsh toa usafiri, toa emergence, toa malazi, kweli huyu mtu atamaliza umlipe 500,000 akubaliane na wewe?

Laki tano ni hela za makeshia wenye diploma bana. Twende mbele turudi nyuma je hao madactari wakirudishwa kwa nguvu watawatibu watu kwa moyo na kwa upendo? Chukua zako changanya na zangu tujijibu swali

Baada ya kuwalazimisha Madaktari kurudi kazini, hali ikawa hivyi
Daktari: Karibu mgonjwa unasumbuliwa na nini?
Mgonjwa: Asante Daktari, najisikia homa, viungo vyote vinauma, usiku na tetemeka kwa baridi
Daktari: Ohh pole sana inaonekana huo ni uchovu tu, labda kama kungekuwa na vifaa tungeangalia kwa makini tatizo ni nini, lakini kwa sasa kapumzike nyumbani utapona tu
Mgonjwa: nitaponaje kwa kupumzika?
Daktari: nani daktari kati yangu na wewe?
Mgonjwa: ni wewe, lakini si uniambie ninaumwa nini?
Daktari: Unaumwa uchovu, kapumzike
:israel:
 
Just go and work where they gonna pay you what u want....
5M kitu gani kwenye elimu? Some people of paid £7000 for tuition fee only and they r working for 1-2M private sector!!!!
2hell kama 5m sio kitu katibiwe india
 
Baada ya kuwalazimisha Madaktari kurudi kazini, hali ikawa hivyi
Daktari: Karibu mgonjwa unasumbuliwa na nini?
Mgonjwa: Asante Daktari, najisikia homa, viungo vyote vinauma, usiku na tetemeka kwa baridi
Daktari: Ohh pole sana inaonekana huo ni uchovu tu, labda kama kungekuwa na vifaa tungeangalia kwa makini tatizo ni nini, lakini kwa sasa kapumzike nyumbani utapona tu
Mgonjwa: nitaponaje kwa kupumzika?
Daktari: nani daktari kati yangu na wewe?
Mgonjwa: ni wewe, lakini si uniambie ninaumwa nini?
Daktari: Unaumwa uchovu, kapumzike
:israel:
Tatizo lako unafikiri ma Dr. wana moyo wa kutu, ni watu kama wewe.!
 
Tatizo lako unafikiri ma Dr. wana moyo wa kutu, ni watu kama wewe.!

Nafahamu kuwa wana moyo wa kibinadamu hata mara nyingine kuzidi wa kwangu na wako, lakini unafikiri bila vifaa watatumia masaburi kumpima mgonjwa? usituletee hoja za udhaifu hapa
 
Mshahara wa Mbunge 2.5 Milioni, Madakatari wanataka 3.5Milion, Haiwezekani nawashauri wafanye analysis kama inawezekana, Kama kusoma Miaka 5 Hata lawyer wanasoma Miaka hiyo na mishahara mmewazidi, Halafu kama unasomei kitu ili kikulipe somea kitu kinacholipwa hakuna mtu aliyelazimishwa kusomea Udaktari,
Halafu mtueleze Madaktari Secta ya afya inaongoza kwa Rushwa na Wizi wa Madawa na Kuwaelekeza wagonjwa kwenye Maduka yenu mtalimalizaje hilo sion tu mnataka Mishahara mikubwa hamsemi yakwenu mtamalizaje

Mbunge ambae hata darasa la saba hakumaliza kwanini alipwe mil 2.5?
 
Nafahamu kuwa wana moyo wa kibinadamu hata mara nyingine kuzidi wa kwangu na wako, lakini unafikiri bila vifaa watatumia masaburi kumpima mgonjwa? usituletee hoja za udhaifu hapa

Mpangamji tuwe wa kweli kabisa, katika madai ya ma dr. yapo 12 kama sikosei. we jiulize kwa nini "kuboreshewa maslahi" wamelinyumbuilisha wanataka nini kwenye hilo mfano "posho ya kuitwa kazini, posho ya nyumba, posho ya usafiri, greencard etc" lakini hii ya "kuboresha mazingira ya kazi" kwanini hawajanyumbulisha? wankuja kunyumbulisha wakiwa kwenye vyombo vya habari? kwa nini lile la kwanza nalo wasingeliacha kama lilivyo yaani "kuboresha maslai"
 
