Mnyika huwezi vita binafsi na Kikwete

Wewe bila shaka utakuwa na utindio wa ubongo, nini maana ya udhaifu? wangemuacha aendelee nadhani mngepata majibu yote. alafu acha kujiwekea dhana eti ukiwa mwana ccm wewe ndio una uchungu kuliko watu wote kwenye hii nchi, eti vita? unaijua vita au unasema tu for the sake of speaking. Alichokisema Mnyika ndio kauli za Watanzania kwa jinsi wanavyomuona Kikwete sasa eti unatoa vitisho unaonyesha jinsi gani ulivyo shallow minded. Alafu nikufahamishe tu likivurugika aitakuwa Mnyika itakuwa ni ccm na wananchi na nadhani sote tunajua watakaopoteza niwakinanani kwani mwananchi asiye na kitu hana shida ila viongozi waliokuwa madarakani ndio watatafuta mahali pa kujificha na hizo A/C zao walizoweka nje usifikiri likivurugiga watu hawajui namna ya kuzuia hizo fedha au mali walizonazo. kuwa makini na kauli unazotoa iko siku zitakukosti
Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".

Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.

Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".

Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?

Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.

Kikwete humuwezi.
 
Mnyika ameharibia watoto wetu wanaofuatilia kwa makini Bunge kwa lengo la kujifunza jinsi wawakilishi wetu wanavyoongea na kuijadili bajeti.

Pamoja na kufurahia bunge, watoto pia wanajifunza jinsi watakavyoongea wakikua iwapo wataamua kuingia kwenye siasa.

Walichojifunza kwa huyu mpuuzi Mnyika ni jinsi ya kuwatukana baba zao hadharani.

Aibu sana, nimewapiga marufuku wanangu kuangalia kipindi cha Bunge ....until further notice.

Kwa nini usiwahamishe kabisa nchi hii? Mnyika ataendelea kuwepo na ukweli atausema tu na hao watoto hawatausikia wakiwa hapo nyumbani kwako lakini wakienda mtaani watauona ukweli wenyewe.
 
Jamaa dhaifu sana huyu ona ahadi zake - alitoa akiwa wapi......

1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36. Kulinda haki za walemavu - Makete
37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha

Halafu kuna mtu humu anasimama kwa nguvu zake zote kusema JK ni rais!!!!! Sasa hapa utasema Mnyika amepotoka...kweli....!!!
 
Wewe anza kwa kuonesha ni lipi la maendeleo alilofanya Rais yeyote wa kabla yake, ambalo yeye hajafanya zaidi.

Mnaleta matusi na ktukana lakini hoja za wazi kabisa zinawashinda. Mnyika kashindwa hoja ya bajeti akaamuwa awatukane wabunge wote, wana CCM wote na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Namwambia hvi; Kikwete asimjaribu, hamuwezi hata kidogo.

Ufanisi au udhaifu (ingawa neno hilo limeonekana ni tusi) wa Rais Kikwete hauwezi kupimwa marais wengine waliomtangulia walifanya au hawakufanya nini. Every epoch has got its own overturns. Nimefuatilia unatoa mifano ya vitu kila mara kiasi kwamba unapitiliza maana unatuhesabia mara nyingi vyuo vikuu vilivyojengwa sasa hivi lakini mara nyingi hutaki kutuambia msingi wa hivyo vyuo.

Itakuwa ni kichekesho ukisema serkali ya Mwalimu haikujenga vyuo kama ya Kikwete ingawa si kweli kuwa Kikwete ndiye kajenga vyuo hivi labda Dodoma still questinable on quality wakati hata primary school zilikuwa za kuhesabu wakati nchi inapata uhuru. Msingi kwanza halafu ndio unajenga nyumba.

Sasa turudi kwenye mada Rais Kikwete atahukumiwa kwa yale aliyopaswa kuyafanya na hajayafanya lakini si yale unayotaka kulazimisha watu wayaone. Kama yapo watu watapiga makofi kama hayapo watu watalalamika tu. Bajeti ambayo imekuwa chanzo cha yote imesemwa na wanauchumi waliobobea kuwa haina kipaumbele kwa mtu masikini maana bado inawakumbatia wenye pesa tena wageni.

Misamaha kwenye uwekezaji wa madini imekuwa donda ndugu? Sikutegemea misaada iendelee tena kwenye mafuta mazito ya mitambo na magari kwenye uwekezaji wa madini. Hivi hili linahitaji uende shule ya wapi? Exemptions on import and corporate taxes na unabaki kukodolea macho mrahaba wa 4% halafu mnataka wananchi waendelee kuwashangilia.

Tanzanians are not intellectual zombies Zomba. Wana akili na wanaona watu wanavyokula bila kunawa. So ingawa neno dhaifu limeoneka na zito mno lakini tunachopaswa kuangalia ni policies zipi zinatungwa na kwa faida ya nani. Kama sio kwa maslahi ya wengi ni kuamsha jazba na mifarakano. Usilazimishe kama Mwigulu Mchemba mwanauchumi daraja la kwnza lakini asiweza kutofautisha kati ya development budget na recurrent expediture
 
Unajifanya hujui kwamba raisi wako ni dhaifu tena sana?
Mnyika amewasaidia tu kuwasemea, hata wanaccm wengi wamefurahi, walikuwa wanaishia na kigugumizi.
Huyo raisi hajachaguliwa na Watanzania wote, ni wewe na wanaccm ambao hawaoni mbali.
Raisi ni dhaifu na ameshindwa kushughulikia wezi wengi tu hasa wale ndani ya chama chako, kwa maana hiyo hawamudu.
Hiyo vita unayotangaza sasa na Mnyika dhidi ya ccm hujui ilianza siku nyingi tangu Mnyika alipoingia upinzani? Hujui kwamba tangia wakati huo yuko against ccm?
 
