kenethedmund
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 347
- 89
Wewe bila shaka utakuwa na utindio wa ubongo, nini maana ya udhaifu? wangemuacha aendelee nadhani mngepata majibu yote. alafu acha kujiwekea dhana eti ukiwa mwana ccm wewe ndio una uchungu kuliko watu wote kwenye hii nchi, eti vita? unaijua vita au unasema tu for the sake of speaking. Alichokisema Mnyika ndio kauli za Watanzania kwa jinsi wanavyomuona Kikwete sasa eti unatoa vitisho unaonyesha jinsi gani ulivyo shallow minded. Alafu nikufahamishe tu likivurugika aitakuwa Mnyika itakuwa ni ccm na wananchi na nadhani sote tunajua watakaopoteza niwakinanani kwani mwananchi asiye na kitu hana shida ila viongozi waliokuwa madarakani ndio watatafuta mahali pa kujificha na hizo A/C zao walizoweka nje usifikiri likivurugiga watu hawajui namna ya kuzuia hizo fedha au mali walizonazo. kuwa makini na kauli unazotoa iko siku zitakukosti
Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".
Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.
Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".
Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?
Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.
Kikwete humuwezi.