Mke wangu na "Mheshimiwa Mbowe!"

yaani huyo sista wangu nimempenda sana. Asante kutuletea hili,maana hata mie nilishaanzisha hili kwa shem wako.
In one car sasa hivi, mambo ya kila mtu na gari wakati wote mwaelekea mjini hakuna. After all ni kwa faida yetu sote na familia nzima.
 
Sijakosea jukwaa maana kuna walioanza kununa, mwezenu nyumbani kumeanza kuwa kuchungu baada ya wifi yenu kuanza visa baada ya vikao vya bunge kuanza. Wiki ya kwanza alianza kama utani eti anataka kupendekeza baba kivuli ili awe ananikosoa na kutoa mtazamo mbadala kwa masuala yetu pale nyumbani. Hili nililipinga kwa nguvu zote kwa kuwa sikuwa na uhakika na hadidu za rejea za baba kivuli, wiki iliyofuata akaanza kupinga posho zangu na misafara mikubwa ya marafiki ninapokwenda bar. Nikidhani itaishia hapo sasa baada kiongozi wa upinzani bungeni kurudisha shangingi lake, yeye sasa ndio amekuja na kali eti anataka kupiga bei ka vitz kake ili tuwe tunapanda gari moja kwenda na kurudi kazini sasa mimi hapo naona kama uhuru wangu unaelekea kunitupa mkono, Nifanyeje wandugu kwa hatua za mwanzo nimepiga marufuku bunge nyumbani kwangu.
Nimefurahi kujua mkeo ana vitz.
 
Tatizo ni huko kubana matumizi kunakoingilia uhuru wangu bana, nilikuwa nitoka kazini napaki pale New Afrika hotel wakati wa Happy Hour sasa hivi hii yote itapeperuka halafu kuna dada jirani nilikuwa namsaidia sana lifti maana yeye ndio kaanza tu kazi sasa wife si atakuwa anambana.

Ecoli aliyekwambia ukioa unabaki na uhuru wako ni nani??
 
babu mi ndo nafanya shortlisting ya baba kivuli hapa, kivuli chako kina urefu na upana wa kutosha kukinga jua na mwezi 24/7?
Uzuri wa baba kivuli, si lazima awe na pesa....ukiwa mwongeaji mzuri na kupangilia hoja zako vizuri kama afanyavyo Mbowe, inshallah unatunukiwa nafasi.........Hebu nijaribu tuone.
 
kwa hiyo qualification yako ni pennyless na maneno kibao? hakuna majaribio hapa babu,job agency inahuika
Uzuri wa baba kivuli, si lazima awe na pesa....ukiwa mwongeaji mzuri na kupangilia hoja zako vizuri kama afanyavyo Mbowe, inshallah unatunukiwa nafasi.........Hebu nijaribu tuone.
 
Huo msaada unaotoa kwa huyo mdada umenikumbusha kauli ya Pinda kuwa kunawa wananchi nje ya majengo ya bunge wanawasubiri na kuwaomba pesa wabunge, so pesa za posho ndo zinafanya kazi hiyo lol' binafsi yangu naunga mkono hoja ya kiongozi wa upinzani nyumbani na ili mwende sawa ni lazima ufanye siasa shirikishi ili uweze kuakomodeti matakwa ya wengine
 
Ukiona mwanaupinzani kaamua ivyo ujue kuna mahali ulianza kufisadi muda wa kukaa na familia. Unatoka alfajiri watoto wamelala, ukirud ucku wa manane wamelala tena na ni mfumo huo kila cku, unataka afanyeje huyo mama zaidi ya kuweka baba kivuli wa kuacomodate psychological needs kwa watoto na physiological kwa mama? I knw hzo pombe sio chai ukifika ur third limb haiwezi kutoa umeme......! Cant imagne house boy atakavokuwa ba kivuli....
 
mmmh nimecheka bila kutarajia, anyway vigezo na masharti ya kuchagua "baba kivuli" ni yepi? maana mmmmh......
 
kwani we ecol upo kambi ya CCM??coz mkeo tayari mpinzani...jivue gamba bana!!
 
Sijakosea jukwaa maana kuna walioanza kununa, mwezenu nyumbani kumeanza kuwa kuchungu baada ya wifi yenu kuanza visa baada ya vikao vya bunge kuanza. Wiki ya kwanza alianza kama utani eti anataka kupendekeza baba kivuli ili awe ananikosoa na kutoa mtazamo mbadala kwa masuala yetu pale nyumbani. Hili nililipinga kwa nguvu zote kwa kuwa sikuwa na uhakika na hadidu za rejea za baba kivuli, wiki iliyofuata akaanza kupinga posho zangu na misafara mikubwa ya marafiki ninapokwenda bar. Nikidhani itaishia hapo sasa baada kiongozi wa upinzani bungeni kurudisha shangingi lake, yeye sasa ndio amekuja na kali eti anataka kupiga bei ka vitz kake ili tuwe tunapanda gari moja kwenda na kurudi kazini sasa mimi hapo naona kama uhuru wangu unaelekea kunitupa mkono, Nifanyeje wandugu kwa hatua za mwanzo nimepiga marufuku bunge nyumbani kwangu.

Nampa hongera sana huyo mke wako.....amewaza jinsi gani ya kukupata, ameona aje na gia ya kubana matumizi!! Kwanini unaogopa hivyo kutembea na mke wako kama huna agenda za siri????!!!!
 
Taratiibu mwana kwetu sasa Somalia tena!!!nikushauri utumie socialist demokrasi badala ya ile ya kiliberali...itakusaidia kuown enterprises muhimu za wapinzani
 
Duh, hii kali sana, ijumaa yangu itakuwa safi kweli kumbe hawa akina mama wako kama Mbowe eeeh, ndio maana jana nimenuniwa home kisa eti housegirl wetu ambaye aliondoka tu mwenyewe kaja jana usiku, hana sababu ya msingi iliyomleta, mara nikashtukia nimeitwa chumbani, kufika naulizwa kafwata nini huyu?? nilishtuka ila nikajibu kwa ujasiri na hekima tu kuwa, ni vyema tukamuulize yeye na sio mimi!!!
 
Ecoli, asikwambie kitu huyo ana'jitafutia umaarufu' tu.

Wewe mwambie sio abane usafiri tu, zile pesa za posho za saloon ndio zing'oke mwanzo na pesa za mchango wa kitchen party zifuatie haraka sana
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom