Nimefurahi kujua mkeo ana vitz.Sijakosea jukwaa maana kuna walioanza kununa, mwezenu nyumbani kumeanza kuwa kuchungu baada ya wifi yenu kuanza visa baada ya vikao vya bunge kuanza. Wiki ya kwanza alianza kama utani eti anataka kupendekeza baba kivuli ili awe ananikosoa na kutoa mtazamo mbadala kwa masuala yetu pale nyumbani. Hili nililipinga kwa nguvu zote kwa kuwa sikuwa na uhakika na hadidu za rejea za baba kivuli, wiki iliyofuata akaanza kupinga posho zangu na misafara mikubwa ya marafiki ninapokwenda bar. Nikidhani itaishia hapo sasa baada kiongozi wa upinzani bungeni kurudisha shangingi lake, yeye sasa ndio amekuja na kali eti anataka kupiga bei ka vitz kake ili tuwe tunapanda gari moja kwenda na kurudi kazini sasa mimi hapo naona kama uhuru wangu unaelekea kunitupa mkono, Nifanyeje wandugu kwa hatua za mwanzo nimepiga marufuku bunge nyumbani kwangu.
Tatizo ni huko kubana matumizi kunakoingilia uhuru wangu bana, nilikuwa nitoka kazini napaki pale New Afrika hotel wakati wa Happy Hour sasa hivi hii yote itapeperuka halafu kuna dada jirani nilikuwa namsaidia sana lifti maana yeye ndio kaanza tu kazi sasa wife si atakuwa anambana.
Nimefurahi kujua mkeo ana vitz.
Ecoli aliyekwambia ukioa unabaki na uhuru wako ni nani??
Uzuri wa baba kivuli, si lazima awe na pesa....ukiwa mwongeaji mzuri na kupangilia hoja zako vizuri kama afanyavyo Mbowe, inshallah unatunukiwa nafasi.........Hebu nijaribu tuone.babu mi ndo nafanya shortlisting ya baba kivuli hapa, kivuli chako kina urefu na upana wa kutosha kukinga jua na mwezi 24/7?
Uzuri wa baba kivuli, si lazima awe na pesa....ukiwa mwongeaji mzuri na kupangilia hoja zako vizuri kama afanyavyo Mbowe, inshallah unatunukiwa nafasi.........Hebu nijaribu tuone.
Ni kwanini lakini uhuru wa "katiba" yangu maishani lazima tu uchakachuliwe kwa kisingizio cha "muafaka" wa ndoa (serikali mseto)?!Ecoli aliyekwambia ukioa unabaki na uhuru wako ni nani??
Ni kwanini lakini uhuru wa "katiba" yangu maishani lazima tu uchakachuliwe kwa kisingizio cha "muafaka" wa ndoa (serikali mseto)?!
Sijakosea jukwaa maana kuna walioanza kununa, mwezenu nyumbani kumeanza kuwa kuchungu baada ya wifi yenu kuanza visa baada ya vikao vya bunge kuanza. Wiki ya kwanza alianza kama utani eti anataka kupendekeza baba kivuli ili awe ananikosoa na kutoa mtazamo mbadala kwa masuala yetu pale nyumbani. Hili nililipinga kwa nguvu zote kwa kuwa sikuwa na uhakika na hadidu za rejea za baba kivuli, wiki iliyofuata akaanza kupinga posho zangu na misafara mikubwa ya marafiki ninapokwenda bar. Nikidhani itaishia hapo sasa baada kiongozi wa upinzani bungeni kurudisha shangingi lake, yeye sasa ndio amekuja na kali eti anataka kupiga bei ka vitz kake ili tuwe tunapanda gari moja kwenda na kurudi kazini sasa mimi hapo naona kama uhuru wangu unaelekea kunitupa mkono, Nifanyeje wandugu kwa hatua za mwanzo nimepiga marufuku bunge nyumbani kwangu.
Should I keep waiting?kwa hiyo qualification yako ni pennyless na maneno kibao? hakuna majaribio hapa babu,job agency inahuika