Kikwete aliwafunga Mramba na Yona kwa Ufisadi, Magufuli alimfunga nani kwa ufisadi?

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,836
Kikwete aliwafunga mawaziri katika serikali ya Mkapa, Basil Mramba na Daniel Yona, hawa walikuwa viongozi wakubwa

Magufuli anasemwa alipambana na ufisadi na Serikali ya Kikwete ilisemwa sana na Magufuli kuwa ilikuwa na mafisadi, je ni kiongozi yupi katika serikali alifungwa kwa ufisadi na Magufuli?
 
Siku za karibuni JF imevamiwa na vichwa panzi wa kutosha...Mramba na Yona walihukumiwa kifungo cha nje na kufanya kazi ya usafi...hii nayo utasema ni adhabu? Hii hukumu was a joke considering makosa waliyofanya...watu walisababisha hasara ya Billioni 11.7 wakahukumiwa kufanya usafi...it was better of wangeaachia huru kuliko kutudharau wanainchi. Then kuna mbuzi inaibuka kutoka malishoni inasema kua Mramba na Yona walifungwa, walifungwa Gereza lipi?
 
Kikwete aliwafunga mawaziri katika serikali ya Mkapa, Basil Mramba na Daniel Yona, hawa walikuwa viongozi wakubwa

Magufuli anasemwa alipambana na ufisadi na Serikali ya Kikwete ilisemwa sana na Magufuli kuwa ilikuwa na mafisadi, je ni kiongozi yupi katika serikali alifungwa kwa ufisadi na Magufuli?
Plea bargaine
 
Siku za karibuni JF imevamiwa na vichwa panzi wa kutosha...Mramba na Yona walihukumiwa kifungo cha nje na kufanya kazi ya usafi...hii nayo utasema ni adhabu? Hii hukumu was joke considering makosa waliyofanya...watu walisababisha hasara ya Billioni 11.7 wakahukumiwa kufanya usafi...it was better of wangeaachia huru kuliko kutudharau wanainchi. Then kuna mbuzi inaibuka kutoka malishoni isema kua Mramba na Yona walifungwa, walifungwa Gereza lipi?
Wanasema Msoga aliambiwa Mnadhimu ana Tzs 3trillion, kaziweka SA. Wanasema ni baada ya hali mbaya ya kifedha serikali iliyokuwa nayo wakati huo baada ya kutumia pesa zote kwenye kuadhimisha sherehe ya miaka 50 ya uhuru, akakosa pesa za mishahara, akaenda kukopa, wakamjuza asiyoyajua, akashindwa kufanya lolote, pengine naye akaomba mgao wake.

Huwa kuna maswali unaweza kujaribu kutafuta majibu, ukaishia kucheka kwa kuhuzunika;

Yule aliyeiba dola 2,000,000 na kukamatiwa Mbeya, alifungwaje?

Liyumba?

Dege beach, ilikuaje?

Magu na Kijazi kuondolewa wizara ya ujenzi, nini ilikuwa shida? Dau alifanya nini? Amefanywa nini?

Chenge na Radar?

Richmond? Dowans, Symbion, Aggreko, Songas?

Tan gold, Green bird?

Wachina kuingia ovyo nchini?

TASAF?

Kilimo kwanza?

Pouda, papaa nani sijui, nani kule?

Liganga na Mchuchuma?

Machimbo ya dhahabu Chunya?

Helium?

Mikataba ya gesi kwa dharula?

Mmiliki wa mashirika ambayo serikali ilikuwa na 51% ya share yakoje kwa sasa?

Shule za kata, zina matokeo chanya mpaka sasa?

n.k
 
UFISADI WA RICHMOND ULIFANYIKA KIPINDI CHA KIKWETE,LKN LUGEMALILA NA SETH ALIWAKAMATA JPM,WAKIWA KTK MWENDELEZO WA TUHUMA ZAO,JPM AKAONDOLEWA,( NA KWA TAARIFA ZILIZOPO NI KUWA SETH NA LUGEMALILA WALIJUA KINACHOENDELEA NJE KUHUSU JPM NDIO MAANA WAO WALIGOMA KUKIRI) KAMA JPM ANGEKUWA HAI,LEO TUNGEKUWA TUNAONGEA MENGINE
 
