Mke wangu aliandaa tukio la mwanangu kubakwa na kulawitiwa na mchepuko wake

Mashaurijr

JF-Expert Member
Oct 8, 2016
639
1,020
Siku hiyo nilikuwa kazini. Mke wangu alibaki nyumbani na mwanangu wa kike wa miaka 11 . Sasa ilipofika muda wa saa 11 mke wangu alitoka na kumwaga mwanangu kuwa anakwenda dukani bila mwanangu kujua kule ndani tayari mchepuko wa mke wangu alikuwa amejificha ndani.

Baada ya mke wangu kuondoka mchepuko alimvizia mwanangu akiwa amejifunika uso na kumvizia mwanangu na kumfunika uso pia na kumfunga mdomo na kumfanyia ukatili huo na kisha kutokomea . Mke wangu hakurudi wakati ule alivizia nirudi wa kwanza nilivyorudi kazini na kuingia ndani niliita nisipate kukaribishwa na yeyote zaidi ya kusikia mtu akijizungusha na kutikisa kitanda chumbani kwangu. Nikatoka pale sebuleni na kuingia chumbani kwangu nikamkuta mwanangu akiwa uchi wa mnyama. Akiwa amefungwa mikono na na mdomo na macho pia. Nilienda haraka kumfungua na hapo ndio mke wangu akaingia ghafla na pale pale kuanza kunishutumu kwa kumbaka na kumlawiti mwanangu. Nilipata maumivu makali sana ndani ya moyo wangu ambayo sijawahi kupata ya kiasi hicho tangu nizaliwe . Nilimweleza sana lakini hakunielewa .

Mke wangu Akanishtaki polisi. Haikuchukua muda mrefu nikakamatwa nikachekwa na kutukanwa na kila mtu. Sio magazeti wala vyombo vya habari au mitandao ya kijamii vilivyobaki nyuma kunitukana na kuniona mchafu na nisiyefaa. Hakika ulikuwa wakati mgumu sana ambao haujawahi kutokea kwenye maisha yangu.
Siku haziku kawia sana nilipandishwa kizimbani nikajitetea sana lakini hakuna aliyenisikiliza. Nikahukumiwa miaka 30 gerezani. Sikuwa na namna zaidi ya kumwachia Mungu kila kitu.

Mke wangu akamchukua mchepuko wake waanza kuponda mali zangu . Wakienda club na sehemu mbalimbali za starehe kwa kutumia gari yangu . Mimi nikiteseka na mateso makali ya gerezani. Haikupita hata siku moja gerezani bila macho yangu kumwaga machozi sio kwa sababu ya mateso ya gerezani hapana bali kwa uchungu mzito wa kesi niliyosingiziwa. Hakika hawa viumbe hawana huruma kabisa. Mwanangu aliteseka sana alinyanyapaliwa hakupewa matunzo ya maana. Aliishi kwa kununua vyakula au kujipikia kwani mama alikuwa bize na mchepuko. Ni bahati tu mwanangu alikuwa na akaunti yake benki na nilikuwa namwekea fedha ndogo ndogo tokea akiwa mchanga hivyo kwenye fedha hakuishiwa na nilikuwa nimemfundisha nidhamu ya fedha.

Sasa mwaka jana mwanangu akiwa na miaka 16 sasa . Mke wangu na mchepuko wakawa wamerudi usiku na wakati huo mwanangu akiwa katoka kujisaidia muda wa saa nane usiku. Mke wangu na mchepuko siku hiyo walikuwa kwenye ugomvi mkali na walikuwa wamelewa sana . Ugomvi huo Kisa kilikuwa ni mchepuko kucheza na mwanamke mwingine ndipo mke wangu aliporopoka aliyoyafanyaga kwaajili ya huyo mchepuko ili wale raha alafu leo hii ana msaliti. Mke wangu alilalamika mwanangu akawa amesikia hilo kwani alitaja kabisa kuwa alinitengenezea kesi ili nifungwe ili wale raha na kumruhusu kumbaka mwanangu.

Mwanangu Aliumia sana baada ya kusikia hayo. Siku hiyo hakupata usingizi na wala hakujua aanzie wapi . Sasa kesho yake baada ya kufikiria sana aliamua kutokwenda shule na kusafiri kutoka dodoma mpaka dar es salaam kwa kaka yangu. Kaka alishangaa tu kumwona mwanangu ghafla na hawakuwahi kuwasiliana tokea nilipofungwa . Kaka alimpokea na ndipo mwanangu alipomweleza kaka kila kitu huku akilia sana . Kaka naye alikosa uvumilivu na kuanza kulia pia.

Hawakuwa na jinsi zaidi ya kuanza harakati na kukusanya ushahidi wa hilo na mwanangu anasema hata alipo bakwa hakutegemea angekuwa baba yake kwani baba yake ni mnene ila aliyembaka hakuwa mnene . Na hilo lilikuwa linamuumiza kichwa tokea akiwa na miaka 11.

Basi mtoto kesho yake alirudi dodoma baada ya kupangana na kaka yangu .hata aliporudi hakuna aliyemuuliza ulikuwa wapi na huenda hata hakuna aliyetambua kama alisafiri kwani walimtelekeza kabisa mwanangu. Mwanangu akawa makini kukusanya zaidi ushaidi wa kutosha akiwasubiri wakirudi usiku na kusogea karibu na mlangoni kwao kurekodi mazungumzo.

