Msemakweli akamatwa, ahojiwa Polisi; aachiwa

Asilimia kubwa ya hawa wate watakuwa wanasuport msemakweli kukamatwa
maana huyu jamaa kakabiziwa file feki litamtokea puani

There are currently 601 users browsing this thread. (171 members and 430 guests)
 
ʞontɹact Sniper;2439049 said:
Nimeahirisha....mimi pia katika kutoa mchango wangu nilkuwa najiandaa nijitokeze hadharani ili kupambana kwasababu ni ushahidi wa mambo mengi mazito........
Kumbe ningejitokeza na kukamatwa watu wangeishia kuajadili kwa keyboard tukio la mimi kukamatwa huku wakizidi kugawanyika kimtazamo??
Duh........mbaya zaidi ni kuwa tunapoongelea jambo tunaonekana kuwa ni timu moja yenye nguvu hasa, utekelezaji ukianza wengine hujificha nyuma ya migongo ya wenzao mithili ya mchezaji aliyechoka uwanjani anapozikwepa pasi kwa kujificha nyuma ya mpinzani wake ili asipasiwe.......watu wangeni support kwa message, wengine.......
Kwa kweli this is......ah...
Wewe umechukuwa hatuwa gani mpaka sasa hivi zaidi yakuwa upo hapa JF online? huu unaitwa unaitwa unafki.
 
Sasa wewe Kiritimba ... mbona unakosa heshima na hekima kwa pamoja!! Ni kitu gani kimekuudhi ktk ndoto yangu? Au kwa vile umejificha ktk jina la kiritimba? Watu wengine tunaweza tukawa baba kama si babu zenu? au ndugu? au tunakwenda msikiti mmoja? au jirani? au kanisa moja?

Hata hivyo kuvunjiana heshima namna hii haikusaidii kubaki na baraka zozote kutoka kwangu au kwa Allah au kwa Mungu wetu...Je umepata nini sasa kwa jibu lako hilo? Nakutakia raha ya matukano yako, ukae ukashibe kashfa na baraka za matusi yako. Mzee sn2139

nisamehe mkuu, nilikuelewa vibaya.
 
Inasikitisha kuona kwamba watanzania wako ktk hali mbaya ya umaskini, na tamko lilitolewa kuhusu mwenye evidences aziwakilishe ili kesi iweze kuendeshwa nafikili hiyo ni kutimiza lengo la kuishirikisha jamii katika ulinzi na usalama wa nchi yao, kwa kweli hakupaswa kushikwa kwa hilo bali anastahili kupongezwa,
Kwa yeyote atakaye pingana na hili ana nia yake ambayo kwa kweli sio nzuri na anatutia mashaka kama kweli ni mtanzania!!
What I can say, every thing in this world has its end and I believe no stone will remain unturned
 
Watanzania nafikiri tunatakiwa kutafuta a turning point. Kama serikali iliwaomba raia wake wawasilishe ushahidi dhidi ya Kagoda, akajitokeza mtu aliye na ushahidi badala ya kuuchambua na kufanya maamuzi ya kuutumia au kuuacha mnaamua kumpa kashikashi mtu mliyemuomba msaada huo.
Watanzania tukiipata hiyo turning point, tuka-flip everything na kuweza kuweka shinikizo hawa watu washitakiwe....na watashitakiwa. Msemakweli katupa mfano hapa na tunatakiwa kumuunga mkono hata kama serikali wakiamua kum-discourage.
 
wakuu sasa ni saa 11 kasoro na prof ulisema kwenye saa 10 utaleta updates zingine au ndio bongo yetu muda haufuatwi..
 
Lugha ya mawasiliano inatakiwa uwandike Brain. kingereza sio kigenzo cha usomi Kenya mpaka mataahira wanaongea kiingereza. pole sana young boy.

Labda kama hicho ni kingereza ambacho wewe ni muasis. Tengeneza kamusi yako kwanza halafu fanya jitihada za kushawishi.
 
hivi kuna issue kubwa yoyote inayolizunguka taifa kwa sasa? Maana unaweza kukuta ni smoke screen kuhamisha attention toka mahala fulani!
 
Jeykey leo kutwa nzima umeshinda kwenye keyboard, hujazalisha chochote Mpwa, hebu sasa nenda kapumzike bhana, waachie wengine wacomment pia, kha! ndio tuseme unajua sana au? au ndio umeajiriwa na hao jamaa kwa ajili ya kukanusha kila kinachozungumzwa humu? au are you paid kutokana na wingi wa posts unazotuma perday? unajaza server Mpwa, twende tukale nguruwe bhana, weekend ndio hii. Na bei ishapanda tena, Msemakweli muache sidhani kama anakuhusu sana unless anakugusa kwenye maslahi yako, twende zetu.
 
Hivi Jeykey muda ule wakati tunaongea ulisema ile kitimoto ya juzi ulikapata wapi pale? walikuuzia bei gani rost ndizi? nikumbushe mie ndio naondoka hapa ofisini sasa, weekend njema jamani, and take good care of yourself, ukipigwa kibuti uje utujulishe tukufariji pia.
 
CHADEMA mmemponza MsemaUWONGO, yeye kapewa faili pasipo kufanyia kazi, SASA cha moto atakiona kwani huo ni uchochezi nchi yetu ya amani. Hatutaki kupewa taarifa bila kufanya uchunguzi wa kina.

Nyie wachangiaji wengine mna ubaguzi wa rangi, HAKUNA SABABU YA KUWAHUKUMU MANJI NA ROSTAM; ACHENI SIASA UCHWARA!!!

Uchunguzi gani unasubiri wewe unazidi kuwapandisha watu hasira, sasa subiri wakati ukifika tukutane huko kwenye kona. hata waliokuwa wanamtetea Ghadaffi waliuwana wenyewe kwa wenyewe kabla waasi hawajawafikia.

Hakuna wa kumgusa msemakweli tupo tutapambana. Ni haki yake kutoa dukuduku lake mahali ambapo atapata haki yake. Kaamua kwenda mahakamani hao polisi kiherehere wanamkamata, kaiba au kafanya nini. Hawana kazi ya kufanya hao wapewe kazi ya kulima bustani kule ukonga.
 
Labda kama hicho ni kingereza ambacho wewe ni muasis. Tengeneza kamusi yako kwanza halafu fanya jitihada za kushawishi.
Anyway kuna jukwaa la lugha hapa JF kama unadhani wewe ni mahili wa Lugha nenda kule utakutana na wenzako, hili ni jukwaa la siasa. PERIOD.
 
daaah hii nchi bana.. ngoja nikalipe kodi kwenye bia sasa! najua hata hiyo kodi wataifisadi ila ndio sina jinsi
 
Back
Top Bottom