Mke wa Mbunge Lema ashtakiwa kwa kumtumia ujumbe Mkuu wa Mkoa wenye neno 'Shoga'

Kwa lipi? Kwani mtu akisema wewe na Chabruma ni mashoga wa muda mrefu kwa sababu kila usemacho wewe au asemacho yeye lazima mpeane support atakuwa katukana?
Msiwe na mawazo kama ya Wassira wakati ule alipopigana ukumbi wa Habari maelezo alipoambiwa yeye ni shogaake mkubwa na Mrema walipokuwa NCCR. Lakini baada ya kupewa maelezo ya maana sahihi ya shoga alitulia.
Tangu lini mwanamke akiwa na shoga mwanaume? Atuambie bayana kuwa huyo Gambo ni mchepuko wake! Asitumie tafsida kumfumba Lema
 
Wasira hakuambiwa ni shoga wa Mrema! aliambiwa ni SWAHIBA sasa akawa hajui maana ya swahiba ndio akatembeza mkono
 
Tangu lini mwanamke akiwa na shoga mwanaume? Atuambie bayana kuwa huyo Gambo ni mchepuko wake! Asitumie tafsida kumfumba Lema
Mbona Jenister na Masaju ni marafiki aka mashoga haushangai? Au wewe unadhani urafiki ni uchepukaji tuu? Utakuwa una tabia mbaya wewe!
 
Hilo ndo la kujiuliza. Halafu anasema kuwa wamekuwa wakiwasiliana mara kwa mara. Hivi Lema anajisikiaje kusikia mkewe akisema hayo? Kwa nini hashtuki?

Mkuu labda mtego ndio upo hapo. Huenda mke wa Lema anaashiria kwamba yupo tayari kutoa ushirikiano ili hayo mawasiliano kati yake na mkuu wa mkoa yawekwe wazi. Swali ni je upande wa mashtaka utakuwa tayari kwa hilo?
 
..this is just STUPID.

..mkuu wa mkoa anashtakiana na wake wa viongozi wenzake?

..Arusha inahitaji mkuu wa mkoa ambaye ni mtu mzima mwenye heshima zake.
 
Tafuta tafsiri ya neno SHOGA katika kamusi hayo mengine yako
Wanafikiri mahakama itaangalia maana ya mitaani.

Gambo anajidhalilisha mwenyewe. Kama mahakama ikichukua maana ya mitaani, itambidi Gambo athibitishe yeye siyo shoga kwa maana anayoitaka vinginevyo hakuna kesi pale.
 
..this is just STUPID.

..mkuu wa mkoa anashtakiana na wake wa viongozi wenzake?

..Arusha inahitaji mkuu wa mkoa ambaye ni mtu mzima mwenye heshima zake.
Mecky Sadick alikuwa anafaa sana Arusha sasa rais kwa kuendeshwa na mihemuko ya kisiasa ili kuwakomoa wapinzani anapeleka watu waliokataliwa kwenye jamii.
 
Alutta continua! continua!

13528718_738782559596571_6772389937267433792_n-jpg.427710
Mbona unajishushia hadhi kiasi hiki?
 
Wanafikiri mahakama itaangalia maana ya mitaani.

Gambo anajidhalilisha mwenyewe. Kama mahakama ikichukua maana ya mitaani, itambidi Gambo athibitishe yeye siyo shoga kwa maana anayoitaka vinginevyo hakuna kesi pale.
una maana itabidi ifanyike physical examination?
 
Back
Top Bottom