yatima wa kitanzania
Member
- Jan 4, 2016
- 53
- 11
Kwa wazee wetu Bazil mlamba na D yona. Kuna somo kwa mawaziri wa sasa
Mawaziri wa zamani Basil Mramba na Daniel Yona wameripoti katika hospitali ya Sinza Palestina na kukabiziwa vifaa kwa ajili ya kufanya usafi.
View attachment 321837
View attachment 321844
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliridhia waliokuwa Mawaziri wastaafu Basil Mramba na Daniel Yona kutumikia adhabu ya kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika maeneo ya kijamii ikiwemo Hospitali ya Sinza Palestina.
Hatua hiyo inatokana na Mramba ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, kupitia Mawakili wao kuwasilisha barua mahakamani hapo kutoka Magereza kuhusu kutumikia kifungo cha nje.
Mawaziri hao, Jul 6, 2015, walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh milioni tano, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.
Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani mwaka 2008, wakikabiliwa na mashtaka ya kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.
Tukitaka tuelewe zaidi tujiulize je kama wafanyakazi hatujawahi kufanya errors katika kutoa maamuzi yetu?!?!?
nashangaa kwanini Mkapa wamemuweka mbali na hizi tuhuma anyway,ccm ya majipu,magamba n.k since 1995 tunaongozwa kwa mizaha na matukioAcha ifikie hapo, pamoja na makosa yao yapo pia waliyoyafanya mazuri enzi zao.
Wachukue uzoefu mwaka 2020 watajiunga kudeki bsrabara za wagombea urais wa vyama watakavyo viunga mkono.Daaah! Natamani niwaone wakiinama na kudeki, hivi hawaruhusiwi kuajiri watu wa kuwasaidia kufanya usafi?
Hatua hiyo inatokana na Mramba ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, kupitia Mawakili wao kuwasilisha barua mahakamani hapo kutoka Magereza kuhusu kutumikia kifungo cha nje.
Mawaziri hao, Jul 6, 2015, walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh milioni tano, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.
Daaah! Natamani niwaone wakiinama na kudeki, hivi hawaruhusiwi kuajiri watu wa kuwasaidia kufanya usafi?
Mazuri waliyofanya ni mengi kuliko hilo walilohukumiwa nalo. Kuna wengi wapo njee wameliibia taifa huku akilindwa na chama pamoja na mfumo.Acha ifikie hapo, pamoja na makosa yao yapo pia waliyoyafanya mazuri enzi zao.
Wao wanafanya masaa ma4 tu kwa siku. Tumia akili yako vizuri!Mimi nikifika hapo nachafua kila waliposafisha.....ili wasafishe kutwa nzima.....