Faruku Mhamadi: Mke wangu alinichoma kisu nikiwa usingizini

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Oct 21, 2021
4,718
11,068
Dah inasikitisha sana bwana faruq kutoka Muleba alikuwa akihojiwa leo asubuhi katika channel ya crouds kiukweli ni kuwa wanawake wa kileo wana roho mbaya sanašŸ˜¢

======

Faruku.PNG

Faruku Muhamadi

"Nilipata maswahibu ya kuchomwa kisu na mke wangu. Nilikuwa nimelala na haukuwepo ugomvi au ilikuwa tunapigana hapana... Nilikuwa usingizini akazamisha kisu tumboni mwangu na akaanza kuchana tumbo. Alianzia kwenye chembe ya Moyo akachana mpaka chini. Niliposhtuka usingizini nikakikuta kile kisu kipo tumboni kwangu. Nilimuuliza mke wangu vipi kulikoni?

Akaniambia Leo ndio mwisho wako! Akachomoa kile kisu akataka kunichoma tena shingoni. Nilipoona hivyo nilijikaza nikaamka kitandani. Ilikuwa ni Saa 10 Alfajiri. Mapambano yalikuwa Makali Sana"

"Namshukuru Mungu ni Mkubwa alinisimamia hadi tunaongea leo. Wakati tunapambana pale kitandani yeye alianguka chini. Na wakati huo majirani walikuwa wameshafika na kuizunguka nyumba. Kutokana na kelele nilizokuwa nikipigia" Faruku Mhamadi, Mkazi wa mkoa wa Kagera.

Alitaka kukimbia na utumbo
"Baada ya mke wangu kunichoma kisu, utumbo ulikuwa umetoka ukining'inia na lengo lake alikuwa akitaka akimbie na utumbo wangu. Nilimbana mgongoni. Nikamkamata mguu nikamrusha sebuleni.

"Watoto walikuwa wamelala. Huku nje majirani walikuwa wakimwambia afungue mlango alikuwa akigoma. Baadae alifungua mlango. Majirani waliingia. Walijua ni jeraha dogo. Walichukua ule utumbo wangu. Wakanipeleka hospitali" Faruku Mhamadi, Mkazi wa Mkoani Kagera, Aliyechomwa kisu na mkewe.

Chanzo ni kumnyima tendo la ndoa
"Yule Mwanamke niliishi naye miaka Sita kwenye ndoa. Na ilipokuwa ikitokea tatizo alikuwa akikimbilia kwao. Nikasema hapa huyu ameshanichoka. Baada ya Miezi Tisa niliamua kuoa mke mwingine. Aliniachia watoto. Nilikuwa nahangaika peke yangu. Baadae ulitokea msiba wa Baba yangu mzazi. Sikuwa na Mahusiano naye mwaka mmoja na miezi Mitano alikuwa na maisha yake na Mimi nina yangu. Taarifa za msiba nilimpa kuwa Baba amefariki. Alikuja msibani. Baada ya matanga. Aliniambia anataka arudi nyumbani ili alee watoto wake.

Na wakati huo tayari nilikuwa nimeoa na nina mke mwingine. Baadae wazazi walitushauri. Baadae nilimwambia aondoke nitamfuata. Aliporudi siku ya pili nilikwenda kwao. Tukizungumza. Alirudi nyumbani. Siku ya pili nilimuita. Nikamwambia kwamba ajitambue kwamba amerudi kwenye ndoa yake. Nikamuuliza kuhusu Mahusiano yake. Alikuwa na simu ina lakini mbili Ile laini nyingine alikuwa akifanya mawasiliano yake, halafu anachomoa. Kumbe kule alipokuwa alikuwa na mwanaume. Kuna siku, simu yake iliita, nilipokea. Alipiga mwanaume. Alikuwa akilalamika.

Baadae nilimwambia anayempigia simu hakuwepo. Nilimwambia nikifika nyumbani nitampatia simu azungumze naye. Akaniambia kwanini napokea simu ambayo sio yangu?

"Baada ya Ile simu mzozo uliendelea. Aliahidi hataendelea naye lakini walikuwa wakiwasiliana kisirisiri. Baadae nikamwambia hatutashirikiana kimwili. Nilikuwa nalala na bukta yangu na tulikuwa kama Kaka na dada. Yeye alikasirika na hiyo ndio ilikuwa chanzo cha kunichoma kisu" Faruku Mhamadi Mkazi wa Mkoani Kagera, Aliyechomwa kisu na mkewe.

Aliyenichoma kisu bado yupo uraiani
"Huyu mke wangu aliyenichoma kisu hadi leo hajatiwa nguvuni na yupo kijijini. Alipelekwa kwenye vyombo vya sheria lakini alitolewa kwa dhamana na ndugu zake walidanganya kuwa mke wangu atoke ili aniuguze.

"Alitoka kwa dhamana baada ya wiki moja aliolewa na yule mwanaume wake. Sijawahi kuitwa mahakamani hadi Leo. Nipo tayari kurudi mahakamani na kutoa ushahidi" Faruku Mhamadi, Mkazi wa Mkoa wa Kagera.

Baada ya kuchomwa kisu siwezi kufanya kazi
"Namshukuru Sana Rais Samia Suluhu Hassan, ilikuwa Mwezi wa Sita mwaka Jana 2022. Alipohutubia kuhusu ishu ya haki kwa wote na kufungua njia Kwa kila Mtanzania. Kuna wakati niliomba kufa. Ndugu zangu wakanisaidia hadi mwandishi wa habari wa CLOUDS alipofika nyumbani kwangu kunihoji na kunitangaza. Mpaka nilipoanza safari ya kufika Muhimbili kutoka mkoani Kagera.

"Kiukweli nimehudumiwa vizuri pale hospitali ya Muhimbili. Niliomba ripoti ya matibabu nilipewa, gharama iliyotumika ya matibabu ni Mil. 13. Nawashukuru Sana Watanzania kwa michango yao. Niliambiwa nirudi tena Muhimbili baada ya mwaka mmoja.

Naendelea vizuri sana. Lakini nahitaji msaada zaidi kwa sababu siwezi kufanya kazi. Kwa msaada ni M PESA 0759 420 135 Jina Faruku Mhamadi" Faruku Mhamadi, Mkazi wa Mkoa wa Kagera.

Chanzo: Clouds TV
 
 
Jamaa story yake nimeisoma kidogo kuna vitu haviko sawa ni vi
Screenshot_20230331-110638_Instagram.jpg
 

Attachments

  • Screenshot_20230331-110546_Instagram.jpg
    Screenshot_20230331-110546_Instagram.jpg
    315.3 KB · Views: 13
  • Screenshot_20230331-110712_Instagram.jpg
    Screenshot_20230331-110712_Instagram.jpg
    417.4 KB · Views: 8
  • Screenshot_20230331-110725_Instagram.jpg
    Screenshot_20230331-110725_Instagram.jpg
    329.5 KB · Views: 4
  • Screenshot_20230331-110740_Instagram.jpg
    Screenshot_20230331-110740_Instagram.jpg
    397.7 KB · Views: 7
Kuna stori ya upande wa pili alitakiwa kuisema. Naamini mke wake sio kichaa aamke amchome kisu bila sababu. Lazima uvumilivu uliisha kutokana na matendo flani.

Wanaume tukumbuke kwamba wanawake nao ni binadamu wanapata hasira pia kwa mambo kama usaliti n.k
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom