Kinachotafutwa hapa ni madaktari kufanya kazi kwa moyo na sio utajiri, unajua huyo dokta angekuwa ameridhika angemtbu mgonjwa wako kwa moyo na labda angepona lakini kutokana na hali aliyo nayo akaopt kukuomba rushwa. Mimi siungi mkono mgomo lakini pia sikubaliani na serikali kutowaongezea angalau wapate moyo wa kufanya kazi. Cha muhimu mgomo ungeisha hata kwa kukubaliana na sio kulazimishana kwamba asiyetaka kazi na aache. HAPA WATAKAOUMIA NI WATU WA CHINI TU NA SIO RAIS KIKWETE, tunapaswa kujifunza kuilazimisha serikali itupatie huduma bora katika maeneo mbalimbaliHongera sana mkuu huo ndio wito tunaohitaji kuridhika na mshahara unaopewa, kuna Dr mmoja nilipeleka mgonjwa wangu akaniomba rushwa nikasema sina hela akaniambia sasa mbona umeniletea maiti? Na kweli nilikaa masaa 2 bila mgonjwa kuhudumiwa mpaka anafariki. Hawa madr wa mishahara bora wafukuzwe tu maana hawana msaada kwa wananchi wa kawaida, wakatafute kazi nje ya nchi kwetu hawatufai kabisa maana kama huna kitu kidogo ndio unazikwa hata kwa ugonjwa mdogo.
Leo katika hotuba ya Rais,alikua akitamka kwa sifa kua serikali inawalipa madaktari hela nyingi Tshs 900,000.Ila Laki tisa,ukikata PPF,PAYE inabaki kama TShs 550,000.Ukiangalia Dr anasoma miaka 5,anafanya kazi za riak kubwa sanaMbunge au waziri anapewa maslahi mazito sana,wengi hata ulinzi baada ya kustafu wanapewa.We unampa Dr mshahara net laki tano na nusu unategemea awe na umakini kwkazini.
eLFU 57,700/= ANAKATWA KULIPIA MKOPO ALIOKOPESHWA NA SERIKALIMshahara wa kuanzia dr mwenye first degree ni 957,700/= na sio 900,000/=. Na mwaka huu upatanda kuanzia kati ya 15% - 20%
Mbona unataka kuminyana na muajiri wako? Tatizo lipo wapi wewe tafuta sehemu wanaolipa mshahara mzuri kafanye kazi uko usiladhimishe ulipwe unavyotaka mkuu serikali aina huo uwezo...au nenda TMJ, Agha Khan, Regency, Hindu, kachukuwe mamilioni.HAPO NI Mil 1.050.000/= sasa mimi nikisema 900,000/=haitoshi hawanielewi kabisa...jameni hiyo haitoshi kabisa.....
duh!.......mishahara yenyewe ndo hio,kunakutoka kweli hapo?Dah hapo nipite tu mimi, maana ugomvi wa Panzi Furaha ya kunguru, Maana kada za Uhasibu hazitajwi sijui sisi ndo hatufanyi kazi katika mazingira hatarishi! Maana kitendo cha kukaa na Mamilioni ya Watu kila siku ni zaidi ya Mazingira hatarishi, Maana ukiziiba tu Unanye.a Kopo, Sijui na sisi tudai Allowance ipo? Maana iyo Tsh. 446,000/= tunayolipwa na ukikata kodi kinabaki kituko! Na hapo unataka mwanao asome International School.
Leo katika hotuba ya Rais,alikua akitamka kwa sifa kua serikali inawalipa madaktari hela nyingi Tshs 900,000.Ila Laki tisa,ukikata PPF,PAYE inabaki kama TShs 550,000.Ukiangalia Dr anasoma miaka 5,anafanya kazi za riak kubwa sanaMbunge au waziri anapewa maslahi mazito sana,wengi hata ulinzi baada ya kustafu wanapewa.We unampa Dr mshahara net laki tano na nusu unategemea awe na umakini kwkazini.
Kwa hiyo Ma Dr wakitimiziwa shida yao nchi itakalika?
Sina maana kuwa wao wapewe wanachodai. Nina maanisha kuwa huu ungekuwa wakati muafaka wa kuwaeleza na kuwashawishi WaTZ kwa ujumla kuwa matatizo ya mfumo yanashughulikiwa kwa dhati. Kuonyesha kwa vitendo maovu yanavyoshughulikiwa, waovu wanavyowajibishwa, upatikanaji wa haki unavyohangaikiwa.
Ubovu wa huduma za afya hauanzi kwa siki moja wala kutatuliwa kwa siku moja; Elimu bora haitajengwa kwa siku moja wala haikuanguka kwa siku moja. Kinachotakiwa kwa sasa ni kuonyesha kwa vitendo, nia ya dhati ya kushughulikia haya, na hii ni kwa ajili ya kutumaini kwamba Wa-TZ watawaelewa na kuvuta subira. Kadri wanavyochelewa kuyashughulikia kwa dhat ndivyo watu wanavyopoteza matumaini. Itakapofika hapo ndipo JANGA litakapokuja.
Kwa hiyo ndugu yangu maneno ya kwenye hutuba yangewekwa hayo maneno ungeridhika?
Hivi mnaelewa kwamba kuna madaktari wanavuta mpaka 5m na zaidi inategemea una miaka mingapi kazini.Vile vile nyumba au posho za nyumba wanapewa.Na rushwa hawaachi na wagonjwa hawawajali very sad....................,Daktari bingwa kama ndiyo kwanza ameajiriwa analipwa 1.5m! Kuna AMO wanalipwa zaidi ya hizo kutokana na miaka mingi kazini tangu wameajiriwa.eLFU 57,700/= ANAKATWA KULIPIA MKOPO ALIOKOPESHWA NA SERIKALI
Mbona Ma Dr hao hao kabla ya kugoma waliambiwa kua maswala yao yanashughulikiwa na wakagoma? mi hapa siafiki kusema kua maneno yatawafanya watu wavute subira.Sio suala la mimi kuridhika ndugu yangu. Ni suala la kutumaini kuwa wa-TZ wataelewa na kuvuta subira na kujenga matumaini ya serikali yao kushughulikia kero za muda mrefu.