Zanta, nakumbuka kuna sehemu ilishawahi kuulizwa "ukweli ni kitu gani"? vyovyote vile ambavyo madaktari wanajenga hoja zao, iwe kwa maslahi binafisi-kwa maana ya ubinafsi au kwa maslahi yao pamoja na kidogo kwa ajili ya wananchi, binafisi sina tatizo nalo. Jiulize mara ngapi Mheshimiwa Dr. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (ingawa Zanzibari) hawataki aliwahi kukemea ufisadi kwa dhati na ukali kama anaotumia kuwapinga madaktari kwenye maslahi yao. Mabilioni yaliyotoroshwa huko Uswizi, Mambo ya Rada. Unafikiri hayo mambo serikali ingekuwa inayafuatilia kwa mkono wa chuma kama ambavyo haitaki maslahi ya madaktari wangapi tungekuwa tunapost humu jf kuipinga serikali na kuonekana na hoja za maana, wamebaki Ritz na Zomba tu vichwa vigumu, unaweza kukuta kuwa wanalipwa kwa kufanya hivyo. Amka. Binafsi hata kama lengo lao ni mshahara wao tu na hawana lengo lolote la kuboresha huduma za afya, nawaunga mkono.
 
kwa hiyo ma dr wakipewa huo mshahara we kwako ndo shida itakua imeisha? na shida ya mambilioni na sijui rada havitasikika tena? au kuna zaidi kinatakiwa kifanyike na sio kushabikia mgomo pekee?
 
Mkuu, Mshahara wa sh 955,000/- ikishakatwa PPF na PAYE inabaki Sh. 720,000/- na sio Laki tano na nusu.
Kimsingi sikubaliani na Mbunge kulipwa 10,000,000/- kwa wiki4 alafu daktari analipwa asilimia 10% ya mshahara wa mbunge.

Tatizo huyo Mbunge anakuwa hana shule zaidi ya kubumba vyeti vya ualimu na kadhalika. Mcheki Mzee Luku anacheti cha ualimu gade IIIA na vicouse vya kuunga analamba 10M kwa kuomba muongozo wa bi kiroboto
 
kwa hiyo ma dr wakipewa huo mshahara we kwako ndo shida itakua imeisha? na shida ya mambilioni na sijui rada havitasikika tena? au kuna zaidi kinatakiwa kifanyike na sio kushabikia mgomo pekee?

Hili suala haliwezi kuisha kwa madaktari kupewa wanachokitaka, hili suala ni suala la mfumo. ni suala ambalo wananchi wangependa kuona mtu anayesema kitu anachokimaanisha na wananchi wakaamini hilo alisemalo. Kwa hali ya sasa yenye taarifa mpya za kifisadi kila siku, Mheshimiwa Dr. Rais hata kama angesema ukweli na kutoa machozi, bado mfululizo wa matukio ya serikali yake, mawaziri wake na mafisadi, wanaleta mashaka mioyoni mwa watanzania. Bila yeye kuanza kuonyesha udikiteta kwa mafisadi, watu wanaoitafuna keki ya taifa akaonyesha kwa macho makavu, hakuna mtu atakayemsikiliza, tulia uone hii ngoma unogile! watu wamechoka, kama hawajachoka basi mimi nimechoka, siku Zomba na Ritz watakapoonja maisha magumu siku hiyo utayakumbuka maneno ya JF members.

Signature yako inaeleza kila kitu.
 
Nakubaliana na wewe unavyosema mi shida yangu ni kwamba kwa nini tushabikie huu mgomo? yaani tukishabikia then wakafanya ndo shida zitakua zimeeisha? huo mfumo unaotaka ubadilike si dhani kama utabdilishwa na huu mgomo? unakumbuka pale mwanzo serikali ilipokubaliana kukaa na ma dr kuna mtu mwingine aliendelea kulalamika? fikiria zaidi broda. tunahitaji kitu zaidi ya hapo
 
Hapa kuna mambo ya kimsingi ambayo yalitakiwa yazingatiwe kikamilifu na pande zote mbili (madaktari na serikali) ili kuepukana na mgomo huu ambao, strictly speaking it is barbaric and inhuman.

Kuhusu kuongeza starting salary ya daktari kutoka 0.9m/= to around 3.5m/= per month, ilitakiwa madaktari kama wasomi waelewe kuwa si Kikwete au hata serikali ina uwezo to effect such massive pay rise at the stroke of a pen. Na kama Kikwete aliwapa matumaini wakati wa mgomo uliopita kuwa, come July 2012, this will have been settled so resume duties, basi huo ulikuwa ni udhaifu mkubwa kwa upande wake na ambao hata hivyo usingetakiwa iwe sababu ya Watanzania walalahoi kufa na wengine mamilioni kutaabika kwa kukosa huduma ya afya kutokana na mgomo. Kwa upande mwingine, madaktari kama wasomi walitakiwa wafahamu kuwa serikali kama mwajiri wao na ambaye pia ni mwajiri wa wafanyakazi wengine wa serikali isingeweza kupandisha mshahara na marupurupu katika sector ya afya pekee - and particularly to affect physicians only - leaving out other cadres in the same sector like nurses, public health professionals, pharmacists, lab technicians, social workers and supporting staff.