Halafu kuna mtu humu anasimama kwa nguvu zake zote kusema JK ni rais!!!!! Sasa hapa utasema Mnyika amepotoka...kweli....!!!

Mbona na yeye mnyika kwake ubungo ametowa ahadi tele na hajazitekeleza? na yeye tumuite Mbunge mwenye akili kweli? ! ameacha mpaka barabara zake zimeota bangi kama kichwa chake!
 
Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".

Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.

Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".

Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?

Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.

Kikwete humuwezi.

Loh Mnyika yupo sahihi kabisa. Kikwete ni DHAIFU.

Mnyika ni JASIRI hasa pale alipokataa kufuta kauli yake.

Udhaifu na Ujasiri ni sifa wala siyo matusi, kejeli au vinginevyo. Udhaifu ni sifa hasi ambayo ndiyo stahiki ya sifa ya Kikwete kwa watanzania wengi ikiwa ni pamoja na bibi yangu mzaa mama.

Naibu spika alipindisha maneno na kutoa tafsiri potofu ya neno dhaifu, ingefaa atoe tafsiri ya neno dhaifu katika muktadha uliotumika. JeMnyika ange tolewa nje ya eneo la bunge kama angempa sifa asiyo stahiki?

Mnyika, umenifurahisha kweli kweli, umetoa sifa zake, hukukejeli wala kurukana.
 
Hivi unadhani CDM tulifurahia pale mlipomuita mwenyekiti wetu wa chama kuwa ni DJ? Pia mnadhani tulifurahia mliposema Slaa ana awara tena mbele ya majukwaa?
Pia eleweni hata Mnyika hakukosea aliposema JK ni dhaifu na msilalamike bure maana mkuki kwa Nguruwe huo?.

BIG UP MNYIKA.
 
Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine? Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu. Kikwete humuwezi.
Mimi nashangaa sana wa JF kama kuna watu wanaoogopa kusema mtu ni dhaifu,unajua rafiki yangu kumuambia mtu ni dhaifu sio TUSI,hata kidogo na kama umewahi kwenda kwenye interview nyingi za kazi huwa watu wanaulizwa swali la kuelezea udhaifu wako na strength!!hakuna mtu aliye 100% perfect,kikubwa hapa ambacho nyie msio na uwezo wa kuchambua mambo mnajikanyaga kanyaga hapa ni kwamba alitakiwa atoe maelezo kwa nini amesema Rais ni dhaifu!!!as you know rais ni taasisi and is not necessarily alikuwa anamtargate Kikwete as an indiviadual,so kosa hapa ni kwamba alitakiwa atoe maelezo kwa nini alitumia neno udhaifu ambalo walimkataza,so kosa ni la NAIBU SPIKA NA SISIEM yake ya wakina mchemba,personally i respect Mnyika na huwa napenda sana kumsikiliza kila anaposimama kuongea na sio mtu wa kukurupuka nadhani mumemuelewa visivyo,apewe time ajieleze nadhani mtamkubali kuwa hajakosea kusema hivyo
 
Nani asiyejua CCM kwa majungu, kulipana kisasi, na visirani...mambo sasa yamebadilika, hamwezi kufanya kama mnavyotaka. Siasa za ubabe zimefika mwisho!
 
Akiishiwa hoja ataanza kutukana! orodhesha na ya mnyika hapa usirukeruke!

Tumia akili wewe hata za jirani yako. Mnyika hana bajeti binafsi na hana dola wala funguo za rasilimali za nchi hii. Mapato yanasimamiwa na wapuuzi kwa hiyo jambo pekee analotakiwa kufanya ni kupiga kelele na kusema ukweli. Kuhimiza na kusisitiza leo na kesho kama anavyofanya kuhusu suala la maji.

Kama unafikiri Mnyika anaongoza Igunga ambako wanaahidiwa mahindi na ya serikali kupitia CCM na wao wanaona kweli yametoka CCM basi umeurop, Ubungo ina wajinga wachache sana ukilinganisha na the rest of the country na ndio maana Mnyika ni mbunge wetu na DHAIFU alipata kura kiduchu huku.

Hata hii ya kutunyima bulldozer la manispaa na kutuambia lipo bize kila leo ni kutukomoa tu kwa kuwa DHAIFU alimleta mama mmoja wa Kipare na sisi tukamdunda KNOCK OUT kwenye sanduku la kura.

Walioishiwa hoja ni wale wanaoanza kwa kulalama kuwa majimbo yao yamesahaulika na bajeti hazitoshi lkn wanamaliza kwa kusema wanaunga mkono hoja kwa ailimia 100. ROBOTS (tuned to sing that song)
 
Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".

Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.

Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".

Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?

Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.

Kikwete humuwezi.

Hakuna vita binafsi kati ya mnyika na jk.wewe mpuuzi unaona ni vita binafsi,mnyika analengo la kuisimamia serikali dhaifu.
 
Mbona na yeye mnyika kwake ubungo ametowa ahadi tele na hajazitekeleza? na yeye tumuite Mbunge mwenye akili kweli? ! ameacha mpaka barabara zake zimeota bangi kama kichwa chake!

Kwa hiyo ahadi za mbunge wa miaka 3 ndani ya uongozi unataka kufananisha na ahadi za rais aliyeko madarakani kwa miaka 8! Siyo?
 
Kiukweli kwa kipaji hiki, Mnyika hamuwezi JK kabisaaaaa


JK.jpg

naona antandika ngoma ya Burundi...au ya Rwanda!!
 
(((((((((((((((((Mnyikaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa)))))))))))))))
(((((((((((((you have Open another door)))))))))))
 
Back
Top Bottom