Kikwete aliwafunga mawaziri katika serikali ya Mkapa, Basil Mramba na Daniel Yona, hawa walikuwa viongozi wakubwa

Magufuli anasemwa alipambana na ufisadi na Serikali ya Kikwete ilisemwa sana na Magufuli kuwa ilikuwa na mafisadi, je ni kiongozi yupi katika serikali alifungwa kwa ufisadi na Magufuli?
Awamu ya tano makosa ya kubambikiza ya ufisadi, uhujumu uchumi, utakatishaji fedha, nk yalitumika kupora watu fedha zao. Watu walifungwa magereza bila mashauri yao kupelelezwa na badala yake walifuatwa huko na waendesha mashtaka kutakiwa kukiri makosa na kununua uhuru wao.
 
Siku za karibuni JF imevamiwa na vichwa panzi wa kutosha...Mramba na Yona walihukumiwa kifungo cha nje na kufanya kazi ya usafi...hii nayo utasema ni adhabu? Hii hukumu was joke considering makosa waliyofanya...watu walisababisha hasara ya Billioni 11.7 wakahukumiwa kufanya usafi...it was better of wangeaachia huru kuliko kutudharau wanainchi. Then kuna mbuzi inaibuka kutoka malishoni isema kua Mramba na Yona walifungwa, walifungwa Gereza lipi?
Hahahaa, nyie watu mtakuwa vichaa mwaka huu, sasa Magufuli alimfunga kiongozi gani hata kifungo cha nje? Au kumpeleka hata mahakamani tu
 
Wanasema Msoga aliambiwa Mnadhimu ana Tzs 3trillion, kaziweka SA. Wanasema ni baada ya hali mbaya ya kifedha serikali iliyokuwa nayo wakati huo baada ya kutumia pesa zote kwenye kuadhimisha sherehe ya miaka 50 ya uhuru, akakosa pesa za mishahara, akaenda kukopa, wakamjuza asiyoyajua, akashindwa kufanya lolote, pengine naye akaomba mgao wake.

Huwa kuna maswali unaweza kujaribu kutafuta majibu, ukaishia kucheka kwa kuhuzunika;

Yule aliyeiba dola 2,000,000 na kukamatiwa Mbeya, alifungwaje?

Liyumba?

Dege beach, ilikuaje?

Magu na Kijazi kuondolewa wizara ya ujenzi, nini ilikuwa shida? Dau alifanya nini? Amefanywa nini?

Chenge na Radar?

Richmond? Dowans, Symbion, Aggreko, Songas?

Tan gold, Green bird?

Wachina kuingia ovyo nchini?

TASAF?

Kilimo kwanza?

Pouda, papaa nani sijui, nani kule?

Liganga na Mchuchuma?

Machimbo ya dhahabu Chunya?

Helium?

Mikataba ya gesi kwa dharula?

Mmiliki wa mashirika ambayo serikali ilikuwa na 51% ya share yakoje kwa sasa?

Shule za kata, zina matokeo chanya mpaka sasa?

n.k
Sasa ufisadi wote huo na Magufuli hakuweza kumfunga hata mmoja kweli? Au alikuwa mmoja wao?
 
Wote hawana tofauti maana fisadi lazima arudishe alicho iba sasa yupi kati yao aliweza kurudisha mali ilio ibiwa na fisadi?.
 
Kikwete aliwafunga mawaziri katika serikali ya Mkapa, Basil Mramba na Daniel Yona, hawa walikuwa viongozi wakubwa

Magufuli anasemwa alipambana na ufisadi na Serikali ya Kikwete ilisemwa sana na Magufuli kuwa ilikuwa na mafisadi, je ni kiongozi yupi katika serikali alifungwa kwa ufisadi na Magufuli?
Ukweli usemwe. JPM Aliwashika watu pabaya. Manake pamoja na kufariki miaka kadhaa iliyopita bado anazungumziwa, yani watu ambao wako hai wanashindana na mfu na bado wanashindwa!

Marehemu Mzee Reginald Mengi aliwahi kusema, nanukuu, "hakuna uwekezaji mkubwa hapa duniani kama kuwekeza kwa watu, kwasababu hata ukifa utaendelea kuishi mioyoni mwao", mwisho wa kunukuu.

Hiki ndiyo kinachoteka kwa Magufuli. Anaishi mioyoni mwa watu.

Povu ruksa ..
 
Back
Top Bottom