Pili, ile dhana kuwa madaktari wanafanya kazi katika mazingira magumu hivyo wanatakiwa walipwe malipo maalum ya ziada sounds rather naive. Mafunzo wanayopata madaktari (au professionals wengine wowote) yana lengo la yawawafanya wawe experts katika fani yao. Sasa suala la mazingira magumu kwa madaktari halipo as medical jobs are not rated anywhere as among the most dangerous/risky jobs. Kadhalika kudai kwa nini TRA, BoT, etc., wanalipwa mishahara mikubwa haina mantiki kwa sababu schemes of service zao zinaruhusu.

Katika manpower hierarchy, first degree holders (kama madaktari general practitioners) wanakuwa katika kundi la middle management cadre hivyo kwa namna moja au nyingine wanahusika katika planning (kama budget preparation) katika maeneo yao ya kazi. Kama hawahusiki inputs za budget ya wizara ya afya zinatoka wapi? Hoja hapa ni kitendo chao kulalamika kutokuwa na adequate working tools na hivyo kuwa moja kati ya sababu ya wao kugoma. Labda hapa kuna tatizo ambalo ni universal katika nchi hii la budgetary constraints ambalo haliwezi kutatuliwa kwa kugoma.

Labda tutazame, kwa mazingira tulionayo, kama serikali ingetekeleza madai ya madktari kwa kuwaongezea mishahara kwa zaidi ya mara tatu nini kingetokea (kumbuka hatua hii ingehusisha pia kuwaongezea mishahara wafanyakazi wengine wa serikali kwa kiasi hicho hicho in line with the existing wage policies). Hii ingeongeza matumizi ya serikali kwa kiasi kikubwa (I cannot provide figures here) na hivyo ni dhahiri vyanzo vya mapato vilivyopo visingetosheleza. Hivyo serikali ingelazimika kukopa (au kuchapisha noti) in order to meet the new inflated wage bill. Kwa kuwa kuna utegemezi kati ya sector ya utoaji huduma na ile ile uzalishaji bidhaa katika nchi, hivyo gharama ya bidhaa ingepanda kwa kiasi hicho cha ongezeko la mishahara au zaidi. Wanauchumi wanaiita hii hali the wage/price spiral. Kwa vile hakuna ushahidi kuwa ongezeko la zaidi ya mara tatu katika mishahara litasababisha kuwepo na ongezeko kama hilo au zaidi katika tija (productivity) ya wafanyakazi, basi hicho ndicho kingekuwa kiama cha uchumi wa nchi kwa kusababisha spiral inflation ambayo ingeifanya Tanzania iwe kama Uganda wakati wa Idd Amin, Zaire wakati wa Mobutu au majuzi huko Zimbabwe ambapo kununua mkate unatakiwa kwenda dukani na kiroba kilichojaa noti. Kwa vile madaktari ni wasomi wangepaswa ku-research ili kufahamu adhari za utekelezaji wa madai yao kwa uchumi wa nchi kabla ya kuyatoa. Hii isingekuwa vigumu kwa sababu senior doctors wamesoma medical economics, so this information was well within the domain of the medical fraternity.

Mwisho nawashauri madaktari yafuatayo: call off the industrial action, resume your duties and go back to the drawing board. Consider this not a failed strike but a tactical retreat. Katika kudai ongezeko la mishahara siku zote fanyeni hivyo kitaalam kwa kudai salary increases that catch up with the rising costs of living as reflected by the Consumer Price Index (CPI).

Lakini ikumbukwe kuwa matatizo mengi ya kijamii na kiuchumi hapa nchini yanatokana na corrupt and ineffective (CCM) government. So while we are working on a new consititution, every one should be keen to show CCM the door, come 2015.
 
