kumbe na wewe ni walewale tu vizalia vya mafisadi. endeleeni na upuuzi wenu huo.Acha ifikie hapo, pamoja na makosa yao yapo pia waliyoyafanya mazuri enzi zao.
Ha ha haaa h joka lenye makengeza linalosaka pesa.wao waliiba wakaacha traces,wamuulize chenge huwa anafanya nini mpaka hatiwi hatiani?joka lenye mabichwa saba
halijawahi onja cello,ila mapesa yanayozaa maswali maswali linayoHa ha haaa h joka lenye makengeza linalosaka pesa.
Mawaziri wa zamani Basil Mramba na Daniel Yona wameripoti katika hospitali ya Sinza Palestina na kukabiziwa vifaa kwa ajili ya kufanya usafi.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliridhia waliokuwa Mawaziri wastaafu Basil Mramba na Daniel Yona kutumikia adhabu ya kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika maeneo ya kijamii ikiwemo Hospitali ya Sinza Palestina.
Hatua hiyo inatokana na Mramba ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, kupitia Mawakili wao kuwasilisha barua mahakamani hapo kutoka Magereza kuhusu kutumikia kifungo cha nje.
Mawaziri hao, Jul 6, 2015, walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh milioni tano, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.
Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani mwaka 2008, wakikabiliwa na mashtaka ya kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.
Ngoja waliokunywa maji ya kijani waje utatukanwaje?Kumbe we ulijua pale watafanya kweli kama inavostahili? Wapumbavu wachache ndio wanaamini kuwa ccm ina nia ya dhati kupambana na mafisadi.. Embu ona watu waizi ila wamefungwa miaka 3 alafu usafi wenyewe siku 3
Enzi za Mkapa uchumi wetu ulikuwa imara...? Hivi tulirank wa ngapi kwa Umaskini? na usikute nawe unajiita msomi, ptyuuuuuuuNi sawa tu... Hawa hata kama walituibia walijenga uchumi imara enzi za Mkapa na ndio vilikuwa vyichwa vyake..
Hawa walioharibu uchumi wetu na ufisadi kutamalaki enzi za JK kuanzia Richmond mpaka Escrow mbona wanakula kuku tu mtaani?? Tena na matusi walitutukana kabisa...