Mramba na Yona, Wakabidhiwa vifaa vya usafi Hospitali ya Palestina

Ni sawa tu... Hawa hata kama walituibia walijenga uchumi imara enzi za Mkapa na ndio vilikuwa vyichwa vyake..

Hawa walioharibu uchumi wetu na ufisadi kutamalaki enzi za JK kuanzia Richmond mpaka Escrow mbona wanakula kuku tu mtaani?? Tena na matusi walitutukana kabisa...
Hii coment imenihuzunisha sana
 
Enzi za Mkapa uchumi wetu ulikuwa imara...? Hivi tulirank wa ngapi kwa Umaskini? na usikute nawe unajiita msomi, ptyuuuuuuu
Mkapa alichukua nchi uchumi ukiwa unakuwa kwa asilimia 4 na kuuacha ukiwa unakuwa kwa asilimia 7 unakimbilia 8.. Inflation rate ya single digit tangia anachukua nchi mpaka anaondoka madarakani, Shillingi kwa Dolla ilikua imara wakati wote, aliondoka Shillingi ikiwa 1150 kwa Dolla (Tanzania Shilling | 2003-2016 | Data | Chart | Calendar | Forecast | News) JK ameichukua hapo kaiacha 2200.. Kauchukua Uchumi ukikua asilimia 7 kukimbilia 8 kauacha unakuwa asilimia 7 hizo hizo.. Mkapa aliweka foundation nyingi sana ambazo zingaipeleka Tanzania mbele sana, miradi kama ya Mtwara Corridor na kufua umeme kutoka Mto Rufiki... Yote hii iliuliwa na JK... Kwa kukuelewesha zaidi, kama Mtwara Corridor ingekamilishwa leo hii Bandari ya Mtwara ingekuwa inahudumia nchi za Malawi, Kaskazini mwa Msumbiji na miji ya kusini ya Kongo acha biashara ya Chuma cha Liganda na Makaa ya Mawe..

Kwa kukupa darasa dogo tu kijana, kama 2005 nchi ingechukuliwa na Rais aliye serious kama hata huyu Magufuli, leo hii tungekuwa tunashindana na super powers wa Afrika kama SA na Nigeria na sio kelele za kuwafukuzia Wakenya..
 
Back
Top Bottom