Mwalimu je anayelibwa 469,000 akikatwa PSPF, PAYE, HESLB, NHIF, CWT
anadaka 324,000 mnategemea nini? Tuzinduke!
Tatizo ya mitanzania minyonge inapingana yenyewe kwa yenyewe. Na hilo ni pepo la ubinafsi. Ni kama vichaa wanaosukumana kutoka kwenye mlango mmoja kwenye chumba kinachowaka moto. Kila mmoja anamvuta shati mwenzake asitangulie kutoka kabla yake. Siwaungi mkono moja kwa moja Drs,lakini siridhiki na mshahara wanaolipwa... Piga hesabu mtoto wako amenyeke miaka yote hiyo darasani,then aingie kwenye kazi ya kuchezea damu ya watu,akirisk maisha yake! Kwa kamshahara ka 0.9m???!!! Huku kuna jitu linagongagonga meza na kusinzia linalipwa mamillion!!!
 
nawashangaa sana wanao toa kigezo cha kusomeshwa bure, huwa watu kama hawa hawana point kabisa, kama bure ni ishu kwanini wao wasinge soma, wapuuzi kabisaaaaaaaaaaaaa
 
Mshahara wa Mbunge 2.5 Milioni, Madakatari wanataka 3.5Milion, Haiwezekani nawashauri wafanye analysis kama inawezekana, Kama kusoma Miaka 5 Hata lawyer wanasoma Miaka hiyo na mishahara mmewazidi, Halafu kama unasomei kitu ili kikulipe somea kitu kinacholipwa hakuna mtu aliyelazimishwa kusomea Udaktari,
Halafu mtueleze Madaktari Secta ya afya inaongoza kwa Rushwa na Wizi wa Madawa na Kuwaelekeza wagonjwa kwenye Maduka yenu mtalimalizaje hilo sion tu mnataka Mishahara mikubwa hamsemi yakwenu mtamalizaje

Saaaafiiii!

Hakuna aliyewalazimisha kusoma michepuo ya PBC, CBG, PCM na mingineyo, hayo yalikuwa ni mapenzi yao. Ina maana yawakujua kuwa kazi ya udaktari is risky? Huu ni utani, by virtue of profession, udaktari is risky, udereva, risky, ulinzi risky kufa anytime, polisi, jeshi, kulima ndo usiseme, nyoka, nge, jua, nvua, other chemical professionals pia. Hivi kila mtu akishika bendera "Kazi yangu is Risky" patakalika?

Madaktari acheni kutu-enjoy na kututesa, ipo siku mtalipa, kumbukeni Newton's third Law of Motion ' To every action, there is an equal and opposite reaction' Be prepared when the reaction equally but opposite na uhuni wenu itakapo kuja, wahenga walisema 'Kuimba kupokezana'
 
Hivi yeye Rais analipwa shilingi ngapi? Yeye na madaktari ni nani anayefanya kazi katika mazingira magumu? ***** zenu CCM
 
Inawezekana na ugali huli maana na mahindi hujayaona japo nimeyataja.
Na ni kweli tunaharibu mazingira sababu wewe na wenzio unaowatetea mnatupeleka huko na ndio sababu ya mgogoro
Na kwa sababu umenunuliwa/au ni sehemu ya tabaka kandamizi lazima ubofye gas na sijui kwa nini unajaribu kutuzuia na sisi kubofya gas kwa kauli zako dhalilifu na za dharau
 
Hakuna ugomvi wowote muajiri wako hana uwezo wa kukulipa huo mshahara unaoutaka...kwa hiyo mkilipwa 7,700,000 nchi ndio itakuwa tajiri? Hamna lolote eti mnasema mnawatetea wanyonge wakati kwenye madai 12 dai 1 tu ndio mmeomba vifaa vya kufanyia kazi madai yote 11 maslahi yenu binafsi...nendeni Ulaya au Amerika nasikia wanalipa vizuri.

Kweli ushabiki upofu!
Ukishajiweka upande wa tabaka kandamizi au ukabahatika kuwa huko by chance, unakuwa na maneno ya kejeli kama uliyotoa...eti nendeni ulaya!!!!
Nakuonea huruma sana sana maana nafsi yako inastahili huruma ndugu
 
Kimsingi hata me imenishangaza ila naona hy laki 9 ni baada ya deduction mkuu!wakiongezewa kila sector itaamka na kudai nyongeza ya mshahara hapa walipaswa kukaa pembeni wao wenyewe wakayamaliza!
Hebu fikiria mwalimu analipwa net pay ya 150 laki kaka hii imekaaje?na wao wagome?

Hapa serikali inaapaswa kuwakumbukaa waajiri wake kila mwaka kwa percent zinazokubalika lkn hili la ma daktari walitaka mkuu aseme hvy hvy!

Mkuu unajua hiyo laki 150 ni shilingi ngapi!?
 
Back
Top Bottom