Alirekodi mengi sana ila baada ya kama wiki tatu ndipo alipopata ushahidi wenye mashiko kuhusu ubakaji aliofanyiwa. Zaidi kaka alisafiri na kupanga chumba jirani na nyumbani kwangu ili kumpanga mwanangu.

Kaka aliamua kumtumia mwangu kumhadaa kimapenzi mchepuko wa mke wangu . Mchepuko kweli aliingia kingi akiamini mwanangu amempenda na hajui chochote . Sasa siku moja mwanangu na mchepuko wakapanga wakafanye mapenzi. Huo ulikuwa mpango wa kaka na kaka alikuwa karibu ndani nyumbani.

Mchepuko siku hiyo alijifanya mgonjwa na kubaki nyumbani mke wangu akienda kwenye biashara. Baada ya muda tu mchepuko aliingia kwenye chumba cha mwanangu na kaka alikuwa amejibanza kurekodi maongezi. Mwanangu aliamua kumfungukia mchepuko kuwa yeye anampenda licha ya kuwa anajua kabisa yeye ndiye aliyembaka na sio baba. Kaka alikuwa amemwandaa vizuri mwanangu hivyo. Jamaa aliamini kweli amependwa.

Jamaa alishtuka lakini kwa tabasamu la mwanangu na uzuri wake alijikuta akikubali hilo . Mwanangu akianza na mbwembwe za kuwa akimpa basi sharti amwache mama. Kaka alimpanga vizuri ili kupata ushahidi wenye mashiko na kweli ulipatikana kaka akajitokeza.

Na kumpiga ngumi moja jamaa akiwa bado kwenye wenge akamshika na kumfunga mikono kisha akatoka na mwanangu na kuwaita polisi na kesi ikaanza . Mke wangu pia akakamatwa na Ukweli wote ukajulikana wakabaki wao jela mimi sasa ndio nikawa huru.

Ningumu kusamehe. Ila najitahidi nimsamehe mke wangu na mchepuko wake ili tu kuokoa roho yangu. Kwa sasa naishi na mwanangu tunapendana sana . Kwa tuliyopitia kuna wakati tukikumbuka utatukuta tunalia sana.

Pia kwasasa nina mpango wa kuoa rasmi yule hatukuwa tumefunga ndoa kanisani ila wa sasa tutafunga ndoa na kuanza maisha mapya ya kumpendeza Mungu.
Kisa kimeandikwa na
Mashaurijr.
Assenga
 
Siku hiyo nilikuwa kazini. Mke wangu alibaki nyumbani na mwanangu wa kike wa miaka 11 . Sasa ilipofika muda wa saa 11 mke wangu alitoka na kumwaga mwanangu kuwa anakwenda dukani bila mwanangu kujua kule ndani tayari mchepuko wa mke wangu alikuwa amejificha ndani.

Assenga
Pole kwa yote mkuu. Kusamehe ni jambo la hiari, ila ikitokea umepata moyo wa kusamehe itakuwa vizuri Kwa ajili ya afya ya moyo wako.
 
Siku hiyo nilikuwa kazini. Mke wangu alibaki nyumbani na mwanangu wa kike wa miaka 11 . Sasa ilipofika muda wa saa 11 mke wangu alitoka na kumwaga mwanangu kuwa anakwenda dukani bila mwanangu kujua kule ndani tayari mchepuko wa mke wangu alikuwa amejificha ndani.

Baada ya mke wangu kuondoka mchepuko alimvizia mwanangu akiwa amejifunika uso na kumvizia mwanangu na
Assenga
Aseee
 
Hii dunia sijui inaelekea wapi. Kila kile ambacho kilikuwa kinachukuliwa takatifu sasa kinachezewa. Ndoa haziheshimiki, maisha hayashemiki hizo dini ndio zimekuwa za kuchezea kabisa.

Pesa na mali ndio vimeshika hatamu.

Mungu atunusuru na kutupa mwisho mwema.
 
Siku hiyo nilikuwa kazini. Mke wangu alibaki nyumbani na mwanangu wa kike wa miaka 11 . Sasa ilipofika muda wa saa 11 mke wangu alitoka na kumwaga mwanangu kuwa anakwenda dukani bila mwanangu kujua kule ndani tayari mchepuko wa mke wangu alikuwa amejificha ndani.

Baada ya mke wangu kuondoka mchepuko alimvizia mwanangu akiwa amejifunika uso na kumvizia mwanangu na
Kisa kimeandikwa na
Mashaurijr.
Assenga
Kosea kujenga nyumba utaweza kuirekebisha ila usikosee kuoa Mke.
 
Japokuwa ni Chai, ila pamoja na kupigwa tukio na Mkeo wa zamani na kwenda kunyea Debe ila bado unaongelea KUOA tena

Teyari una mtoto bado unataka kuhangaika na Ndoa, Kuna watu wanapenda kuoa utadhani wao ndio walipewa agizo la kuja kuijaza Dunia

Ngoja uoe huyo mwingine yeye aje na mbinu ingine ya kukutoa Uhai ili abakie na mchepuko waendelee alipoishia mke wa Kwanza
 
Back
Top Bottom